JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
MULEBA
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA MULEBA
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

Uchumi

 

Pato la mwananchi wa Muleba linakadiriwa kuwa kati ya Tshs. 100,000 – 150,000 kwa mwaka. Hali hii ni chini ya mstari wa umaskini hivyo kuashiria kuwa wilaya hii ni kati ya wilaya maskini sana katika nchi ya Tanzania .

Zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wa Muleba wanategemea zaidi shughuli za kilimo kwa maisha yao ya kila siku. Zao kuu la biashara ni kahawa na mazao ya chakula ni ndizi na maharage. Kuporomoka kwa bei ya kahawa kumewakatisha tamaa wakulima hivyo kupelekea kutothanimi zao hili.

Zao la ndizi pamoja na kuwa ni zao la chakula pia huwapatia wakulima kipato kwani huuzwa katika masoko ya nje ya wilaya na mikoa jirani kama Mwanza na Shinyanga. Pia zao hili huwapatia wakulima kipato wanapotengeneza pombe ya kienyeji (Rubisi). Maharage mara nyingi hutumiwa na familia wakati zao la chai halipewi kipaumbele baada ya bei yake kuwa ya chini sana hivyo kupelekea wakulima kutelekeza mashamba.

•  Umiliki na matumizi ya ardhi

Ardhi mara nyingi inamikiwa katika mfumo wa kiukoo ambapo mara kwa mara inamilikiwa na kurithiwa na wanaume. Maeneo ya mbuga yanamilikiwa na jamii kwa shughuli za ufugaji na kilimo cha mazao ya muda mfupi.

•  Utaratibu wa kilimo:

Kilimo cha kujikimu hufanywa katika ngazi ya familia kwa kutumia wanakaya. Zipo aina tatu za matumizi ya ardhi zinazotambuliwa ambazo ni Kibanja, Kikamba na Rweya

•  Kibanja - Ni shamba la migomba ambalo pia huchanganya na mazao mengine kama miti ya matunda, kahawa, mihogo, mahindi, magimbi, viazi vikuu, maharage n.k. na miti ya mbao kama mihumula. Mara nyingi hapa ndipo makazi ya kaya.

Ardhi ya eneo hili huwa na rutuba sana kwani takataka zote pamoja na samadi ya mifugo mbalimbali hufugwa kwenye eneo hili. Kibanja kwa kawaida kimegawanyika katika matabaka manne ambapo mazao mbalimbali, tabaka la chini – maharage, magimbi na mboga, tabaka la pili – mahindi na mihogo ambayo huwa na urefu takriban mita 1.5 kutoka ardhini, tabaka la tatu ni zao la kahawa na tabaka la nne ni migomba, miti ya matunda na miti isiyodhuru mazao.

(b ) Kikamba ni shamba lililokanda kabisa ambalo hutumika kwa kulima mazao ya msimu kama viazi, mihogo, maharage, mahindi na mara nyingi huwa ni pembezoni mwa kibanja na kina rutuba ya wastani.

(c) Rweya : Hili ni eneo lenye rutuba ya chini na ni mbuga ya nyasi ambayo kwa kawaida hupandwa miti ya aina mbali mbali na hutumika kwa malisho ya mifugo. Mazao kama karanga, mtama, njugumawe hulimwa maeneo haya. Nyasi za kutandaza mashambani kupatikana katika maeneo haya.

 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 028-2752184