JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BIHARAMULO
 
 
 
WILAYA YA BIHARAMULO
 
[ Nyumbani ] au
 
[ MKUU WA WILAYA ] [ WABUNGE ] HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO [IDARA & TAASISI ]
 
UTAWALA UTUMISHI FEDHA BIASHARA ELIMU MAFUNZO YA UFUNDI VIJANA UTAMADUNI
KILIMO MIFUGO USHIRIKA UJENZI ARDHI USTAWI WA JAMII MIPANGO URATIBU
TAKWIMU AFYA MAJI MALIASILI MICHEZO MAENDELEO YA JAMII MAZINGIRA
...............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
   

HALI YA WILAYA KWA JUMLA

 
 

Biharamulo ni mojawapo ya wilaya nane za Mkoa wa Kagera yenye eneo la kilometa za mraba 5,627. Kwa upande wa Kaskazini Wilaya inapakana na Wilaya za Muleba na Karagwe, Kusini inapakana na Wilaya za Kibondo na Bukombe. Kwa upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Ngara na Mashariki inapakana na Wilaya ya Chato. Wilaya ipo kati ya nyuzi 2 0 15' – 3 0 15' Kusini mwa Ikweta na 31 o – 32 o Mashariki mwa “Standard Meridian ”. Pia Wilaya iko kwenye mwinuko wa kati ya mita 1135 – 1650 kutoka usawa wa bahari.

 

 

UTAWALA

Wilaya ya Biharamulo imegawanyika katika Tarafa mbili (2) za Nyarubungo na Lusahunga. Pia inazo Kata 8 zenye jumla ya Vijiji 49 vyenye Vitongoji 299.

 

IDADI YA WATU

Kutokana na sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, Wilaya ina idadi ya watu 162,181 kati ya hao 82,716 ni wanawake na 79,465 ni wanaume. Kutokana na wastani wa ongezeko la 4.8% la mwaka,kwa mwaka 2007 Wilaya inakadiriwa kuwa na watu 198,066. Pia Wilaya ina idadi ya kaya 27,066 zenye wastani wa watu 6 kwa kila kaya. Kutokana na takwimu hizo, Wilaya ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapatao 76,712 ambao ni sawa na asilimia 47.3 ya wakazi wote wa Wilaya hii.

HALI YA ULINZI NA USALAMA

Hali ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya hii kwa sasa ni shwari. Hali hii inatokana na elimu ya uhamasishaji wa Serikali ikishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP). Aidha Kamati za Ulinzi na Usalama za ngazi zote kwa kushirikiana na Wananchi ziliendelea kufanya doria za mara kwa mara na kutoa ushirikiano wa kutosha katika kudhibiti uhalifu.

 
KANDA ZA KILIMO

Wilaya imegawanyika katika kanda kuu tatu (3) za Kilimo:

•  Ukanda wa Mashariki: wenye udongo wa kichanga na wenye rutuba hafifu. Mazao yanayostawisha ni pamba, tumbaku, migomba, mihogo, mtama, mpunga, mahindi na viazi vitamu. Pia asilimia 85% ya mifugo wilayani hupatikana katika kanda hii.

•  Ukanda wa Kati: Kanda hii iko katikati ya Wilaya, ikiwa na mwinuko wa mita 1250 – 1700 toka usawa wa bahari. Kanda hii inapata kiasi cha mvua kati ya mm 800 – 1000. Mazao yanayolimwa ni Migomba, Mahindi, Maharage, Mpunga, Viazi Vitamu, Mtama na Muhogo. Kahawa na Tumbaku ni mazao makuu ya biashara katika kanda hii. Mifugo inayopatikana katika kanda hii ni ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku.

•  Ukanda wa Magharibi: UKanda huu sehemu kubwa ni misitu ya hifadhi ambayo hupata mvua kiasi cha mm 900 – 1000. Mazao yanayostawishwa katika ukanda huu ni Kahawa, Tumbaku, Muhogo, Viazi vitamu, Mahindi, Mtama na Maharage. Mazao mengine ya misitu hupatikana katika ukanda huu.

HALI YA UCHUMI

Asilimia 90 (90%) ya wakazi wa Wilaya ya Biharamulo hutegemea kilimo kwa kujiongezea kipato. Asilimia 6% hujihusisha na biashara ndogo ndogo na asilimia 4% ni ajira katika mfumo rasmi.

Chanzo kikuu cha mapato ya Wilaya hutegemea mauzo kutokana na mazao ya kilimo kama vile pamba, mihogo, mahindi, mpunga/mchele, karanga na tumbaku. Pia ufugaji na mazao yake hutegemewa sana na wakazi wa Wilaya hii kutokana na asilimia 25% ni wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku na bata.

 

 

   
   
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 028-2752184