JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
MISENYI
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA MISSENYI
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 
MAJI
 

Hali ya upatikanaji wa maji safi na salama vijijini imeongezeka toka 41% mwaka 2007/08 hadi 48% mwaka 2008/09 na kuwezesha asilimia ya watu wanaopata maji safi na salama kufikia 94,340 toka 92,740 mwaka 2007 sawa na ongezeko la 7.12%. Hii imewezeshwa na utekelezaji wa mradi wa maji na usafi wa mazingira (RWSSP – Quick wins) ambapo chini ya mpango huu vyanzo vya maji 22 vimefanyiwa ukarabati hivyo kuongeza upatikanaji wa maji toka vyanzo 221 mwaka 2007/08 na kuwa na vyanzo 243 aidha miundombinu ya maji imeboreshwa kwa 52% kwa jumla ya TShs. 195,583,000/=

Halmashauri ya wilaya Missenyi inashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo hususani WV(T) Kupitia ADP ya Missenyi, Kagera sugar Co. Ltd, Partage, UN habitat na Programme ya maji na usafi wa Mazingira Vijijini ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama wilayani. Kwa mwaka 2008/09 Jumla ya miradi 38 ya maji imejengwa Vijijini miradi hiyo ni:-

•  Visima virefu (Handpump) - 2

•  Visima vifupi (Handpump) - 30

•  Gravity schemes - 1

•  Mabwawa - 2

•  Matanki ya maji ya Mvua (46,000M 3 ) - 3

 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
Jengo hili ni Ofisi Mpya ya Maji Wilayani Missenyi.
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184