JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
 
 
     
AFYA
 
Afya [ nyumbani ] au
 
 
Utangulizi

Dira ya Sekta ya Afya ni kuinua hali ya afya na Ustawi wa wanainchi hasa wale walioko kwenye hatari zaidi (at risk) ya kuathiriwa na magonjwa, kwa kukuza na kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya utakaokidhi mahitaji ya wanainchi. Matarajio ni kutoa huduma muhimu za afya kwa gharama nafuu, zenye ubora na uwiano unaokubalika, zinazozingatia jinsia, endelevu na zinazolenga kuinua hali ya afya ya wanainchi wa Mkoa wa Kagera.

Katika kutoa huduma za afya Mkoa una jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 246, zikiwemo hospitali 13, Vituo vya afya 23na zahanati 210 (Angalia Jedwali Na. 1,2, na 3) Sekta ya afya ina jumla ya watumishi 2,063, lakini walio na taaluma ni 966. Mahitaji halisi ya watumishi wenye taaluma ni 1, 241; kwa hiyo kuna upungufu wa wataalamu 275 (Jedwali Na. 4) vitendea kazi muhimu ambavyo vipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na upungufu wake umeonyeshwa (Jedwali Na. 6) Uwiano wa wataalamu wa afya na Idadi ya watu umeonyeshwa (Jedwali Na. 5). Hali ya afya Mkoani inaonyesha kwamba Mkoa una matatizo ya magonjwa ya kuambukiza. Magonjwa kumi yanayoongoza ni:- Malaria, Magonjwa ya njia za hewa, magonjwa ya kuhara, “Pneumonia”, upungufu wa damu, Minyoo, “Surgical Conditions”, magonjwa ya njia za mkojo, UKIMWI, “Pregnancy Related Problems” (Jedwali Na. 7).

Magonjwa kumi yanayoongoza kwa kusababisha vifo ni; Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu, Upungufu wa damu, “Pneumonia”, Magonjwa ya moyo na shinikizo la damu, magonjwa ya njia za hewa, “Pelvic infections”, Kisukari, na Homa ya Uti wa Mgongo (Jedwali Na. 8) .


MALENGO

 

Kupunguza Vifo vya watoto

 

•  Kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja kutoka 99/1000 wanaozaliwa hai mpaka 85/1000.

•  Kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano kutoka 150/1000 wanaozaliwa hai mpaka 127/1000.

•  Mkakati mkubwa unaotumika ni kuinua kiwango cha chanjo zote kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja hadi asilimia 95.

•  Kutoa dawa za vitamin A (vitamin A Supplementation) kwa watoto chini ya miaka 5.

•  Mkakati mwingine ni kutekeleza mpango wa ”Intergrated Management of Childhood illness”ambao unahusika na tiba sahihi ya magonjwa ya malaria, kichomi, kuharisha, surua, upungufu wa damu na utapiamulo.

 

Kupunguza Vifo vya akina mama kutokana na uzazi

•  Kupunguza vifo vya akina mama kutokana na uzazi kutoka 529/100,000 hadi 450/100,000.

•  Mkakati muhimu ni kuinua kiwango cha wajawazito wanaojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kufikia asilimia 80.

•  Mkakati mwingine ni mpango wa ”Basic and Compressive Obstetric Care Including Emergency Obstetric Care”. Huu mpango unahusu Huduma za dharura kwa wajawazito.

Kudhibiti Ugonjwa wa Malaria

 

  Mkakati muhimu wa kudhibiti Malaria ni kutoa tiba sahihi ya Ugonjwa huu kwa asilimia 90 ya wagonjwa wa Malaria wanaofika katika Vituo vya tiba.

•  Mkakati mwingine ni kuhamasisha na kusambaza vyandarua viuatilifu ili vitumiwe na asilimia 75 ya wajawazito na watoto chini wa miaka mitano (voucher scheme).

•  Mkakati mwingine ni kunyunyizia dawa za ukoko majumbani katika wilaya zote kasoro Bukoba Manispaa.

Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma

•  Mkakati wa kudhibiti Kifua Kikuu ni kupunguza ugonjwa huu na vifo vinavyotokana nao kwa asilimia 50 kwa kutumia mpango wa ”DOTS” katika kutibu Kifua Kikuu. Mkakati wa kudhibiti Ukoma ni kwa kutumia mpango ”MDT” katika kutibu ugonjwa huo.

Kudhibiti UKIMWI

  Mikakati ya kudhibiti UKIMWI ni pamoja na kufikisha elimu kuhusu ugonjwa wa UKIMWI kwa wananchi hasa vijijini (HIV/AIDS awareness) kufikia asilimia 95.

•  Ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa Virusi vya UKIMWI kufikia asilimia 20 ya wananchi wenye umri kati ya miaka 15 na 49.

•  Kuzuia maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto.

•  Kutoa dawa za kurefusha maisha ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wapatao 30,000.

