Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya pamoja na wadau wengine wa maendeleo umejiwekea mikakati mbalimbali ya utekelezaji.
Mikakati hiyo ni pamoja na:
Kuhamasisha umma na sekta binafsi katika Kilimo cha umwagiliaji.
Kuhakikisha kwamba mifumo ya umwagiliaji (Inayoanzishwa na itakayoanzishwa) inazingatia sheria na taratibu za nchi.
Kuhamasisha matumizi bora ya rasilimali maji katika mifumo ya Kilimo cha umwagiliaji.
Kuhakikisha kwamba Maendeleo ya Kilimo cha umwagiliaji yanazingatia masuala ya kiufundi, kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Kuhakikisha kwamba rasilimali maji ya umwagiliaji yanatumika kikamilifu kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia tija.
Kuhakikisha kwamba miundo ya maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji(Irrigation development models) inatumika kuzalisha mazao yenye tija kulingana na mahitaji ya soko.
Kuhuisha masuala mtambuka kama vile jinsia, ukimwi, mazingira, afya, ardhi na maji katika maendeleo ya Kilimo cha umwagiliaji.
Kuendelea kutekeleza Kilimo cha umwagiliaji kupitia programu ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) kwa kuongeza eneo lenye miundo mbinu ya umwagiliaji kutoka hekta 19,414 za Juni 2011 hadi hekta 50,000 ifikapo mwaka 2015. Sekta binafsi itashirikishwa katika uendelezaji na uwekezaji kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Kuzihimiza Halmashauri kukamilisha kutunga sheria ndogo za umwagiliaji.
Kujenga na kukarabati miundombinu ya umwagiliaji ya wakulima wadogo na wakati ili kuongeza uzalishaji na ufanisi wa matumizi ya maji.
Kujenga na kukarabati mabwawa ya kuvuna na kuhifadhi maji ya mvua na mito kwa ajili ya umwagiliaji kwa kila Halmashauri ya wilaya.
Kujenga uwezo wa Taasisi zinazohusika na umwagiliaji katika ngazi ya Halmashauri za wilaya na wakulima katika usimamizi na uendeshaji endelevu wa miradi ya umwagiliaji. |