Katika mwaka 2006/07 wilaya ilipata walimu wapya 65, walimu waliopatikana pia ni wale waliokuwa wameacha kazi nao ni 9. Jitihada zinafanywa kuziba upungufu uliopo wa walimu. Kutokana na Walimu watakaopata ajira ya moja kwa moja kutoka vyuoni.
MMEM
Katika kipindi cha mwaka 2006/07 mkazo katika mpango wa maendeleo ya Elimu ya Msingi umewekwa katika, uanzishwaji wa madarasa ya Elimu ya Awali, uandikishaji wanafunzi darasa 1, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa nyumba za Walimu, mafunzo kwa Kamati za Shule na ununuzi wa vitabu vya kiada. Aidha katika kipindi hicho jumla ya Tshs 682,474,041.= zililetwa kutoka hazina kwa ajili ya mpango wa MMEM kwa Mchanganuo ufuatao; Ujenzi wa madarasa Tsh.62,000,000.=. ujenzi wa Nyumba za Walimu Tshs 126.000.000.= Ununuzi wa Vitabu Tsh 197,777,308.80 Ununuzi wa vivunge vya Hisabati TShs.32,079,600.= na Utekelezaji halisi umekuwa kama ifuatavyo:-
Ujenzi wa madarasa 62,000,000.= kwa madarasa 20.
Ujenzi wa nyumba za Walimu 126,000,000.= kwa nyumba 35.
Ukarabati/mitihani/utawala 351,085,319.20.
Ununuzi wa vitabu 197,777,308.80.=
Kwa kuunga mkono juhudi za Serikali, wananchi wamechangia jumla ya TShs230,132,500.= katika ukusanyaji wa mawe, mchanga, kokoto, utengenezaji wa matofali, madawati na nguvu kazi.
Elimu ya Watu Wazima
Vipo vituo vya Ufundi Stadi 3 Isingiro (1), Nyaishozi (1) na Kibondo (1) vyenye jumla ya wanafunzi 70, wavulana 46 na wasichana 24. Pia zipo maktaba 107 kati ya mahitaji ya 204 na upungufu 97.
ELIMU YA UFUNDI
Wilaya inavyo vyuo viwili vilivyo rasmi vyenye matawi matatu (kikiwemo chuo kimoja cha Halmashauri ya Wilaya na chuo kimoja cha binafsi) vyuo hivi hutoa mafunzo ya Uashi, Useremala, Ufundi wa magari, Ufundi umeme, Udereva ushonaji na kuchomelea vyuma katika ngazi mbalimbali. Vyuo hivi huandikisha wastani wa wanafunzi 100 kila mwaka. Wanafunzi wa vyuo hivi wanafanya mitihani ya Taifa inayosimamiwa na VETA katika madaraja mbalimbali. |