Utekelezaji katika sekta ya Ushirika unahusisha usimamizi, utoaji ushauri, ukaguzi wa vyama vya msingi na utoaji elimu ya ushirika kwa umma. Aidha juhudi kubwa inayofanyika ni kutafuta ufumbuzi juu ya matatizo ya ukosefu wa mtaji kwa chama kikuu cha Ushirika cha KDCU Ltd na pia kuboresha uongozi na uendeshaji wa Ushirika. Aidha vyama vya Akiba na Mikopo vimeongezeka kutoka 16 mwaka 2003/04 hadi 40 mwaka 2006/07 na wanachama wa Ushirika wameongezeka kutoka 12,413 mwaka 2003/04 hadi 16,516 mwaka 2006/07.
Idadi ya vyama vilivyoandikishwa ilikuwa 93 kuanzia 1994/95 ukilinganisha na 118 kwa 2006/07, hili ni ongezeko la asilimia 27%.
Ufungaji wa vitabu kwa 2006/07 uliongezeka toka vyama 87 2003/04 na kufikia vyama 109 na kuweza kukagua vyama vyote 109.
|