SEKTA YA KILIMO (MAZAO)
Uzalishaji wa Mazao msimu uliopita wa 2006/07 na mavuno
Utekelezaji wa malengo ya Kilimo kwa msimu wa 2006/07 kwa Wilaya ya Chato ni kama inavyooneshwa hapa chini
Mazao ya Chakula
Na. |
Zao |
Lengo (Ha.) |
Matarajio ya Mavuno (MT) |
Utekelezaji (Ha.) |
Mavuno Halisi (MT) |
1. |
Mahindi |
23,346 |
29,265 |
22,916 |
34,082 |
2. |
Maharage |
7,499 |
3,235 |
7,124 |
3,749 |
3. |
Mtama (chakula) |
3,969 |
5,556 |
709 |
993 |
4. |
Muhogo |
27,874 |
139,400 |
28,226 |
225,808 |
5. |
Viazi vitamu |
10,859 |
43,412 |
7,958 |
31,832 |
6. |
Mpunga |
2,000 |
3,778 |
1,760 |
5,280 |
7. |
Karanga |
2,967 |
2,047 |
2,087 |
1,460 |
8. |
Ulezi |
622 |
313 |
427 |
214 |
9. |
Uwele |
287 |
255 |
216 |
130 |
|
Jumla |
79,423 |
227261 |
71,423 |
303,548 |
Kutokana na takwimu ya idadi ya watu Wilayani Chato kwa mwaka 2007, mahitaji halisi ya chakula ni MT 95,472 ya nafaka kavu (baada ya kutoa maji maji). Kutokana na mavuno ya msimu wa 2006/2007 MT. 303,548 ya nafaka na mihogo, Wilaya ina ziada ya MT. 208,076
Mazao ya Biashara
Na. |
Zao |
Lengo (Ha.) |
Matarajio ya Mavuno (MT) |
Utekelezaji (Ha.) |
Mavuno (MT) |
1. |
Pamba |
14,052 |
12646.8 |
8,072 |
3,238 |
Hali ya Mvua Kwa Msimu wa 2007/08
Katika msimu wa kilimo 2007/2008, mvua zilianza kunyesha mapema sana, Mvua zimeanza kunyesha katikati ya mwezi wa Agosti kama jedwali linavyoonyesha hapa chini:
Mwezi |
Kiasi (mm) |
Idadi ya siku |
Agosti |
85.9 |
4 |
Septemba |
80.3 |
2 |
Oktoba |
60 |
3 |
Novemba |
164.1 |
14 |
Hadi Desemba,31 |
113.2 |
9 |
Jumla |
503.5 |
32 |
Pamoja na mvua kuanza mapema, zimeendelea kunyesha katika mtiririko/mtawanyiko mzuri kiasi cha kufanya mazao yaliyoko mashambani kuwa katika hali ya kuridhisha. Kwa mazao yaliyopandwa katikati ya Oktoba halikadhalika yanaendelea kukua vizuri
Ununuzi wa Mazao ya Biashara Msimu 2006/07
(i) Pamba:
Msimu wa ununuzi wa pamba ulifunguliwa tarehe 25/6/2007 . Jumla ya kampuni 6 za Kahama oil Mills, Kahama Cotton Company, Mass Trading Company, Cop - Cot Company, Birchand na Dimond Ginning Company zilipewa kibali cha kununua pamba mbegu Wilayani. Hadi Novemba, 2007 jumla ya Kg 3,238,047 zimenunuliwa. Bei ya kuuzia kwa kilo ilikuwa kati ya Tshs. 325/= hadi Tshs. 550/=. Bei hizi ni kwa wastani wa Tshs. 437.50 kwa kilo. Wananchi walijipatia jumla ya Tshs. 1,416,645,563/=.
Hali ya Pembejeo kwa Msimu 2006/07
Upatikanaji wa mbegu bora za Mahindi na mtama zimekuwa zikipatikana kwa wafanya biashara binafsi. Wafanya biashara wa pembejeo hizi wanapatikana katika Kata za Buziku, Bwanga, Chato, Buseresere na Muganza.
Aidha, Wilaya ilipata mbolea ya ruzuku aina ya UREA Tani 5 na zilisambazwa kwa walengwa na ilitumika sana katika maeneo yanayolima kilimo cha bustani kandokando mwa ziwa Victoria.
Upatikanaji wa Pembejeo kwa Msimu wa 2007/08
Wilaya ya Chato na Mkoa wa Kagera kwa ujumla haimo katika orodha ya Wilaya zitakazostahili kupata mbolea ya ruzuku. Hii ni kufuatia maelezo ya Wizara kupeleka mbolea katika mikoa maalumu inayolima nafaka kwa wingi. Hata hivyo yako maduka ya pembejeo za kilimo katika miji ya Chato,Buziku,Buseresere na Muganza.
Matumizi ya mbolea bado yako chini, hata hivyo wakulima wanaendelea kupewa elimu juu ya matumizi ya mbolea za viwandani, samadi na mboji kupitia mashamba darasa. Wilaya pia imepokea viuwadudu vya zao la pamba kiasi cha chupa 25,600 zenye ujazo wa 200ml toka Bodi ya Pamba na usambazaji kwa wakulima unaendelea wilayani kote.
Hali ya Kilimo cha Wanyamakazi
Wilaya ya Chato kwa sehemu kubwa inafaa kuendesha shughuli za kilimo kwa kutumia zana mbalimbali zinazokokotwa na wanyamakazi. Aidha kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya wanyamakazi katika shughuli za kilimo.
Aidha katika msimu wa kilimo wa 2006/2007, jumla ya kaya 2,387 kati ya 47,736 sawa na asilimia 5% zinatumia wanyamakazi katika shughuli za kilimo.
Katika Msimu wa Kilimo wa 2007/08 Wilaya imepokea zana mbalimbali zinazokokotwa na wanyamakazi toka Ofisi ya Kanda Umwagiliaji kama ifuatavyo:Ox-Plough 8,Magoye rippers 8,Cultivators/weeders 8,Jab Planters 2,Direct Seeder1na chains 8 na zana hizi zimesambazwa katika vikundi vya wakulima vilivyopatiwa mafunzo na baadhi ya zana hizi zitarudishwa katika kituo cha mafunzo Buziku (OTC) kikishakamilika.
|