Kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma za ushauri Nasaha na upimaji wa VVU kwa hiari toka vituo 4 vilivyopo sasa hadi vituo 10.
Kuongeza idadi ya vituo vinavyotoa huduma za kuzuia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) toka vituo 2 vilivyopo sasa hadi 10.
Uimarisha kituo cha huduma, Tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) kilichopo Hospitali ya Chato kukifanyia ukarabati na kuongeza vifaa vya kupimia kama CD4 Count machine n.k.
Kupanua huduma za Tiba na matunzo (CTC) kwa kuanzisha vituo vingine vipya vine (4), ambavyo ni kituo cha Afya Bwanga, Zahanati za Katete, Kasenga na Buseresere.
Kuimarisha huduma za wagonjwa nyumbani kwa kuboresha mfumo wa ufuatiliaji na rufaa kwa kushirikisha vikundi mbalimbali vya kijamii (CBOs, NGOs na FBOs).
Kutambua na kuimarisha vikundi vya sanaa na maonyesho vinavyohamasisha mapambano dhidi ya UKIMWI.
Kuimarisha kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi ya kata vijiji na vitongoji.
|