DIRA (VISION) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KARAGWE
|
| |
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imedhamiria kuwa, katika kipindi cha miaka tisa ijayo, wananchi wa Wilaya hii kwa jinsia zote walioko Wilaya hii wawe jamii yenye maisha bora, inayowajibika kwa maendeleo yake, uchumi imara na endelevu na uongozi unaozingatia mipango shirikishi na utawala wa kisheria ifikapo 2025.
|
| |
|
| |
MWELEKEO (MISION): |
| |
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe imedhamiria kuandaa mazingira bora ya ukuaji uchumi kwa kutumia mbinu za kisasa, ushirikishwaji wananchi na matumizi endelevu ya raslimali zilizopo ili kuwapa maisha bora Watanzania kwa kuongeza kipato cha kila mkazi, kukuza uchumi na kupunguza Umaskini ifikapo 2025.
|
LENGO KUU: Lengo kuu la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kama ilivyoainishwa kwenye Dira na Mwelekeo, ni kuwa na jamii yenye kiwango cha juu cha maisha ya wakazi wake kwa miaka kumi ijayo ili kuondoa umaskini na kuishi maisha bora yenye kufuata utawala bora/sheria ifikapo 2015. |
|
|
|
MIPAKA NA ENEO
Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ni moja kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Kagera. Wilaya inapakana na nchi ya Uganda kwa upande wa Kaskazini, Rwanda kwa upande wa Magharibi, Kusini inapakana na Wilaya za Biharamulo na Ngara, Mashariki inapakana na Wilaya ya Muleba, Bukoba Vijijini na Misenyi. Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 7,716. mwinuko wa Wilaya ni kati ya mita 1500 na 1800 juu ya usawa wa bahari.
Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa nyuzi 26.C. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800 – 1100 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei.
Wilaya imegawanyika katika Tarafa nne, Kata 28, vijiji 109 na Vitongoji 1,162 na mitaa kama inavyoonyeshwa hapa chini:-
TARAFA |
KATA |
VIJIJI |
VITONGOJI |
Kituntu/Mabira
Kaisho/Murongo
Bugene/Nyaishozi
Nyabiyonza |
8
6
9
5 |
47
26
21
15 |
500
238
271
153 |
JUMLA |
28 |
109 |
1162 |
Wilaya inayo Majimbo 2 ya uchaguzi ambayo ni Jimbo la Kyerwa na jimbo la Karagwe.
|
| |
|
| |
|
| |
IDADI YA WATU |
| |
|
| |
Kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2002 Wilaya ina watu 425,476 wakiwemo wanaume 208,620 na wanawake 216,856 Ongezeko la watu la Wilaya 2.9 kwa mujibu wa sensa ya watu ya 2002 Asilimia ya watoto yatima 1.35 . Mwaka 2007 idadi inakadiriwa kuwa 473,128 Me – 232,020, Ke – 241,108. Wenyeji wa Wilaya hii ni Wanyambo ingawa kutokana na kupakana na nchi jirani makabila mengine kama Wachiga, Wanyarwanda, warundi wanaishi hapa. Idadi ya Kaya ni 89,188 na wastani wa watu ni 4.8 kwa Kaya.
|
| |
|
| |
|
| |
|
| |
|
| |
HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA WILAYA |
| |
|
| |
Takwimu za Kiwilaya zinaonyesha kwamba pato la mtu (per capital) ni Tshs. 185,000/= kwa mwaka. Juhudi zinaendelea kufanyika katika sekta kuu za uzalishaji, huduma za jamii na sekta za huduma za kiuchumi ili kuboresha hali ya maisha ya wananchi. Shughuli kuu ni kilimo cha Kahawa kama zao la biashara, Ndizi na Maharage kama chakula na biashara na ufugaji wa wanyama hususan ng'ombe na mbuzi. Kazi za ajira na asilimia zake ni kilimo 85%, shughuli za biashara 3%, watumishi (kazi za ofisini) 3%, ufugaji 1%, kazi nyingine ndogo ndogo 3%.
|
| |
|
| |
|
| |
|
|