JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
MISENYI
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 
 
 

Huduma za Afya

Kuna Hospitali 2, kituo cha Afya 1 na Zahanati 28 kama inavyoonekana katika jedwali la hapa chini:-

Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati :-

KITUO CHA HUDUMA

MMILIKI

 

SERIKALI

TAASISI

JUMLA

Hospitali

0

2

2

Kituo cha Afya

1

0

1

Zahanati

19

9

28

Kliniki Mzunguko

62

16

78

Chanzo: Idara ya Afya, 2009

 

 

 
 
 
 
Watumishi wa Afya Waliopo
 

• 

Idadi ya watumishi wanaotoa huduma za kinga na tiba kwa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ni 330 kama ifuatavyo:-

  • Madaktari

1

  • Madaktari Wasaidizi (AMO)

2

  • Tabibu (Clinical Officers)

9

  • Wauguzi

19

  • RCH Aides

7

  • Wakunga wa Jadi

138

  • Wahudumu wa Afya Vijijini

148

  • Afisa afya

2

  • Bw/Bibi Afya

4

JUMLA

330

 

 
 

Magonjwa makuu 10

Magonjwa makuu 10 katika Halmashauri ya wilaya ya Missenyi ni kama ifuatavyo:-

Magonjwa makuu kumi kwa wagonjwa wa nje (Januari – Novemba 2008).

Na.

Ugonjwa

Idadi ya waliougua

Vifo

1

Malaria

117907

70

2

Mangonjwa ya Njia ya hewa (ARI)

28431

2

3

Minyoo

6296

0

4

Kuhara

17726

8

5

Macho

1865

0

6

Ngozi

3892

8

7

Kichomi (Pneumonia)

15206

8

8

Kupungukiwa Damu (Anaemia)

3577

12

9

Upasuaji mdogo ( Minor Surgical Condition )

6205

0

10

Magonjwa ya Zinaa ( UTI)

2471

0

Chanzo:, Idara ya Afya, 2009

 

Kati ya magonjwa haya, Malaria ndiyo inaongoza, Watu 117,907 waliugua Malaria katika mwaka 2008, ARI ndiyo inayofuata ambapo watu 28,431 waliungua.

 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
Magonjwa hatari ya kuambukiza ni kama yafuatavyo:-
 

•  Kuumwa na mbwa wenye kichaa.

•  Uti wa mgongo.

•  Homa ya matumbo.

•  Kuhara damu.

•  Magonjwa ya watoto.

•  UKIMWI.

Elimu ya Afya inaendelea kutolewa kwa wananchi ili wajikinge na magonjwa haya. Kuna mafanikio makubwa katika magonjwa mengine isipokuwa Ugonjwa wa Ukimwi ambao bado ni tishio kwa wananchi wetu. Juhudi zaidi zinahitajika ili kufanya jamii iweze kubadili tabia.

Hali ya Ukimwi Wilayani

Hali ya Ugonjwa wa UKIMWI katika Wilaya ya Missenyi – Maambukizi:-

Kwa ujumla hali ya maambukizi ya HIV/AIDS katika Wilaya inaonyesha kuongezeka. Sawia na kuongezeka kwa ugonjwa wa UKIMWI kuna ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa jambo linaloonesha kwamba jamii bado haijabadili tabia kwa kufanya ngono salama.

Matokeo ya vipimo vya damu yanaonesha kiwango cha maambukizi kupungua na kuongezeka kila mwaka. Kiwango cha maambukizi ya HIV/AIDs katika Wilaya kwa mwaka 2007 kilikuwa wastani wa 3.3% na Kwa mwaka 2008 kiwango cha maambukizi kimefikia 5.9% kufuatia takwimu za VCT 7%, PMTCT(4.8%) na Wanaojitolea damu.( 0%)

Mikakati ya Kupambana na UKIMWI

•  Kuendelea kutoa elimu shuleni, vyuoni na Jamii nzima

•  Kuhamasisha jamii kupima Afya zao na kubadili tabia.

•  Kuimarisha kampeni ya Ishi ambayo imeanzishwa wilayani.

•  Kutoa elimu kuhusu UKIMWI katika sehemu za kazi.

•  Kutoa elimu kwa wafanyakazi wa baa, mahoteli na nyumba za kulala wageni,

•  Kushirikisha na kushirikiana na madhehebu ya dini ili kutoa elimu kwa waumini wa madhehebu mbalimbali.

•  Kuanzisha na kuimarisha Kamati za UKIMWI za Wilaya, Kata na Vijiji/Vitongoji.

•  Kuelimisha jamii kufanya ngono salama kwa kuhimiza matumizi ya kondomu kwa usahihi, kwa kutumia vikundi vya sanaa na mikutano ya hadhara.

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184