JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BKB VIJ
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA VIJIJINI
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 
KILIMO
 

Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba inalo eneo linalofaa kwa kilimo lenye ukubwa wahekta 2,293. Eneo hili hutumiwa na wakulima kwa makazi, kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Kwa utamaduni, wilaya hii inalima migomba (ndizi), mahindi na maharage kama mazao ya chakula na kahawa na chai kama mazao ya biashara. Kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuchoka kwa ardhi, kushuka kwa bei ya mazao ya kahawa na chai katika soko, mazao kama vanilla, alizeti na Kahawa ya Vikonyo yameanza kushika kasi kuwa mazao ya nyongeza/mbadala kwa mazao ya biashara.

Katika kulinda na kuimarisha mashamba hayo, kampeni maalum ya ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa imeendeshwa Vijijini. Lengo la kampeni hii ni kuwawezesha wakulima kupata mbolea ya samadi kwa ajili ya kilimo chao na kuepuka mbolea ya viwandani ambayo kwa kiasi kikubwa inayo madhara ya uharibifu wa mazingira.

 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184