Walaya ya Muleba inazo barabara zenye urefu wa kilomita 1103 nyingi zikiwa za udongo na changarawe kama jedwali namba 4 linavoonyesha hapa chini.
Aina za barabara.
Na |
Aina ya barabara |
Urefu km. |
Asilimia |
1. |
Barabara kuu |
103 km |
9 |
2. |
Barabara za mkoa |
175 km |
15 |
3. |
Barabara za Wilaya |
210 km |
19 |
4. |
Barabara za vijiji |
615 km |
57 |
|
Jumla |
1103 km |
100 |
Barabara hizi kwa ujumla si mbaya sana , lakini kutokana na mmomonyoko wa udongo unaotokana na wingi wa mvua zinazonyesha kati ya mwezi Septemba hadi Desemba na Machi hadi Mei zinahitaji matengenezo ya mara kwa mara. Kikwazo kikubwa ni uhaba wa fedha za kuboresha barabara hizi.
Mpango wa Taifa wa kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami tayari umeonyesha matunda ambapo barabara ya Mtukula – Bukoba – Kagoma (Muleba) tayari imejengwa kwa kiwango cha lami.
Pia barabara kutoka Kyamyorwa hadi Chato imeshatengenezwa kwa kiwango cha lami. Aidha ujenzi wa barabara kuanzia Kagoma kwenda Rusahunga kupitia Biharamulo umekwishaanza japokuwa kwa sasa umesimama.Matarajio yetu ni kwamba mradi huo utaendelea hivi karibuni.
Usafirishaji wa abiria na mizigo
Usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo hutegemea sana magari kwa nchi kavu na mitumbwi kwa upande wa majini. Vyombo vyote hivi humilikiwa na watu binafsi. Hatuna usafiri wa anga kwa kuwa hatuna uwanja wa ndege, isipokuwa. kuna uwanja mdogo wa ndege kwa ajili ya ‘'Flying Doctors'' kwa hospitali teule ya wilaya (Rubya).
|