JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA WA KAGERA
     
 
     
MULEBA
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

MAENDELEO YA JAMII

 

 

Idara ya Maendeleo ya Jamii ni moja wapo ya Idara 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Muleba na hutekeleza shughuli zake kupitia kwenye vitengo 3 ambavyo ni:-

•  Kitengo cha utafiti na Takwimu

•  Kitengo cha Maendeleo ya Wanawake na Watoto

•  Kitengo cha Ujenzi na Mafunzo ya Ufundi vijijini.

Majukumu ya idara ni kuwezesha Jamii:

Œ Kutambua na kuchambua matatizo yake na hatimaye kuyapangia mikakati ya kuyatatua kwa njia ya kushirikishana wajibu wa nani afanye nini na nani, wapi na lini na kwa manufaa ya nani,  Kupanga mipango inayoweza kuisimamia, kuiendesha, kuiratibu, kuitathimini na kuitunza kwa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira yao na pale inapolazimu kupata msaada wa hali na mali kutoka nje ya mazingira yao.

Watumishi wa Idara hii wanao wajibu wa kuandaa Jamii kwa kutumia mbinu raghbishi, shirikishi Jamii, hamasa na mafunzo ili jamii yenyewe iweze kujiletea maendeleo endelevu kwa kuishawishi, kuielekeza, kuiwezesha na kuianzishia mkereketo wa kutaka kujifunza mambo wasiyoyafahamu ili waweze kuyatekeleza kwa vitendo.

 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184