JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BKB VIJIJIN
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA VIIVJINI
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

Huduma za Afya

 

Kuna Hospitali 1, Vituo vya Afya 5 na Zahanati 53 kama inavyoonekana katika jedwali la hapa chini:-

Jedwali Na. 5 – Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati :-

KITUO CHA HUDUMA

MMILIKI

SERIKALI

TAASISI

BINAFSI

JUMLA

Hospitali

0

1

-

2

Kituo cha Afya

4

2

-

6

Zahanati

21

4

1

26

Kliniki Mzunguko

92

-

-

92

•  Watumishi wa Afya Waliopo

Idadi ya watumishi wanaotoa huduma za kinga na tiba kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ni 239 kama ifuatavyo:-

•  Madaktari 1

•  Madaktari Wasaidizi (AMO) 4

•  Tabibu (Clinical Officers) 25

•  Waganga Wasaidizi (V) 13

•  Maafisa Wauguzi 4

•  Wauguzi Wakunga 37

•  Maafisa Afya 5

•  Mabwana Afya Wasaidizi 13

•  Wauguzi Afya ya Jamii 8

•  MCHA 22

•  Wahudumu wa Afya 70

JUMLA: 207

Kulingana na takwimu hizi, Daktari mmoja anahudumia wastani wa wananchi 241,178 ukilinganisha na lengo la Kitaifa la wastani wa watu 15,000 kwa Daktari moja.

Magonjwa Makuu 10

Na.

Ugonjwa

Idadi ya waliougua

Vifo

1

Malaria

74,697

178

2

Mangonjwa ya Njia ya hewa (ARI)

37,719

34

3

Minyoo

8,393

15

4

Kichomi (Pneumonia)

7,162

13

5

Kuhara

5,083

50

6

Ngozi

4,057

0

7.

Uchunguzi mwingine

3,686

33

8.

Macho

3,532

0

9

Kupungukiwa Damu (Anaemia)

1,748

20

10.

Magonjwa ya masikio

1,506

 

Kati ya magonjwa haya, Malaria ndiyo inaongoza, Watu 74,697 waliugua Malaria katika mwaka 2006, ARI ndiyo inayofuata ambapo watu 37,719 waliungua.

 

 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
Magonjwa hatari ya kuambukiza ni kama yafuatavyo
 

•  Kuumwa na mbwa wenye kichaa.

•  Uti wa mgongo.

•  Homa ya matumbo.

•  Kuhara damu.

•  Magonjwa ya watoto.

•  UKIMWI.

Elimu ya Afya inaendelea kutolewa kwa wananchi ili wajikinge na magonjwa haya. Kuna mafanikio makubwa katika magonjwa mengine isipokuwa Ugonjwa wa Ukimwi ambao bado ni tishio kwa wananchi wetu. Juhudi zaidi zinahitajika ili kufanya jamii iweze kubadili tabia yake ya maisha
 
 
 

Hali ya Ukimwi Wilayani

 

Hali ya Ugonjwa wa UKIMWI katika Halmashauri ya Wilaya Bukoba – Maambukizi:-

Kwa ujumla hali ya maambukizi ya HIV/AIDS katika Wilaya inaonyesha kuongezeka kutokana na mabadiliko yanayojitokeza ya kupanda na kushuka kwa magonjwa ya zinaa katika jamii.

Matokeo ya vipimo vya damu yanaashiria kupungua na kuongezeka kila mwaka. Kiwango cha maambukizi ya HIV/AIDs katika Wilaya kwa mwaka 2002 kilikuwa wastani wa asilimia14% na Kwa mwaka 2007 kiwango cha maambukizi kimeonekana kufikia wastani wa asilimia 10% kufuatia takwimu za VCT ((3.6), PMTCT(6.1%).

 

 

Mikakati ya Kupambana na UKIMWI

•  Kuendelea kutoa elimu shuleni, vyuoni na Jamii nzima

•  Kuhamasisha jamii kupima Afya zao na kubadili tabia.

•  Kuimarisha kampeni ya Ishi ambayo imeanzishwa wilayani.

•  Kutoa elimu kuhusu UKIMWI katika sehemu za kazi.

•  Kutoa elimu kwa wafanyakazi wa baa, mahoteli na nyumba za kulala wageni,

•  Kushirikisha na kushirikiana na madhehebu ya dini ili kutoa elimu kwa waumini wa madhehebu mbalimbali.

•  Kuanzisha na kuimarisha Kamati za UKIMWI za Wilaya, Kata na Vijiji/Vitongoji.

•  Kuelimisha jamii kufanya ngono salama kwa kuhimiza matumizi ya kondomu kwa usahihi, kwa kutumia vikundi vya sanaa na mikutano ya hadhara.

 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184