Maendeleo ya Miundo Mbinu ya Barabara ni muhimu katika kukuza uchumi na huduma za kijamii katika Halmashauri yetu na Taifa kwa ujumla. Mtandao wa barabara katika Halmashauri yetu ni kama ifuatavyo:
Barabara Kuu km. 36 (tabaka la lami), barabara za Mkoa km 234, na barabara za Wilaya km. 578 (changarawe/udongo).
Matengenezo ya barabara hufanyika mara kwa mara ili ziweze kuendelea kupitika kwa mwaka mzima, hivyo kurahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo, hatimaye kukua kwa uchumi katika jamii.
|