Ufugaji ni moja ya Sekta muhimu katika uchumi wa Wilaya yetu. Sekta hii inasaidia na kutegemewa sana katika:-
Kilimo (urutubishaji).
Chakula (Lishe).
Biashara (Mazao yake kama nyama, ngozi, mifugo yenyewe).
Jedwali Na: 8 takwimu za mifugo Wilayani
NA |
AINA YA MFUGO |
IDADI |
1. |
Ng'ombe |
58,329 |
2. |
Mbuzi |
54,797 |
3. |
Kondoo |
4,750 |
4. |
Nguruwe |
1,366 |
|
|
|
Chanzo:, Idara ya Kilimo na Mifugo 2009
Katika kuendeleza mifugo juhudi zimeelekezwa katika uzuiaji wa magonjwa ya mifugo, kuongeza ubora wa mifugo kwa njia ya uhamilishaji na kuanzisha huria za ufugaji katika maeneo yanayofaa kwa ufugaji kwa wawekezaji wa ndani.
Wakulima na Wafugaji wetu wanapata huduma ya kinga na tiba kwa kushirikiana na Wataalam wa Mifugo. Magonjwa makuu ya mifugo ni minyoo, ndigana kali, ndigana baridi na kichaa cha mbwa.
|