Hali ya Ulaji wa Nyama na Unywaji wa Maziwa
Mazao ya mifugo yanayopatikana ndani ya wilaya ni maziwa ya ng'ombe, Nyama ya ng'ombe na ile ya wanyama wadogo pamoja na ndege. Ng'ombe 5,011 mbuzi 4,665 na nguruwe 59 walichinjwa na kuzalisha nyama kilogramu 652,100 yenye thamani ya Tshs. 1,173,780,000 kwa mwaka 2007, ukilinganisha na kilogramu 400,860 yenye thamani ya Tshs. 601,290,000 kwa mwaka 2006. , Aidha inakadiliwa kuwa zaidi ya Lita 14,230,080 za maziwa zilizalishwa kwa mwaka 2007. Kutokana na takwimu hizo wastani wa unywaji wa maziwa kwa mtu mmoja ni lita 45 kwa mwaka.
|