JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
CHATO
 
 
 
WILAYA YA CHATO
 
[ Nyumbani ] au
 
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
 
UTAWALA UTUMISHI FEDHA BIASHARA ELIMU MAFUNZO YA UFUNDI VIJANA UTAMADUNI
KILIMO MIFUGO USHIRIKA UJENZI ARDHI USTAWI WA JAMII MIPANGO URATIBU
TAKWIMU AFYA MAJI MALIASILI MICHEZO MAENDELEO YA JAMII MAZINGIRA
...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
       

HALI YA WILAYA KWA UJUMLA

 
 

Chato ni mojawapo ya Wilaya mpya katika Mkoa wa Kagera yenye eneo la Kilometa za mraba 3,572 kwa upande wa Kaskazini Wilaya inapakana na Wilaya ya Muleba, Kusini inapakana na Wilaya ya Bukombe. Kwa upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Biharamulo na Mashariki ni Geita. Wilaya ipo kati ya nyuzi 2 0 15'- 3 0 15' Kusini mwa Ikweta na 31 0 - 32 0 mashariki mwa “Standard Meridian”. Pia wilaya iko kwenye mwinuko wa kati ya mita 1135 - 1410 usawa wa bahari.

 
 
 

UTAWALA

Wilaya ya Chato imegawanyika katika Tarafa tatu (3) za Buzirayombo, Bwanga na Nyamirembe. Pia inazo kata 14 zenye jumla ya Vijiji 76 na Vitongoji 445 . Makao Makuu ya Wilaya ni Chato.

IDADI YA WATU

Kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, Wilaya ilikuwa na Idadi ya watu 251261 kati ya hao 128,145 ni Wanawake na 123,119 ni wanaume. Kutokana na ongezeko la watu la 4.8% kwa mwaka, kwa mwaka 2007 Wilaya inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 318,240 yenye kaya 53,040 kwa wastani wa watu 6 kila kaya. Kutokana na takwimu hizo, Wilaya ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapatao 118,847 ambao ni sawa na asilimia 47.3 wakazi wote wa Wilaya hii.

 

 

MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA KATIKA WILAYA

Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chato ilifunguliwa rasmi tarehe 10.08.2006. tangu Taasisi hii ianze kazi zifuatazo zimetekelezwa:-

•  Kuanzia Agosti, 2006 hadi 2007 taarifa 112 zilipokelewa na kushughulikiwa.

•  Kuanzia Julai, 2007 hadi Desemba 2007 taarifa zilizopokelewa ni 93.

•  Hadi sasa kesi 5 zipo mahakamani.

TAKUKURU inaendelea na kazi za uelimishaji Umma, utafiti mdogo kubaini mianya ya rushwa katika taasisi mbalimbali na uchunguzi. Aidha, taarifa nyingi zinapokelewa kutoka kwa wananchi hazina mwelekeo wa rushwa hivyo huhamishiwa kwenye taasisi husika.

Katika kipindi cha mwak 2007, Klabu za wapinga rushwa 17 zimefunguliwa katika shule za sekondari 17 wilayani zikiwa na wanachama 1,568; kati yao wasichana ni 499 na wavulana ni 1,069.

Semina na mikutano 14 imefanyika ambapo wananchi takribani 5,468 walielimishwa.

Changamoto iliyopo ni kuendelea kuelimisha wananchi juu ya madhara ya rushwa na ufisadi ili waweze kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa.

 

 

 

 
 

HALI YA UCHUMI

Asilimia 90 (90%) ya wakazi wa wilaya ya Chato hutegemea kilimo kwa kujiongezea kipato. Asilimia 60% hujihusisha na biashara ndogondogo, asilimia 3% hutegemea uvuvi, asilimia 0.5% ni ajira ndogondogo na asilimia 0.5% ni ajira katika mfumo rasmi.

Chanzo kikuu cha mapato ya Wilaya hutegemea mauzo kutokana na mazao ya kilimo kama vile pamba, mihogo, mahindi. Mpunga/mchele, karanga. Pia ufugaji na mazao yake hutegemewa sana na wakazi wa Wilaya hii kutokana na asilimia 25% ni wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na bata.

MATUMIZI YA ARDHI

Matumizi ya ardhi yamegawanyika katika maeneo yafuatayo:

  • Kilimo - 55%
  • Malisho ya mifugo - 15%
  • Uvuvi - 2.5%
  • Hifadhi ya Misitu na Wanyama pori - 27.5%

HALI YA ULINZI NA USALAMA

Elimu ya Ulinzi Shirikishi imeendelea kutolewa kwa Wananchi na Wadau kwa ujumla. Vyombo vya Ulinzi vimeweka mikakati ya kupunguza kero ya uhalifu na ujambazi. Aidha operesheni mbalimbali ziliendeshwa kwa kuwasaka na kuwashughulikia wahalifu kisheria. Kamati za ulinzi kuanzia ngazi za Vitongoji, Vijiji, Kata, Tarafa hadi Wilaya zimeendelea kufanya kazi ya ziada kuimarisha Ulinzi na kudhibiti matukio ya Uhalifu. Hii ni pamoja na doria za mara kwa mara kwa kushirikisha vyombo vyote vya Ulinzi.

CHANGAMOTO

Huduma za mahakama ya Wilaya zimekuwa zikipatikana katika wilaya ya Biharmulo Km. 60 kutoka Chato. Hali hiyo inasababisha Jeshi la Polisi na Mashahidi kuingia gharama kubwa za usafirishaji na hatimaye mashahidi kujitoa na kusababisha haki kushindwa kutendeka. Mazingira hayo yanasababisha kuwepo kwa malalamiko mengi. Kutokana na hali hiyo Wilaya inaomba Mahakama na Gereza la Wilaya ili kupunguza kero kwa wananchi.

 

 
       
       
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/18, FAX: 028-2221356