Ufugaji ni moja ya Sekta muhimu katika uchumi wa Wilaya yetu. Sekta hii inasaidia na kutegemewa sana katika:-
Kilimo (urutubishaji).
Chakula (Lishe).
Biashara (Mazao yake kama nyama, ngozi, mifugo yenyewe).
Aina mbili za ufugaji zinatumika Wilayani hapa ambazo ni ufugaji huria na ufugaji wa ndani. Wananchi wetu hasa wa Vijijini kwa asili ni wafugaji huria. Ufugaji huria umetengewa hekta 660 kwa ajili ya malisho. Pamoja na uendelezaji wa ufugaji huu, juhudi za kuwahamasisha wakulima na wafugaji kupanua ufugaji wa ndani zinafanywa. Mashirika mbalimbali Mfano; World Vision imeendesha mpango wa kutoa mafunzo ya ufugaji ng'ombe wa maziwa na kuwakopesha wakulima/wafugaji ng'ombe wa maziwa.
Wakulima na Wafugaji wetu wanapata huduma ya kinga na tiba kwa kushirikiana na Wataalam wa Mifugo. Magonjwa makuu ya mifugo ni minyoo, ndigana kali, ndigana baridi na kichaa cha mbwa.
Zifuatazo ni takwimu za mifugo Wilayani:-
NA |
AINA YA MFUGO |
IDADI |
1. |
Ng'ombe wa Asili
Ng'ombe wa Maziwa |
30,272
2,769 |
2. |
Mbuzi wa Asili
Mbuzi wa Maziwa |
66,226
735 |
3. |
Kondoo |
5,686 |
4. |
Nguruwe |
1,277 |
5. |
Kuku wa Asili |
74,560 |
6. |
Bata |
6,025 |
7. |
Mbwa |
4,795 |
|
|
|
|