Maendeleo ya Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS)
Wilaya ina vyama vya Ushirika kama ifuatavyo:-
SACCOS 19 zenye wanachama 3,086, AMCPS 28, Chama cha Wavuvi 1. Pia kuna vikundi vidogo vidogo 323 vya uzalishaji mali ambavyo vimejiunga na SACCOS. Aidha kuna Chama cha Ushirika 1 (BCU).
Hisa zilizokusanywa toka katika SACCOS ni Tshs. 29,586,000/=, akiba zilizokusanywa ni Tshs. 274,376,000/= na amana ni Tshs. 317,985,000/=. Jumla ya mtaji ni Tshs. 621,947,000/=. Mikopo iliyokopeshwa ni Tshs. 854,800,000/=. Mikopo iliyorejeshwa ni Tshs. 356,657,000/= na ambayo bado kurejeshwa ni Tshs. 498,143,000/= ambayo iko katika mzunguko.
Awamu ya Kwanza ya Utekelezaji wa Mpango wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Halmashauri ya Wilaya kupitia Afisa Ushirika na Madiwani katika maeneo yao iliwahamasisha wananchi kujiunga kwa wingi katika SACCOS zilizopo katika maeneo yao ili waweze kuboresha miradi yao binafsi kwa kuomba mikopo yenye riba nafuu katika awamu ya kwanza. Maombi 427 yenye thamani ya Sh. 1,512,099,000 yalipokelewa NMB Tawi la Biharamulo. Maombi matatu ya Mwambao SACCOS, Mshikamano SACCOS na Angaza SACCOS yenye thamani ya Tshs. 100,000,000 lilipokelewa na kukopewshwa.
Mpaka kufikia tarehe 31, Desemba 2007 Mwambao SACCOS imekwisha rejesha CRDB Tshs.41,000,000, fedha ambazo bado hazijarejeshwa zipo katika mizunguko.
|