Wilaya ya Karagwe inavyo vyanzo vya maji vilivyoboreshwa kwa msaada wa miradi mbalimbali 126 na visima vifupi 118. Upatikanaji wa huduma ya maji umechangiwa na wananchi, Serikali na Wahisani mbalimbali. Hali hii inaonyesha kwamba mtandao wa upatikanaji unaojitosheleza umefikia vijiji 15 kati ya vijiji 109 vilivyopo visivyojitosheleza 75 kati ya 109, visivyo na vyanzo 27, mifuko ya maji 94 yenye thamani ya Shs.10,000,000.=. Wananchi wanaendelea kuhamasika kuunda mifuko ya maji pamoja na vikundi vya watumiaji maji. Jumla ya mifuko 94 imeundwa ikiwa na thamani ya Tshs. 10,000,000.=. Aidha usanifu unafanyika kwa ajili ya maandalizi ya kuombea ufadhili na kukarabati mradi wa maji wa Kayanga na Omurushaka (Kayanga, Omurushaka water master plan).
|
UGAVI WA MAJI SAFI NA TAKA
Maeneo ya miji inayokuwa kama ya Kayanga, Omurushaka, Murongo, Isingiro (kwa kuanzia) ukuaji wa maji safi na taka unapanuka haraka, uimarishaji wa mtandao wa maji safi na taka ni ya msingi ili kukuza wazo na shughuli za uwekezaji. Mji wenye mtandao mzuri wa maji safi , mengi na salama na pia mtandao uliopangiliwa na maji taka, ni eneo ambalo huvutia wawekezaji. Juhudi hapa ni kukazania mtandao ulioboreshwa ili kuvutia wawekezaji wa viwanda, biashara (maduka) na kukua kwa mji, mambo haya yote yataongeza kipato hivyo kukuza uchumi na kuboresha maisha ya mtu mmoja mmoja. Mategemeo mengine ya kuwa na mtandao mzuri wa maji safi na taka, kutoa fursa kwa miji kukua bila kuchafua mazingira au kusababisha kuenea magonjwa ya kuambukiza. |