JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BKB VIJ
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA VIJIJINI
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

•  HIFADHI YA MAZINGIRA

 

Katika kipindi cha mwaka 2006, lengo lilikuwa ni kupanda miti 1,056,000. Utekelezaji halisi ni kuwa jumla ya miti 932,200 ilipandwa sawa na 88%. Mwaka 2008 tunatarajia kupanda miti 1,500,000 katika Vijiji vyote 92.

 

 
 
 

MAENDELEO YA UCHUMI NA VITA DHIDI YA UMASKINI

Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ina Wadau (Stakeholders) mbalimbali wanaojishughulisha na shughuli za kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi ili kufanikisha juhudi za kuondoa umaskini. Wadau hao ni pamoja na Serikali Kuu, Vyama vya kuweka na kukopa, Wafanya biashara, Wavuvi na Asasi za kiraia na zisizo za Kiserikali na Programme za maendeleo kama vile TASAF, Columbia University, TADEPA na World Vision Tanzania
 
 

KUONDOA KERO ZA WANANCHI NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Kero na vitendo vya rushwa ni mambo yanayosababisha chombo au Serikali yeyote ichukiwe sababu ya kutokuwepo haki. Kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000. Halmashauri imeendesha shughuli zake zikilenga kuondoa kero za wananchi na kupunguza au kuondoa kabisa mianya ya rushwa kwa njia zifuatazo:-

 

•  Taarifa za mapato na matumizi huwa wazi kwa umma.

•  Taratibu za ajira wakati wote zinazingatia miongozo na sheria.

•  Mipango ya maendeleo imeweka kipaumbele matakwa na inajibu hoja za wananchi mfano wake ni:-

•  Ujenzi wa madarasa.

•  Miradi ya kilimo na ufugaji.

•  Uimarishaji Vyama vya Ushirika ili viweze kutenda kazi kwa uwazi.

•  Mabaraza ya Kata yameundwa ili kusuluhisha migogoro miongoni mwa wananchi.

•  Halmashauri imeweka masanduku ya maoni ili kuwawezesha wananchi kutoa maoni yao na malalamiko yao na yanafanyiwa kazi kwa huandikwa kwenye rejista ya maoni ambayo hukaguliwa chini ya Mpango wa uboreshaji wa Serikali za Mitaa (yaani ni kigezo cha utawala bora)

•  Uendeshaji wa shughuli zote kwa njia za vikao:-

•  Baraza la Madiwani hutangazwa na huwa wazi kwa watu wote.

•  Mikutano Mikuu ya Mitaa/Vijiji hujadili kwa uwazi mambo yote yahusuyo maisha yao.

•  Vikao vya Mitaa/Vitongoji hutoa pia nafasi kwa wanavijiji kujadili kwa uwazi. Mambo yote yahusuyo maendeleo na maisha yao.

Vikao vingine kama vile Kamati za Kudumu za Madiwani, Wakuu wa idara, Serikali za Vijiji na Mikutano ya Mradi mbalimbali kama vile ya “World Vision (T)”, Columbia Universty, TADEPA, n.k. hutoa nafasi za wahusika kwa niaba ya wale wanaowawakilisha

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
UWEKEZAJI KATIKA SEKTA BINAFSI
 

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali, Wilaya yetu imefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza. Tumefanya jitihada kubwa kuboresha mazingira ya Wilaya yetu ili yavutie wawekezaji hao kuweka mitaji yao kwetu. Uboreshaji wa huduma za jamii zitolewazo Wilayani hapa kama kuwa na barabara nzuri zinazopitika muda wote, hali ya amani na utulivu, kuinua viwango vya uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara ni katika jumla ya mbinu za kuvutia wawekezaji katika Sekta Binafsi. Kutokana na hivyo, Wilaya imefanikiwa kupata wawekezaji katika maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:-

•  Kiwanda kimoja kimejengwa Kemondo na tayari kimeanza uzalishaji (Kagera Fish Company). Kiwanda hiki tayari kimeajiri wafanyakazi 125 na hadi Julai, 2007 kina jumla ya wafanyakazi 300.

•  Katika kuitikia Sera ya soko huria ili kuwapa mwanya wakulima kupata bei nzuri, wameruhusiwa wanunuzi mbalimbali wa kahawa kufanya hivyo. Hao ni Chama Kikuu cha Ushirika KCU na Kampuni Binafsi zaidi ya nne. Lengo ni upatikanaji wa bei nzuri kwa wakulima.

•  Wawekezaji wa ndani wamefunguliwa milango na hivyo kujisikia huru kuwekeza katika Sekta hiyo. Hoteli ya WALKGARD & TOURS imefunguliwa na inatoa changamoto kubwa ya huduma ya Kisasa na Utalii wa vivutio vingi vya Wilaya na Mkoa huu vilivyokuwa havitangazwi kwa uhai wa kuwepo kwavyo.

•  Kiroyela Tours ni Kampuni ya Wawekezaji wa Ndani ambayo nayo inajihusisha na masuala ya Utalii. Wamefanya kazi kubwa ya kuvibaini na kuvitangaza vivutio vya utalii wa Wilaya na Mkoa ndani na nje ya nchi hii. Aidha wameamsha ari na moyo wa wananchi wetu kupenda na kujali vivutio hivyo ili nao washiriki kuviona.

Kwa jumla Sekta Binafsi inatoa mchango mkubwa katika kuongeza ajira ya watu wetu, kuinua pato la wananchi na Taifa kwa jumla lakini pia kuwa chachu ya maendeleo ya jamii. Aidha maeneo 16 yametengwa wilayani kwa ajili ya wawekezaji (Land bank) zenye hekta 8,490 ha kwa ajili ya Kilimo, ufugaji na viwanda.

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184