JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
 
 
     
 
 
[ Nyumbani ] au
 
muda

KAGERA WAADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA KATIKA MIJI YA BUKOBA NA DAR ES SALAAM

 

 

Maadhimisho ya miaka hamsini (50) ya Uhuru wa Tanzania Bara mkoani Kagera yameadhimishwa rasmi kuanzia tarehe 28/11/2011 katika viwanja vya Kyakailabwa nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, ambapo mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo.

Uzinduzi wa maadhimisho ya Miaka hamsini (50) ya Uhuru wa Tanzania Bara mkoani Kagera yalihudhuriwa na wageni mbalimbali wa heshima ambao walitoka ndani na nje ya mkoa wa Kagera. Wageni waliohudhuria maadhimisho hayo ni wakuu wa Mkoa wa Kagera wastaafu ambao ni Mhe. Generali T. N. Kiweru na Mhe, Mohammed A. Babu, na mkuu wa mkoa wa Kigoma Mhe. Kanali Mstaafu Issa Machibya. Pia maadhimisho hayo yalihudhuriwa na ujumbe kutoka Rwanda na Burundi katika mikoa ya jirani na mkoa wa Kagera.

Katika maadhimisho hayo ya miaka hamsini ya uhuru mkoani Kagera yanayoendelea mpaka Desemba 9, 2011 yamepambwa na maonyesho mbalimbali ya taasisi, idara, wakala wa serikali, taasisi binafsi, mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya serikali na watu binafsi ambapo wanaonyesha shughuli mbalimbali katika mafanikio ya miaka hamsini mkoani Kagera.

Uzinduzi wa maadhimisho ya miaka Hamsini ya Uhuru mkoani Kagera yalipambwa na gwalide la Jeshi la Mgambo ambapo siku hiyo Jeshi hilo lilikuwa linahitimu mafunzo ya mgambo. Mkuu wa mkoa mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe alikagua gwalide hilo pia na kushuhudia jinsi jeshi hilo lilivyofunzwa mbinu mbalimbali za kijeshi za kupambana na adui, kuchoma singe na kutawanya maandamano yasiyokuwa halali.

Vilevile katika sherehe hizo mkuu wa mkoa wa Kagera alisoma taarifa ya Miaka 50 ya Uhuru ya mkoa wa Kagera. Taarifa hiyo inaonyesha ni wapi mkoa umetoka, ulipo na unakoelekea katika miaka hamsini ijayo. Aidha Mkuu wa mkoa alibainisha matarajio ya mkoa katika miaka hamsini ijayo kuwa ni;

Kudumisha amani na utulivu pia ujirani mwema na nchi jirani, kuimarisha uchumi ili kuongeza pato la mwananchi wa Kagera, Kuimarisha maisha bora ya wananchi kupitia mamlaka za serikali za mitaa, Kuimarisha kiwango cha elimu, mafunzo kwa walimu na miundombinu ya elimu, Kudumisha utawala bora kwa kuziba mianya ya rushwa na ukwepaji wa kulipa kodi. Pia mkoa utahakikisha unasimamia uadilifu katika utumishi wa umma.

Wakati huohuo , mkoa wa Kagera unashiriki maonesho ya kitaifa ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanzania Bara katika jiji la Dar es Salaam, maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Mh. Rais wa Zanzibar mhe. Dr. Ally Mohamed Shein. Katika uzinduzi huo, mhe.rais aliweza kutembelea banda la mkoa wa Kagera na kuona shughuli mbalimbali ambazo zinafanywa na wananchi wa mkoa wa Kagera. Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 12/12/2011.

Hapa chini ni picha mbalimbali zinazoonesha bidhaa katika viwanja vya maonesho Bukoba na dar es Saalm na wageni waliofika kutembelea mabanda ya mkoa wa kagera.

R

Rais wa Zanzibar mhe. Dr. Ally Mohamed Shein akikagua banda la mkoa wa Kagera jijini Dar es salaam.

Kahawa iliyosindikwa na kiwanda cha Tanica kilichopo mkoani Kagera.
Bidhaa zinazotokana na miamba kutoka wilaya ya Karagwe
Bidhaa za nafaka kutoka Karagwe ambazo zinawapatia kipato wananchi
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
         
 
[ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 0282752184