Zipo shule 28 ambazo kati ya hizo 24 ni za Serikali na 4 zinamilikiwa na watu binafsi na zisizo za Kiserikali. Kuna jumla ya wanafunzi 7,719 kati ya hao wasichana ni 3,525 (sawa na 46.0%) na wavulana ni 4,194 (sawa na 54.0%).
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Sekondari hizo mwaka 2007 ni kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 4 – Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Sekondari kwa Halmashauri ya Wilaya Bukoba .
HALMASHAURI YA WILAYA BUKOBA .
|
WAV
|
WAS
|
Jumla
|
Asilimia |
Waliofanya mtihani |
2,057 |
2,299 |
4,806 |
86.8 % |
|
|
|
|
|
Waliofaulu |
1,857 |
1,517 |
3,378 |
70.2% |
|
|
|
|
|
Waliochaguliwa |
1,857 |
1,517 |
3,378 |
100% |
Hatua kadha zinachukuliwa ili kukabiliana na upungufu wa wanafunzi wanaojiunga na Sekondari ni pamoja na:-
Kuihamasisha Sekta Binafsi/Taasisi kuwekeza katika Elimu ya Sekondari.
Kuanzisha ujenzi wa shule mpya za kutwa katika ngazi za Kata kwa kushirikisha jamii kuchangia nguvu, fedha na vifaa.
Kuendelea kushirikisha Wadau wengine wa Elimu ili kukarabati majengo na kujenga majengo mapya ya Sekondari za kutwa zilizoanzishwa.
Kuhakikisha kila Kata wanajenga shule moja ya Sekondari ya wananchi.
Kuendelea kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (MMES).
|