JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
CHATO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

Mazingira

 

Katika kukabiliana na uharibifu huo, Wilaya imeweka mikakati ifuatayo ambayo inaendelea kutekelezwa:

•  Kuwaondoa wavamizi wafugaji na mifugo kwenye maeneo waliyovamia: “Operation” ya kuondoa mifugo katika misitu ya hifadhi na mapori imefanyika.

•  Matumizi bora ya teknolojia ya nishati: Katika suala la kuhifadhi misitu, wilaya inaendeleza teknolojia ya matumizi bora ya nishati kwa kutengeneza majiko sanifu.

•  Kuwa na Mpango kamambe wa matumizi bora ya ardhi uwe umehuishwa na kusambazwa vijijini. Mafunzo juu ya matumizi bora ya ardhi yametolewa katika vijiji 74 na vijiji vyote vimeshatengeneza Mipango kamambe wa matumizi bora ya ardhi. Kazi iliyopo sasa ni kuihuisha mipango hiyo.

•  Kuwajibisha Uongozi wa eneo husika utakaoshindwa kutekeleza zoezi la kudhibiti matukio ya moto katika maeneo yao. Viongozi wa ngazi zote wameshaelekezwa juu ya suala hili.

•  Operesheni ya kukamata mkaa, kuni na mbao inaendelea kufanyika na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

 

Athari za Uharibifu wa Mazingira
 

Kutokana na shughuli hizo zinazofanywa na binadamu zipo athari za dhahiri kama ifuatavyo:

•  Kutoweka au kupungua kwa kiwango kikubwa cha raslimali zilizopo kwa kutozingatia uvunaji endelevu.

•  Uharibifu mkubwa wa mazingira ambao unaweza kusababisha maeneo haya kugeuka jangwa

•  Uchafuzi wa vyanzo vya maji unaosababishwa na wachimbaji wa dhahabu kutumia maji ya mito kuoshea madini

•  Kutoweka kwa misitu kunakosababishwa na uchomaji moto misitu ovyo

•  Ardhi inayotumika kukosa rutuba kunakotokana na matumizi yasiyozingatia kanuni za kilimo bora.

Kutokana na hali hiyo, Wilaya imefanya na inaendelea kufanya jitihada za kuokoa hali hiyo kwa:

•  Kuwataka wavamizi watoke kwenye maeneo hayo pamoja na wachimbaji wadogo wadogo wa madini ambao wanafanyiwa utaratibu wa maeneo mbadala.

•  Operesheni ya kukamata mkaa, kuni na mbao inaendelea kufanyika na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

•  Elimu imekuwa ikitololewa kwa wananchi wanaochafua vyanzo vya maji kwa kuezeza athari kubwa zinazoweza kutokea kutokana na shughuli hizo. Elimu hii imekuwa ikitolewa kupitia Wataalamu na Viongozi mbalimbali kupitia mikutano mbalimbali.

 

 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 0282752184