•  Kupunguza kasi ya maambukizo ya VVU/UKIMWI kutoka ya sasa ambayo ni 3.7 hadi 1.8.

 

 

MAGONJWA YA MLIPUKO

UGONJWA WA EBOLA

Mkoa umechukua tahadhari zote kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa huo kwa majirani zetu wa nchi ya Uganda.

Wananchi wetu wanaoishi sehemu za mpakani wameelimishwa kuhusu dalili za ugonjwa huo kwamba ni:

•  Homa kali

•  Kuumwa kichwa

•  Kutapika na kuharisha

•  Mwili kuishiwa nguvu

•  Kutokwa damu sehemu mbali mbali za mwili

•  Hatimaye kifo

Wananchi wameshauri wasipeane mikono na wageni au jamaa zao wanaotoka Uganda hususani maeneo ya mlipuko wa ugonjwa huo. Pia wameshauriwa kutoa taarifa kwenye Vituo vya huduma za Afya vilivyo karibu nao mara wanapoona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo. Mipaka yote na nchi jirani imezuia wagonjwa wa aina yoyote kupenyeza ndani ya nchi.

TAARIFA MBALIMBALI ZA AFYA

 

Idadi ya Zahanati na Umiliki wake.

 

 

Wilaya

Mmiliki

Jumla

Serikali

Serikali

Mashirika ya Dini

Mashirika ya Umma

Binafsi

Karagwe

37

5

2

1

45

Bukoba Manispaa

11

1

1

2

15

Bukoba Vijijini

41

8

1

5

55

Muleba

20

7

2

0

36

Biharamulo

25

3

-

2

30

Ngara

33

2

0

1

36

Jumla

167

25

6

12

210

 

Idadi ya Hospitali na Umiliki wake.

 

Wilaya

Mmiliki

Jumla

 

Serikali

Mashirika ya Dini

Mashirika ya Umma

Binafsi

Karagwe

0

3

0

0

3

Bukoba Manispaa

1

0

0

0

1

Bukoba Vijijini

0

1

1

0

2

Muleba

0

3

0

0

3

Biharamulo

1

1

0

0

2

Ngara

0

2

0

0

2

Jumla kimkoa

2

10

1

0

13

 

Rasilimali watu kwa baadhi ya taaluma katika sekta ya Afya, Mkoa wa Kagera, ikionyesha mapungufu

Taaluma

Mahitaji

Waliopo

Upungufu

% Pungufu

Madaktari Bingwa

8

2

6

75%

Madaktari

55

24

31

56%

Wauguzi wote

966

856

110

11%

Madaktari Meno

7

1

6

86%

Madaktari wasaidizi

68

18

50

74%

Wafamasia

8

4

4

50%

Radiografa

12

2

10

83%

Fundi Maabara

18

2

16

89%

Maafisa Tabibu

99

57

42

42%

Ujumla

1,241

966

275

22%

 

 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

MABORESHO KATIKA SEKTA YA AFYA

•  Lengo la mabadiliko katika sekta ya afya ni kuboresha huduma na kusambaza huduma za afya katika maeneo ya vijijini ambapo asilimia 80 ya wanainchi wanaishi.

•  Malengo mahususi ni pamoja na kutafuta vyanzo vipya vya fedha za kuendeshea huduma za afya, kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa na vifaa muhimu, kushirikisha sekta binafsi katika uendeshaji wa huduma za afya (Public- Private Partnership). Kuimarisha maendeleo ya watumishi wa ngazi zote katika sekta ya afya.

 
UTEKELEZAJI NA MAFANIKIO

 

Kupunguza Vifo vya Watoto

Kiwango cha chanjo zote kwa watoto chini ya umri wa mwaka mmoja kimeongezeka kutoka asilimia 91 (mwaka 2005) hadi asilimia 93 (mwaka 2006) . Katika kupunguza vifo vya watoto, halmashauri zote zinatekeleza mpango wa ”Intergrated Management of Childhood illness” ambao unahusika na kutibu magonjwa ya malaria, kichomi, kuharisha, surua, upungufu wa damu na utapiamulo. Vifo vya watoto wa umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 150/1000 mwaka 2000 hadi 112/2000 mwaka 2004 (Dermographic Health Survey of 2004)

Kupunguza Vifo vya akina mama vinavyotokana na Uzazi

Kiwango cha wajawazito waliojifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kimeongezeka kutoka asilimia 53.8 mwaka 2005 hadi asilimia 57 mwaka 2006. Katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi, halmashauri zote zinatekeleza mpango wa Huduma za dharura kwa wajawazito. Vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi vimepungua kutoka 135/100,000 mwaka 2005 hadi 118/100,000 mwaka 2006.

Kudhibiti ugonjwa wa Malaria

Kiwango cha wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano wanaotumia vyandarua viuatilifu kimeongezeka kutoka asilimia 35 mwaka 2003 hadi asilimia 68 mwaka 2006. Kiwango cha vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano kutokana na ugonjwa wa Malaria kimepungua kutoka asilimia 22.8 mwaka 2002 hadi asilimia 13 mwaka 2006. Aidha Mkoa haukupata mlipuko wa Malaria mwaka 2007 kama ilivyokuwa inatokea miaka ya 1998 hadi 2006.

Kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma.

Vituo vya tiba vinavyotumia ”Direct Observed Treatments” kwa ugonjwa wa Kifua Kikuu vimeongezeka kutoka 15 mwaka 2001 hadi 68 mwaka 2006. Idadi ya vituo vya tiba vinavyotumia ”Multi Drug Therapy” kwa ugonjwa wa Ukoma vimeongezeka kutoka 40 mwaka 2003 hadi 75 mwaka 2006.

Kudhibiti UKIMWI.

Mkoa umefikisha elimu kuhusu ugonjwa wa UKIMWI kwa wanainchi na kiwango cha ”HIV/AIDS awareness” kimeongezeka kutoka asilimia 75 mwaka 2004 hadi asilimia 95 mwaka 2006. Mkoa umeweza kutoa dawa za kurefusha maisha ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika hospitali nane. Kuanzia Mei 2005 hadi Desemba 2006 , jumla ya wagonjwa 2,619 walianzishiwa madawa kati ya watu 5,183 waliosajiliwa. Mkoa una vituo 18 vinavyotoa huduma za kuzuia maambukizo ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto (PMTCT) . Mkoa pia una vituo 43 vinavyotoa huduma za ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa viruzi vya UKIMWI.

Utafiti uliofanywa na TACAIDS mwaka 2004 uligundua kuwa kasi ya maambukizo ya Virusi vya UKIMWI (HIV Prevalence) ilikuwa asilimia 3.7 ukilinganisha ya kitaifa ambayo ni asilimia 7. Mkoa uliendesha kampeni ya Taifa ya upimaji wa Virusi vya UKIMWI kwa hiari kuanzia tarehe 22 Septemba 2007 hadi 26 Novemba, 2007. Matokeo ni kuwa wanainchi 172,768 kati ya walengwa 253,988 walipimwa sawa na asilimia 68. Aidha watu 6,514 kati ya watu 172,768 waliopimwa walikutwa na Virusi vya UKIMWI (HIV POSITIVE) sawa na asilimia 3.8.

Maboresho katika Sekta ya afya

Lengo la mabadiliko yanayofanyika katika Sekta ya afya ni kuboresha huduma na kusambaza huduma za afya katika maeneo ya vijijini ambapo asilimia 80 ya wanainchi wanaishi. Katika kutoa madaraka zaidi kwa halmashauri juu ya uendeshaji wa huduma za afya, Bodi za afya (Council Health Service Boards) na kamati za vituo vya afya na Zahanati zilianzishwa na kuimarishwa. Mpango wa ”Indent System” umeanzishwa katika halmashauri zote ili kuhakikisha kwamba dawa na vifaa muhimu vinapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya. Katika kutafuta vyanzo vipya vya fedha za kuendeshea huduma za afya Halmashauri ya Karagwe imeanzisha mfuko wa afya ya Jamii (Community Health Fund) . Aidha halmashauri zingine ziko kwenye hatua mbali mbali za kuanzisha mfuko huo wa afya ya jamii.

CHANGAMOTO

Mkoa unakabiliwa na matatizo yanayoathiri utoaji bora afya.

•  Mkoa una upungufu wa watumishi wenye stadi na ujuzi unaotakiwa

•  Mkoa bado una upungufu wa zahanati 448, Vituo vya afya 130, na hospitali 7. (Jedwali Na.10).

•  Mkoa una upungufu wa vitendea kazi (Jedwali Na. 6).

MIKAKATI

•  Sera ya Taifa ya afya ni kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Kwa hiyo matarajio ya Mkoa ni kutekeleza mpango wa maendeleo ya afya (MMAM) .

•  Katika kutekeleza sera hiyo mkoa utakamilisha mpango wa ujenzi wa zahanati katika kila kijiji na Kituo cha afya katika kila kata.

•  Katika mwaka 2007/2008 mkoa unatarajia kuajiri wataalamu ili kukidhi mahitaji ya zahanati na vituo vya afya vilivyopo.

•  Ujenzi rasmi wa zahanati na vituo vya afya vipya utaanza mwaka 2008/2009.

•  Katika mpango huu wa MMAM tutatumia dhana ya ushirikishwaji wa wananchi kama ilivyotumika katika mpango wa maendeleo wa Elimu ya msingi na Sekondari.

 

Magonjwa kumi ya juu yanayosababisha vifo (Ten top diseases causing mortality) .

1. Malaria

2. UKIMWI

3. Kifua Kikuu

4. Upungufu wa Damu

5. ”Pneumonia”

6. Magonjwa ya moyo na shinikizo la damu (Cardiorascular Diseases)

7. Magonjwa ya njia za hewa

8. “Pelvic Infections”

9. Kisukari

10. Homa ya Uti wa Mgongo.

 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 028-2752184