KAGERA WAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU KATIKA MIJI YA BUKOBA NA DAR ES SALAAM
Maadhimisho ya miaka hamsini (50) ya Uhuru wa Tanzania Bara mkoani Kagera yameadhimishwa rasmi kuanzia tarehe 28/11/2011 katika viwanja vya Kyakailabwa nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
Pichani kanali mstaafu Fabian I. Massawe akizindua kitabu cha miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania Bara mkoa wa Kagera katika maadhimisho hayo.