JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
CHATO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

MAJI

 

Lengo kuu la sekta hii ni kuendeleza na kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya hii kwa kutumia teknolojia sahihi na rahisi inayokubalika na yenye gharama nafuu kiuendeshaji.

Wilaya ya Chato ina watu 318,240 kati yao wakazi 72,867 ambao ni 23% ya wakazi wote wanapata maji safi na salama kutokana na vyanzo kama inavyoonyeshwa katika jedwali hapo chini. Pia Inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2010 idadi ya Wakazi 190,944 sawa na 60% ya wakazi wote Wilayani watapata maji safi na salama kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira.

 
 
 
 
Hali ya Upatikanaji Maji Wilayani Chato
 

 Na

Aina yachanzo

Idadi ya vyanzo

Watu wanao hudumiwa

%

1.

Miradi ya Bubujiko

1

12,717

17

2.

Visima vifupi

149

44,700

61

3.

Visima Virefu

29

8,700

12

4.

Matanki ya kuvuna maji ya mvua

35

6,750

9

5.

Miradi ya maji ya nguvu ya pump diesel/Solar

14

42,00

0.1

Jumla

228

72,867

100

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
Matatizo yanayokabili huduma ya maji
 
  • Uharibifu wa vyanzo vya maji unaotokana na ukataji miti, uotaji wa miti inayotumia maji mengi katika ukuaji, ufugaji usiopangiliwa, ujenzi wa makazi kwenye vyanzo vya maji
  • Uhaba wa vyanzo vya maji
  • Ongezeko kubwa la watu lisiloendana na matumizi endelevu ya raslimali zilizopo
  • Gharama kubwa ya uendeshaji na ukarabati wa miundo mbinu ya maji
 
 
 
Mikakati ya Utatuzi
 
  • Kuelimisha jamii zana ya utunzaji wa vyanzo vya maji.
  • Kutunga sheria ndogo ya kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji.
  • Kuhusisha sekta binafsi katika uendeshaji wa miradi ya maji
  • Kuendeleza jitihada za kuimarisha vyanzo vya maji vya asili
  • Kushirikiana na Sekta ya Afya katika suala zima la Uzazi wa Mpango wa uzazi
  • Kuendeleza miradi ya maji yenye kutumia teknolojia rahisi na yenye gharama nafuu kiuendeshaji.
  • Kuhusisha jamii katika utunzaji endelevu wa miradi ya maji.

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
 
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/18, FAX: 028-2221356