• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
KAGERA REGIONAL WEBSITE

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na SerikaliI za Mitaa Mkoa wa Kagera

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu/Vitengo
      • Sehemu
        • Mamlaka za Serikali za Mitaa
        • Miundombinu
        • Elimu
          • Elimu ya Msingi
          • Elimu ya Sekondari
          • Elimu ya Watu Wazima
          • Elimu ya Juu
          • Michezo
          • Vijana
        • Afya
          • Afya
          • Ustawi wa Jamii
        • Utawala na Rasilimali Watu
        • Mipango na Uratibu
          • Mipango
          • Takwimu
          • Maendeleo ya Jamii
          • TASAF
        • Uchumi na Uzalishaji
          • Kilimo cha Umwagiliaji
          • Viwanda na Biashara
          • Uvuvi
          • Mifugo
          • Maliasili, Utalii na Mazingira
          • Ushirika
          • Kilimo
        • Maji
      • Vitengo
        • TEHAMA
        • Sheria
        • Fedha na Uhasibu
        • Ukaguzi wa Ndani
        • Ugavi
  • Wilaya
    • Bukoba
      • Viongozi wa Bukoba
    • Biharamulo
      • Viongozi wa Biharamulo
    • Karagwe
      • Viongozi wa Karagwe
    • Kyerwa
      • Viongozi wa Kyerwa
    • Missenyi
      • Viongozi wa Missenyi
    • Muleba
      • Viongozi wa Muleba
    • Ngara
      • Viongozi wa Ngara
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Misseny
    • Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ngara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Fursa za Ufugaji
    • Fursa za Kilimo
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Ufugaji
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Jarida
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali

Historia

HISTORIA YA MKOA WA KAGERA




CHIMBUKO AU ASILI YA MKOA WA KAGERA

Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la Mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliyounda Jimbo lililoitwa “Lake Province”. Jimbo hili lilijumuisha Wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region’ (Ziwa Magharibi) na kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba. Jina hili (Ziwa Magharibi) lilidumu katika kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru mwaka 1961 mpaka mwaka 1979 baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda (Vita ya Kagera).

Mkoa ulipata jina la Kagera kutokana na Mto Kagera zamani ukijulikana kama “Akagera” ambao hutiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia Kaskazini na kumwaga maji yake katika ziwa Victoria

UKUBWA WA MKOA NA MAHALI ULIPO

Mkoa wa Kagera unapatikana Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Tanzania. Makao Makuu ya Mkoa yapo katika mji wa Bukoba umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam, Mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa Magharibi,Mikoa ya Geita na Kigoma,  kwa upande wa Kusini. Pia Mkoa wa Kagera unapakana na  Ziwa Victoria kwa upande wa Mashariki ambapo kwa ndani ya Ziwa hilo mkoa unapakana na Mikoa ya Geita, Mwanza na Mara. Vile vile Mkoa wa Kagera uko Kusini mwa Ikweta kati ya Latitude 1 “00” na 2”45”. Mashariki mwa ‘Greenwich' katika Longitudi 30”25” na 32”40”

Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la Kilomita za mraba 35,686 kati ya hizo Kilomita za Mraba 25,513 ni eneo la nchi kavu ambalo ni sawa na asilimia 73 ya eneo lote la Mkoa na kilomita za mraba 10,173 ni eneo la maji sawa na asilimia 27. Mkoa una visiwa vikubwa katika Ziwa Victoria ambavyo ni Bumbire, Iroba, Kelebe, Goziba, Ikuuza na Mhutwe na visiwa vingine vidogo jumla vikiwa 27 vinavyokaliwa na watu na jumla ya visiwa 21 vidogo vidogo visivyokaliwa na watu.  Ukiacha mbali Wilaya ya Biharamulo ambayo ni tambarare, sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga. Upande wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika Mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika Ziwa Victoria. 

Mwinuko wa nchi (altitude) ni kati ya mita 1,100 na 1,800 juu ya usawa wa Bahari. Mchanganuo wa kilomita za mraba kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo: - Halmashauri ya Wilaya Biharamulo (5,627 km2), Halmashauri ya Wilaya Bukoba (5,071 km2), Bukoba Manispaa (80km2), Halmashauri ya Wilaya Karagwe (4,630 km2), Halmashauri ya Wilaya Kyerwa (3,086 km2), Halmashauri ya Wilaya Missenyi (2,709 km2), Halmashauri ya Wilaya Muleba (10,739 km2), na Halmashauri ya Wilaya Ngara (3,744 km2).

