Wakazi wengi waishio mjini wanajishughulisha na biashara za aina mbalimbali. Aidha wakazi wengine ni waajiriwa katika taasisi za serikali na zisizo za kiserikali hususani Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kwa wale waishio Muleba mjini. Bidhaa kuu zinazouzwa ni zile za viwandani na mazao ya kilimo.
Uwekezaji katika shughuli za viwanda bado ni wa kiwango cha chini kwani viwanda vilivyopo ni vidogo vidogo vya kusindika matunda, kusaga nafaka na kusindika maziwa. Viwanda vingine ni vya ushonaji, uhunzi, useremala na ushonaji viatu. Aidha wilaya inayo fursa kubwa kwa ajili ya wawekezaji katika viwanda vya kusindika samaki na kahawa.
|