Chini ya sekta hii juhudi zilizofanyika ni pamoja na kujenga uwezo wa jamii katika kutambua na kuandaa mikakati ya kutatua matatizo yake yenyewe. Aidha Halmashauri ikishirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika kipindi cha kuanzia 1998 jumla ya vikundi vya Wanawake 82 na Wanawake binafsi 65 vilipatiwa mikopo yenye thamani ya Tshs 43,002,500.= na zikirejeshwa na Riba Tshs 3,447,500.= Hadi kufikia 31/08/2007 kiasi cha shs. 36,089,612.= sawa na asilimia 77.6 ya fedha zimerejeshwa. Juhudi zinaendelea za kurejesha fedha zilizosalia kiasi cha Tshs 11,229,388.=. Wilaya pia inaendelea kufanya ufuatiliaji wa urejeshaji kwa kushirikisha kamati za mikopo za kata, Watendaji wa kata na vijiji ambapo wadaiwa wapo. Kwa kutumia fedha zilizokusanywa Shs. 22,000,000/=,SACCOS 4 zimekopeshwa ikiwa ni mikopo kwa vikundi vya akina mama.
|