Halmashauri ya Wilaya ina Tarafa 4, Kata 24, vijiji 92 na vitongoji 508. Kuna Jimbo moja la Uwakilishi Bungeni (Jimbo la Bukoba Vijijini); Wilaya ina Madiwani 35 na Mbunge 1 kati ya madiwani hao 24 ni wa kuchaguliwa kutoka kwenye Kata na 11 ni kutokana na Viti Maalum
|
Ishara za Halmashauri
Bendera
Halmashauri inayo bendera ambayo ina vipimo kulingana na ngazi ya uongozi ambako inapeperushwa kwenye ngazi ya Halmashauri, Ngazi ya Kata, ngazi ya Kijiji, Ngazi ya Kitongoji na ndogo ya kuweka Mezani. Bendera hiyo ina rangi ya Dhahabu na imewekewa nembo ya Halmashauri (maelezo ya nembo yameelezwa hapo chini)
Nembo
Hapa chini kuna nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, ambayo ni ngao ilichorwa kwa rangi nyeusi na mabaka ya pembe tatu za rangi ya udongo, ndani ya ngao hiyo kuna picha ya Mtu aliyevaa kanzu ya kijani na juu yake amevaa ngozi ya chui. Mtu huo anapiga ngoma akiashiria kuita wananchi kuja kukusanyika ili kupata maagizo ya watawala. Mbele ya mtu huyo kuna migomba miwili mmoja mkubwa una ndizi na mwingine mdogo, nyuma yake kuna mbuni/kahawa iliyopamba mazao yaliyoiva tayari kwa kuvunwa. Aidha chini ya nembo hiyo kuna maandishi yanayosomeka Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba kama inavyoonekana hapa.

|