BARABARA
Mkoa wa Kagera unao mtandao wa barabara zenye urefu wa Km. 4785.66 zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) na Halmashauri za Wilaya/Manispaa.
Wakala wa Barabara (TANROADS)
Barabara zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) ni Km. 1840.2 ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo :-
Na. |
Aina ya barabara |
Lami (Km) |
1 |
Barabara za lami |
397.8 |
2 |
Barabara za Changarawe |
1,442.4 |
|
JUMLA KUU |
1,840.2 |
Halmashauri za Wilaya/Manispaa
Barabara zinazohudumiwa na Halmashauri za Wilaya/Manispaa ni Km. 2,945.46 ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo :-
Na. |
Aina ya barabara |
Lami (Km) |
1 |
Barabara za lami |
9.92 |
2 |
Barabara za changarawe |
1,394.65 |
3 |
Barabara za udongo |
1,540.89 |
|
JUMLA KUU |
2,945.46 |
HALI YA BARABARA
Hali ya barabara kwa ujumla ni nzuri na karibu asilimia 90 ya mtandao wa barabara za mkoa huu zinapitika bila matatizo. Hali hii inatokana na Mkoa huu kuwa na miradi mingi ya barabara. Hata hivyo, baadhi ya barabara hasa zinazohudumiwa na Halmashauri ziko katika kiwango cha udongo na zinapitika kwa shida husasani kipindi cha mvua. Serikali imekuwa ikizifanyia matengenezo mbalimbali barabara hizo kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund) . Katika mwaka wa fedha wa 2007/08 Serikali imetenga jumla ya TShs. 6.96/= bilioni kwa matengenezo ya barabara za mkoa zinazohudumiwa na Wakala wa barabara (TANROADS) .
Fedha za matengenezo ya barabara za TANROADS
Na |
Aina ya kazi |
Malengo ya kazi |
Fedha zilizoidhinishwa 2007/08
(Tshs. milioni) |
1 |
Matengenezo ya Barabara kuu |
Km. 467.26 |
3,641.957 |
Madaraja 126 |
2 |
Matengenezo ya Barabara za mkoa |
Km. 1151.16 |
2,944.314 |
Madaraja 26 |
3 |
Miradi ya maendeleo katika barabara za mkoa kwa kiwango cha Lami |
Km. 37 |
375.000 |
JUMLA |
6,961.271 |
Na kiasi cha fedha Tshs.2.87/= bilioni kwa matengenezo ya barabara zinazohudumiwa na Halmashauri.
Fedha za matengenezo ya barabara za Halmashauri
Na |
Aina ya kazi |
Malengo ya kazi |
Fedha zilizoidhinishwa 2007/08
(Tsh milioni) |
1 |
Matengenezo ya kawaida |
Km. 1833 |
1145.2 |
2 |
Matengenezo ya muda maalumu |
Km. 100.94 |
1261.03 |
3 |
Matengenezo ya sehemu korofi |
Km. 201.1 |
226.4 |
4 |
Ujenzi wa Madaraja/makaravati |
Madaraja/makaravati |
238.1 |
JUMLA YA GHARAMA |
2,870.73 |
Karibu asilimia 25 ya bajeti ya barabara hizo imetumwa kwenye Halmashauri. Aidha, kwa kutumia wadau mbalimbali chini ya mpango wa STABEX jumla ya Km. 228.1 zimefanyiwa matengenezo kwa kiwango cha changarawe kwa gharama ya Tshs. 2.457/= bilioni. Kwa kutumia mfuko wa TASAF, mpango wa VTTP/LGTP na LGCDP , na wadau mbalimbali Mkoa umezifanyia matengenezo mbalimbali barabara za Halmashauri hususan maeneo ya vijijini.
HALI YA UTEKELEZAJI WA BARABARA KUU.
Mkoa unayo miradi ya ujenzi wa barabara kuu kwa kiwango cha lami ambayo imefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyamyorwa -Buzirayombo (Km. 120) kwa kiwango cha lami umefikia kiwango cha asilimia 99. Mradi wa ujenzi wa barabara ya Buzirayombo- Geita (Km 100) kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 80, na ujenzi wa barabara ya Kagoma-Rusahunga (Km. 154) kwa kiwango cha lami umekwishaanza na maendeleo ya jumla ya mradi huu ni asilimia 10. Hata hivyo, kasi ya utekelezaji bado ni ndogo.
MATATIZO YA SEKTA YA BARABARA
Upungufu/Ukosefu wa Wakandarasi wenye uwezo na mitambo
Kulima/kujenga kwenye maeneo ya hifadhi ya barabara (Road reserve) .
Uharibifu/wizi wa alama za barabara (road sign)
Hali ya hewa hususan mvua nyingi ambayo huchangia kuharibu barabara.
Upungufu wa fedha (bajeti) za matengenezo ya barabara.
MKAKATI WA KUKABILIANA NA MATATIZO
Kutumia Mfuko wa kuinua Wakandarasi (CAF) ili kupata mikopo ya kununulia vifaa/mitambo ya ujenzi wa barabara.
Kutumia sheria n dogo ndogo (by-law) kulinda hifadhi ya barabara.
Kuomba fedha za kutosha kutoka kwenye Mfuko wa Barabara.
|