Tunashukuru juhudi za Mkuu wa mkoa kuanzisha mfuko wa kuendeleza elimu mkoani Kagera zilizoanza mwishoni mwa mwaka jana. Baadhi ya matunda ya mfuko huo katika mkoa wetu ni kama ifuatavyo:-
Kufadhili ujenzi wa vyumba vya madarasa. Shule ya sekondari za Ijuganyondo imejengewa madarasa 3 kupitia ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania. Pia shule ya sekondari ya Bugene iliyopo wilayani Karagwe imejengewa madarasa matatu kupitia kampuni ya Vodacom.
Kufadhili ujenzi wa maabara. Shule sita kutoka halmashauri za Muleba (Kagondo), Ngara (Shyunga), Biharamulo (Rubondo), Chato (Makurugusi), Bukoba Vijijini (Izimbya) na Missenyi (Bunazi) zimepata ufadhili wa kujengewa maabara na tayari walishapewa malipo ya awali ya shilingi 14,000,000/- kwa kila shule. Malipo mengine yapo mbioni kutumwa ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizi. Tunaomba uongozi wa wilaya kurekebisha upungufu wanayoagizwa na uongozi wa Kagera Day ili kukamilisha ujenzi.
Benki ya NBC tawi la Kagera imefadhili mifuko ya saruji 150 yenye thamanni ya shilingi 3,000,000/- kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za sekondari. Baadhi ya wilaya hazijafika kuchukua mgawo huu. Wilaya hizi ni Chato, Muleba na Karagwe. Wafanye jitihada za kuchukua mifuko hii.
Kampuni ya Multichoice imeweza kufadhili shule 8 kwa kuwawekea “dish” na TV kwa ajili ya kutoa channels za mambo ya kielimu.
Ufadhili wa Kompyuta. Mfuko wa Kagera Day umeweza kupata wafadhili ambao wameleta kompyuta 51 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari. Kompyuta hizo zimegawanywa kwa shule mbalimbali za mkoani Kagera. Kila halmashauri iliteua shule moja kwa ajili ya mgawo huo. Shule zilizonufaika na mgawo huo ni kama ifuatavyo:-
Biharamulo Shule ya Sekondari |
Biharamulo |
6 |
Nyamirembe Shule ya Sekondari |
Chato |
6 |
Maruku Shule ya Sekondari |
Bukoba Vijijini |
6 |
Shule ya Sekondari |
Missenyi |
6 |
Shule ya Sekondari |
Muleba |
7 |
Ngara Shule ya Sekondari |
Ngara |
7 |
Bugene Shule ya Sekondari |
Karagwe |
7 |
Rugambwa Shule ya Sekondari |
Manispaa |
6 |
Ufadhili wa Mabati. Mfuko umeweza kuto mabati 600 ambayo yamegawiwa kwa halmashauri zote kwa uwiano wa mabati 75 kwa kila moja. Tunawashukuru wafadhili hao na watu wenye mapenzi mema ambao wanazidi kutoa misaada hii ili kuuendeleza mkoa wa Kagera katika sekta ya Elimu. Pia tunasisitiza kuwa wanaonufaika na misaada hii waitumie kwa makusudi yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
|