MUUNDO WA KIUTAWALA

Kiutawala Mkoa wa Kagera umegawanyika katika Wilaya Saba (7) ambazo ni Biharamulo, Bukoba, Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Ngara. Mkoa una Halmashauri za wilaya 7 na ya Manispaa moja (1), Tarafa 27, Kata 192, Vijiji vilivyosajiliwa 662, Mitaa 66 na Vitongoji 3,728. Aidha, Mkoa una Majimbo tisa (9) ya uchaguzi.

IDADI YA WATU

Mkoa wa Kagera una jumla ya watu 2,458,023 wanawake 1,252,340 na Wanaume 1,205,683 (sensa ya Mwaka 2012) Aidha, Pato la Mkoa wa Kagera ni Shilingi 1,760,458 ambapo pato la mwananchi mmoja mmoja ni Shilingi 716,209 (NBS Tanzania 2012) kwa mwaka.

WATU WA MKOA WA KAGERA

Kabla na baada ya kuja kwa wakoloni Mkoa wa Kagera ulikuwa na utawala wa Kimila (Chiefdoms) uliogawanyika katika himaya 8. Himaya hizo ni pamoja na Kyamutwara, Kihanja (Kanazi), Kiziba, Ihangiro, Bugabo, Karagwe, Biharamulo (Rusubi) na Maruku (Bukara).

Baadhi ya Watemi waliotawala himaya hizo ni pamoja na Emmanuel Rukamba (Kyamtwara), Rumanyika (Karagwe), Kasusura (Biharamulo), Lugomola (Bukara), Rutinwa (Kiziba), Kayo za (Bugabo), Kahigi (Kihanja) na Nyarubamba (Ihangiro). Kila mtemi alikuwa na walinzi wake walioitwa Warugaruga.

Makabila yanayopatikana hivi sasa katika mkoa wa Kagera ni pamoja na Wahaya ambao wanapatikana zaidi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Missenyi. Makabila mengine ni Wanyambo, wanaopatikana katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa, Wasubi katika wilaya ya Biharamulo, Wahangaza wanaopatikana katika Wilaya ya Ngara. Pia kuna Waha, Wazinza and Warongo.

Baada ya kuja kwa wazungu waliongeza ulimaji wa kahawa kama zao la biashara lililowasaidia kujiongezea kipato. Wakazi wa asili ya Kagera ni wabantu na wengi wao wanaasili ya Bunyoro. Wanaongea lugha sawa na ile ya Wanyoro, Wanyankole, Watoro na Wakiga. Busubi na Bugufi wana lugha na desturi sawa na Watusi, Wahutu na Waha. Lakini makabila hayo ni ya Wabantu wa Ziwa (Interlacustrine Bantu) na yanafanana mila na desturi.

Makundi hayo yaligawanyika katiya wachungaji (Bahima) ambao walitawala na wakulima (Bairu) ambao walitawaliwa na mara nyingi kudharauliwa. Bahima (Balangira) walikuwa na koo chache zipatazo 20 na walitawaliwa na Wahinda, Wabito na Wankango Bairu walikuwa na koo kama 130 zenye mashina 24 ambayo kiasili walikuwa Bairu lakini kwa kuoa katika Bahima au kufanya kazi kwa Watemi walipandishwa hadhi na kuwa Bahima (Batware). Kila ukoo uliitwa jina la Baba mwanzilishi wake na kina ukoo ulikuwa na kitu walichokatazwa kula (Omuziro) na mnyama walioshirikishwa nae (Ekyerumono).

HALI YA HEWA

Hali ya hewa ya Mkoa wa Kagera kwa ujumla ni ya joto la wastani wa 26.02 sentigredi. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800-1,100 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei. Mvua hizi ndizo zinazowezesha kuwepo kwauoto wa asili wa kuvutia katika maeneo mengi ya mkoa. Kwa miaka ya kawaida mkoa hupata mvua za uhakika za vuli na masika ambazo ni muhium kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Uchumi wa wenyeji wa mkoa wa Kagera ulijikita katika mashamba ya migomba na kahawa. Chakula chao kikuu ni ndizi katika aina zake mbalimbali. Katika mashamba yao hulima mazao mengine kufuatana na msimu. Mazao hayo ni pamoja na maharage, mihogo, mahindi na mboga.

