JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BIHARAMULO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 

AFYA

Sekta hii imeendelea kutekeleza sera ya afya (Tiba na Kinga).

Huduma za Tiba

Wilaya ina jumla ya vituo 17 vinavyotoa h uduma za tiba na kinga kama inavyoonyeshwa katika mchanganuo ufuatao:

Aina

Serikali

NGOs

Binafsi

Jumla

Hospitali

-

1

-

1

Vituo vya Afya

2

-

-

2

Zahanati

12

-

2

14

JUMLA

14

1

2

17

 

MATATIZO MAKUU YA KI-AFYA YALIYOJITOKEZA

•  Ongezeko la vifo vya akina mama vinavyotokana na sababu za uzazi

•  Ongezeko la vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano

•  Ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa malaria katika jamii

•  Ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI katika jamii

•  Ongezeko la wagonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma waliogunduliwa.

 

MALENGO NA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI KATIKA MPANGO WA MWAKA 2007/08

 

Na.

Lengo

Mikakati ya Utekelezaji

1.

Kupunguza vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano kutoka kiwango cha 251/1000 mpaka 200/1000 ifikapo Juni, 2008

•  Kufundisha watumishi kuhusu tiba sahihi ya magonjwa ya watoto (IMCI)

•  Kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwahi hospitali na matunzo ya wagonjwa

•  Kuimarisha huduma za mkoba (Outreach)

 

2.

Kupunguza vifo vya wazazi kutoka 101/100,000 hadi 100/100,000 ifikapo Juni, 2008

•  Kununua gari moja la wagonjwa la Kituo cha Afya

•  Kununua “radio call” kwa ajili ya zahanati 5

•  Kuhamasisha jamii kuhusu vikwazo vya uzazi na umuhimu wa kuwahi hospitali

•  Kuhamasisha jamii kuhusu uzazi wa mpango

•  Kufuatilia vifo vya wazazi hospitalini na katika jamii

3.

Kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kutoka wagonjwa 18,648/100,000 hadi wagonjwa 16,800/100,000 ifikapo Juni, 2008

•  Kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya chandarua

•  Mafunzo ya tiba sahihi ya malaria

4.

Kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka asilimia 19 hadi 18 ifikapo Juni, 2008

•  Kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga naUKIMWI

•  Kufundisha wataalamu kuhusu ushauri nasaha

•  Kufundisha wakunga wa jadi mbinu za kuzuia maambukizi ya UKIMWI

5.

Kupunguza maambukizi ya Kifua Kikuu na Ukoma kutoka wagonjwa 323 hadi kufikia 303 (kifua kikuu) na wa ukoma kutoka 4/1000 hadi 1/1000 ifikapo Juni, 2008

•  Kufundisha watumishi 10 juu ya matumizi ya darubini ili kugundua wagonjwa wapya na kupewa tiba

•  Kuimarisha huduma za mkoba za Kifua Kikuu na Ukoma

6.

Kuinua kiwango cha usafi wa mazingira katika jamii kutoka 52% hadi kufikia 60% ifikapo Juni, 2008

•  Kukusanya na kusomba taka kila mwezi

•  Kutoa elimu ya usafi wa mazingira katika jamii

•  Kujenga vyoo 2 katika masoko ya Buseresere na Kasenda

•  Kupima afya za wanafunzi shuleni

•  Kupima maji ya visima na kuimarisha ufuatiliaji

 

 


 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 

HALI YA UKIMWI WILAYANI

Hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI inaendelea kushuka, katika vipindi tofauti kama inavyoonyeshwa katika takwimu zifuatazo:-

 

HALI YA UPIMAJI WA HIARI WA VIRUSI VYA UKIMWI-KAMPENI YA KITAIFA ILIYOZINDULIWA RASMI KI-WILAYA TAREHE 22-9-2007

LENGO LA WILAYA KATIKA UPIMAJI

Lengo la Wilaya lilikwa ni kupima idadi ya watu 8,700, lakini kutokana na

kushirikisha jamii kwa kutoa elimu juu ya faida ya kupima kwa hiari, kushirikisha wadau mbali mbali kama vile mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Mashirika ya kijamii, na Mashirika ya Dini kabla ya utekelezaji wa zoezi zima la upimaji limeleta mafanikio makubwa katika kufanikisha zoezi hilo .

