Elimu ya Sekondari
Zipo shule 21 ambazo kati ya hizo 18 ni za Serikali na 3 zinamilikiwa na watu binafsi/Mashirika ya dini. Kuna jumla ya wanafunzi 7,465 kati ya hao wasichana ni 3,567 (sawa na 48%) na wavulana ni 3,897 (sawa na 52%). Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Sekondari mwaka 2009 ni kama ifuatavyo:-
WALIOFAULU |
WAV |
WAS |
Jumla |
Asilimia |
1487 |
1481 |
2968 |
100 |
WALIOCHAGULIWA |
WAV |
WAS |
Jumla |
|
1487 |
1481 |
2968 |
100 |
Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Sekondari kwa Halmashauri ya Wilaya Missenyi
Chanzo: Idara ya Elimu, 2009
Hatua kadha zinachukuliwa ili kukabiliana na upungufu wa wanafunzi wanaojiunga na Sekondari nazo ni:-
Kuihamasisha Sekta Binafsi/Taasisi kuwekeza katika Elimu ya Sekondari.
Kuanzisha ujenzi wa shule mpya za kutwa katika ngazi za Kata kwa kushirikisha jamii kuchangia nguvu, fedha na vifaa.
Kuendelea kushirikisha Wadau wengine wa Elimu ili kukarabati majengo na kujenga majengo mapya ya Sekondari za kutwa zilizoanzishwa.
Kuhakikisha kila Kata wanajenga shule moja ya Sekondari ya wananchi.
Kuendelea kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa mpango wa uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (MMES).
Kuaanda mazingira ya kuendesha na kusimamia Elimu ya sekondari kuanzia julai mwaka 2009 kama ilivyoamuliwa na Serikali.
Vyuo vya Ufundi
Kuna chuo kimoja cha ufundi. Maandalizi ya kujenga chuo kingine cha ufundi yameanza ili kukabiliana na changamoto za vijana wengi wanaomaliza shule na kukosa kuendelea na mafunzo ya sekondari .
Elimu ya Watu Wazima
Vipo Vituo 94 vya kisomo vyenye jumla ya wanafunzi 12,519 Kati ya hao 5312 ni wanaume na 6207 ni wanawake. Elimu ya Watu Wazima inakabiliwa na tatizo la mahudhurio duni, viwango vidogo vya malipo ya Walimu wa Kisomo, upungufu wa vifaa na vitendea kazi. Vile vile Vituo 42 vya MEMKWA vimeanzishwa vikiwa na wanafunzi 1005 sawa na wavulana 540 na wasichana 465 |