Wilaya inayo maeneo yenye vivutio vikubwa vya uwekezaji kibiashara, maeneo hayo yakipata umeme yatavutia sana wawekezaji, maeneo hayo ni:-
Maporomoko ya Murongo ( Murongo Falls )
Eneo hili kwa mujibu wa tafiti kadhaa ambazo zilishafanyika likiwekezwa na kuhudumiwa ipasavyo, lina uwezo wa kuzalisha umeme unaoweza kutosheleza maeneo ya Wilaya ya Karagwe, Ngara, Biharamulo na Wilaya za Bukoba na Misenyi. Kupatikana kwa umeme huo utaleta nafuu ya maisha, kuongeza biashara, kuongeza kipato na hatimaye kupunguza umasikini
|