Katika utekelezaji wa kampeni ya upimaji wa hiari, uhamasishaji wa jamii kwa njia ya sanaa, Mikutano ngazi ya jamii, kujituma kwa Watendaji na Viongozi mbali mbali, kumewezesha Wilaya kuvuka lengo la kupima watu 8,700, hivyo kupelekea Mkoa kutoa lengo la pili la idadi ya watu 15,000, ambapo Mpaka kufikia mwezi Desemba 2007 Jumla ya Watu waliojitokeza kupimwa imefikia 24,491 . Wilaya ilikuwa na idadi ya vituo 28 (VCT) vilivyotumika katika upimaji wa VIRUSI VYA UKIMWI)

 

MAPUNGUFU YALIYOJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA UPIMAJI

  • Kutopatikana vifaa kwa wakati, ikiwa ni wakati wa upimaji wa hiari na wakati zoezi la upimaji unaendelea.
  • Kuwa na wataalamu wachache(Watoa ushauri nasaha ).
  • Kuchelewa kwa fedha kwa ajiri ya zoezi la upimaji.

MAPUNGUFU YA JUMLA KATIKA KUKABILIANA NA MAAMBUKIZI YA VVU NA UKIMWI KATIKA WILAYA.

•  Kutokuwepo gari maalumu kwa ajiri ya shughuli za UKIMWI

•  Upungufu wa watoa ushauri nasaha

•  Kuwa na kituo kimoja kwa ajiri ya utoaji wa dawa za kurefusha maisha (ARV)

•  Ukosefu wa huduma ya chakula kwa watu wanaotumia dawa za ARV hasa kwa wale ambao wana utapiamlo, hivyo wengine kukata tamaa ya kuendelea kutumia dawa.

•  Ukosefu wa fedha kwa ajiri kufundishia Kamati za kudhibiti UKIMWI ngazi za Kata,Vijiji na Vitongoji.

MIPANGO YA BAADAYE YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA UKIMWI KATIKA WILAYA

  1. Kutoa elimu lika katika Shule za Msingi na Sekondari.
  2. Kushirikiana na wadau mbali mbali hasa ngazi ya jamii kutoa huduma kwa Wagonjwa wa UKIMWI.
  3. Kuendelea kutoa elimu ya kuzuia maambukizi ya VVU na UKIMWI kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto. (PMCT).
  1. Kutoa huduma ya kutibu magonjwa ya ngono.
  2. Kuhimiza matumizi ya Kondomu.
  3. Kutoa huduma ya wagonjwa wa UKIMWI, na wanaoishi na VVU.
  4. Kutoa elimu ya kupunguza unyanyapaa kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI.
  5. Kusaidia watoto Yatima kwa kuishirikisha zaidi jamii.
  6. Kuendeleza vikundi vya usanii ili viweze kutoa elimu ya kujikinga na maabukizi ya VVU na UKIMWI, kwa kutumia njia ya sanaa.
  7. Kupanua huduma ya Vituo vya kutolea dawa za kurefusha maisha kutoka kituo kimoja kwa sasa hadi kufikia vituo vitatu

: MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA MAPAMBANO YA VVU NA UKIMWI

  1. Kupanua huduma za upimaji kwa hiari kutoka vituo 4 mwaka 2005 hadi kufikia vituo 15 kufikia Desemba 2007.
  1. Kiasi cha shilingi 19,852,600/= zimetolewa kuviwezesha vikundi vya kijamii 12 vinavyojishughulisha na kupambana na UKIMWI, vinavyotoa huduma kwa watoto Yatima, Wagonjwa wa UKIMWI , Wajane na kutoa elimu, fedha iliyotolewa na TACAIDS kupitia wakala wake TANESA.
  1. Kutoa elimu ya kutokomeza unyanyapaa kwa watu wenye VVU na UKIMWI katika Kata 5 kati ya Kata 8, zilizo katika Wilaya, mafunzo yaliyotolewa na Shirika la ACORD kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya.

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa KAGERA, BUKOBA, TEL: 028 - 2222341/18, FAX: 028-2221356