| UTANGULIZI |
|
| |
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ni moja kati ya Halmashauri za Wilaya nane zilizomo katika Mkoa wa Kagera. Halmashauri ya Wilaya hii ni miongoni mwa Halmashauri kongwe nchini kwani imekuwepo tangu kabla ya Uhuru wa Nchi yetu.
|
| |
|
| |
MAHALI ILIPO KIJIOGRAFIA |
| |
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina jumla ya eneo lipatalo hekta 284,100, kati ya hizo hekta 2,293 ni eneo linalofaa kwa kilimo hekta 660 ni eneo la malisho ya mifugo, hekta 300 zimefunikwa na maji. Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba upande wa mashariki inapakana na Ziwa Victoria na Halmashauri ya Manispaa Bukoba, kaskazini inapakana na Wilaya ya Missenyi, magharibi inapakana na Wilaya Karagwe na kusini inapakana na Wilaya ya Muleba. Wilaya ipo katika vipimo vifuatavyo; Nyuzi 3 o 0045-31 o 00' Mashariki mwa Greenwich na nyuzi 1 o 00-3 o 00' kusini mwa Ikweta. Ipo milimita 1200 juu ya usawa wa Bahari. Hali hii inafanya Halmashauri ya Wilaya Bukoba kuwa na misimu miwili ya mvua yaani Vuli ambayo huanza mwezi Septemba na kumalizika mwezi Desemba na masika ambayo huanza mwezi Machi na kumalizika mwezi Juni. Kipindi cha Julai hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba ni kiangazi na kipupwe uanza mwezi Januari hadi mwezi Februari.
|
| |
|
|
| Halmashauri inazo kanda 3 za mvua |
| |
| |
| |
Ukanda wa mvua nyingi:
Ukanda huu hupata wastani wa mvua kati ya mm. 1,400 – 2,000, ukanda huu hupatikana sehemu za Tarafa za Bugabo, Kyamtwara, pamoja na sehemu kidogo za tarafa ya Katerero. |
| |
Ukanda wa mvua za kati:
Ukanda huu hupatikana katika Tarafa za Kyamutwara, Bugabo na Katerero aidha, hupata mvua za wastani kati ya mm 1,000 – 1,400. |
| |
| |
Ukanda wa mvua kidogo:
Ukanda huu hupata wastani wa mvua kati ya mm 600 – 1,000 kwa mwaka. Ukanda huu hupatikana Tarafa za Rubale na sehemu ya Tarafa Katerero. |
| |
| |
|
| |
|
| |
| |
| |
|
|
|
| |
ENEO
Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina ukubwa wa hekta 284,100 kati ya hizo hekta 300 zimefunikwa na maji hasa ya ziwa Victoria na Ikimba eneo lilobaki hekta 2,838 Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 2,293.
|
IDADI YA WATU |
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya 2002, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina watu 241,178 ikiwa na wanaume 119,288 na wanawake 121,890. Aidha ongezeko la watu ni asilimia 1.1.
|
| |
| |
| |
| |
| |
| |
|
| |
| |
| |
|