ORODHA YA WAKUU WA MKOA WA KAGERA TANGU UHURU MWAKA 1961 HADI SASA

NA.
PICHA
JINA KAMILI

MWAKA WA KUINGIA

MWAKA WA KUTOKA

1.

Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti

2018
-

2.



 Maj. Gen.(Mst) Salum M. Kijuu


2016


2018

3.



 Bw. John V.K. Mongella


2014 


2016

4.



 Col. (Mst) Fabian I. Massawe           


2011


2014

5.



 Bw. Mohammed A. Babu         


2009


2011

6.



 Col. Enos Mfuru


2006


2009

7.


Gen. T. N. Kiwelu


1999



2006

8.



 Bw. Mohammed A. Babu


1996


1999

9.



 Bw. Philip J. Mangula


1993


1996

10.

 


 Capt. A. M. Kiwanuka             

1991

1993

11.


 
 Bw. Paul Kimiti                       


1989


1991

12.



 Bw. Horace Kolimba


1987


1989

13.

 


 Lt. Col. Nsa Kaisi                     

1981

1987

14.



 Capt. Peter  Kafanabo            


1978


1981

15.

 



 Bw. Mohamed Kisoki

1977

1978

16.



 Col. T. A. SIMBA


1975


1977

17.

 


 Brig. M. M. Marwa

1974

1975

18.



 Maj. Gen. Twalipo


1972


1974

19.

 


 BW. L. N. Sijaona

1970

1972

20.

 


 BW. P. C. Semshanga

1967

1970

21.

 


 Bw. P. C. Walwa

1966

1967

22.

 


 BW. Osward Marwa       

1964

1966

23.


 
Bw. Samwel N. Lwangisa


1961


1964

 

Matangazo

  • Mko wa Kagera Unaandaa Wiki ya Uwekezaji Lengo Kuu likiwa ni Kutangaza Fursa za mkoa wa Kagera ili Kuinua uchumi wa wananchi na mkoa kwa ujumla. Wiki hiyo itaanza tarehe 12 hadi 17 Agosti, 2019 July 01, 2019
  • Wanafunzi wa Darasa la VII Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka 2019 Mkoani Kagera. December 21, 2018
  • Wanafunzi wa Darasa la VII Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato Cha Kwanza Mwaka 2018 Mkoani Kagera. December 20, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Kagera Azindua Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru Na 57 ya Jamhuri Kwa Kuwaongoza Wananchi Kufanya Usafi na Kujitolea Kuchangia Damu

    December 04, 2019
  • Profesa Ndalichako Azindua Chuo Cha VETA Ndolage Aagiza Uongozi wa VETA Kukamilisha Miundombinu ya Chuo Hicho Kwa Gharama Zao Wenyewe

    November 27, 2019
  • Mkuu wa Mkoa Awachukulia Hatua Wasimamizi wa Miradi ya Ukarabati wa Shule Kongwe Kwa Uzembe Ampiga Stop Mkandarasi wa Barabara Manispaa ya Bukoba Kutotoka Nje ya Mkoa

    November 21, 2019
  • Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Nchini Awasili Mkoani Kagera Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Tatu Kutatua Changamoto Mbalimbali za Uhamiaji

    November 13, 2019
  • Tazama zote

Video

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Akizindua Wiki ya Uwekezaji Kagera Agosti 14, 2019
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Taratibu za biashara ya ndani
  • Barabara Kuu na ndogo za Mkoa
  • Vituo vya Redio Katika Mkoa wa Kagera
  • Wakuu wa Mkoa wa Kagera Tangu Uhuru Mwaka 1961
  • Matokeo ya Darasa la VII 2018, Wanafunzi 10 Bora, Shule 10 Bora, Watakaojiunga Kidato cha I, 2019
  • Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera 2019
  • FOMU YA USAJILI WA WAFANYABIASAHARA NA WADAU WA MKOA WA KAGERA, ZIARA YA KUTEMBELEA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KWA LENGO LA KUTAFUTA FURSA ZA BIASHARA NA UWEKEZAJI NOVEMBER, 2019.

Tovuti Mashuhuri

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Takwimu Huria

Wafuatiliaji Kimataifa

world map hits counter

Kaunta ya Wageni

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera

    Anwani: S.L.P 299 BUKOBA

    Simu ya Mezani: 255 28 2220215/17

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras.kagera@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu
    • Hakimiliki

Haki zote zimehifadhiwa