JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BIHARAMULO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
SEKTA YA KILIMO (MAZAO)
 

Hali ya Mvua

Katika msimu wa kilimo 2006/2007, mvua zilianza kunyesha kwa kuchelewa, na baadaye kunyesha kwa wingi kama inavyoonyesha hapo chini: -

Na.

Mwezi

Kiasi (mm)

Idadi ya siku

1.

Julai

0.5

-

2.

Agosti

12.6

2

3.

Septemba

15.2

2

4.

Oktoba

46.1

8

5.

Novemba

246

16

6.

Desemba

211.9

23

7.

Januari, 2007

81.6

9

8.

Februari

71.2

9

9.

Machi

144.6

13

10.

Aprili

126.3

12

11.

Mei

85.9

3

12

Juni

69.8

3

13.

Julai

-

-

Hakuna athari za kimaumbile ambazo zimejitokeza, aidha zao la Maharage liliathirika sana kutokana na mvua nyingi zilizonyesha mwezi wa Novemba na Desemba 2006.

 

Uzalishaji wa Mazao msimu uliopita wa 2006/07 na mavuno

Utekelezaji wa malengo ya Kilimo kwa msimu wa 2006/07 kwa Wilaya ya Biharamulo ni kama inavyooneshwa hapa chini:

Mazao ya Chakula

Na.

Zao

Lengo (Ha.)

Utekelezaji (Ha.)

Matarajio ya Mavuno (MT)

Mavuno Halisi

(MT)

1.

Mahindi

11,356

10,902

14,254

15,262

2.

Maharage

10,124

7,867

4,557

5,507

3.

Mtama (chakula)

2,021

2,260

2,848

3,242

4.

Mhogo

10,240

9,931

46,505

79,448

5.

Viazi vitamu

6,746

5,036

26,116

25,180

6.

Mpunga

242

239

483

717

7.

Karanga

1,646

1,003

1,151

702

8.

Ulezi

606

416

302

188

9.

Uwele

72

81

65

48

10.

Ndizi

2,533

2,510

20,040

20,080

 

Jumla

46,625

40,245

116,321

 

150,374

Kutokana na takwimu ya idadi ya watu Wilayani Biharamulo kwa mwaka 2007, mahitaji halisi ya chakula ni MT.50, 461.3 ya nafaka kavu (baada ya kutoa maji maji). Kutokana na mavuno ya mwaka huu ya MT. 150,374 ya nafaka ikiwemo mihogo mibichi, Wilaya ina ziada ya MT. 99,912.7 ikiwemo mihogo mibichi.

Mazao ya Biashara

Hali ya Mvua Kwa Msimu wa 2007/08

Katika msimu wa kilimo 2007/2008, mvua zilianza kunyesha mapema sana, Mvua zimeanza kunyesha katikati ya mwezi wa Agost kama jedwali linavyoonyesha hapa chini:

Na.

Mwezi

Kiasi (mm)

Idadi ya siku

 

Agosti

61.6

5

 

Septemba

83.8

4

 

Oktoba

65.8

6

 

Novemba

129.9

8

 

Hadi Desemba, 10

20.6

5

 

Hivyo kutokana na kuwahi kwa majira ya mvua isivyo kawaida baadhi ya Wakulima wametumia mvua hizi kulima na mazao mengi ya haya karibu yataanza kuvunwa ifikapo mwishoni mwa desemba. Aidha mazao yaliyopandwa msimu wa kawaida katikati ya oktoba yanaendelea vizuri.

 

Malengo na Matarajio ya mavuno msimu 2007/08

Malengo na matarajio ya mavuno kwa msimu wa mwaka 2007/2008 Kwa Wilaya ya Biharamulo ni kama inavyooneshwa hapo chini.

Mazao ya Chakula

Na.

Zao la Chakula

Lengo (Ha)

Matarajio ya Mavuno (MT)

1

Mahindi

11,356

19,873

2

Mtama

2,034

3,305

3

Mhogo

9,301

58,131

4

Maharage

10,124

4,557

5

Viazi Vitamu

6,529

27,664

6

Mpunga

242

595

7

Migomba

2,533

41,793

8

Karanga

1,646

1,151

9

Ulezi

606

302

10

Mawele

72

72

 

JUMLA

44,443

157,443

Mazao ya Biashara 

Na.

Zao la Biashara

Lengo (Ha)

Matarajio ya Mavuno (MT)

1

Pamba

3,716

4,645

2

Tumbaku

66

71.4

3

Kahawa

702

737

4

Mtama Pombe

3,456

3,888

 

JUMLA

7,940

9,341.4

 

Tumbaku ya mvuke ndiyo iliyolimwa msimu huu kwa majaribio na kuacha kulima Tumbaku ya hewa

 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

UNUNUZI WA MAZAO YA BIASHARA MSIMU 2006/07

 

Pamba:

Msimu wa ununuzi wa pamba ulifunguliwa tarehe 25/6/2007 . Jumla ya kampuni 5 za Kahama oil Mills, Kahama Cotton Company, Mass Trading Company, Cop - Cot Company na Dimond Ginning Company zilipewa kibali cha kununua pamba mbegu Wilayani. Hadi Novemba,2007 jumla ya Kg 890,093 zimenunuliwa. Bei ya kuuzia kwa kilo ilikuwa kati ya Tshs. 350/= hadi Tshs. 550/=.

 

  Kahawa :

Zoezi la ununuzi wa kahawa limemalizika. Jumla ya kampuni 2 za Nile Commercial Company na Tanganyika instant Cofee zilipewa kibali cha kununua kahawa. Hadi kufikia tarehe Novemba, 2007 jumla ya Kg 8,131 za Kahawa ya maganda zimenunuliwa. Bei ya kuuzia kwa kilo ilikuwa Tshs. 500/ = hadi Tshs 550.

 

Tumbaku :

Jumla ya MT Kg 53,430 za Tumbaku ya hewa zimenunuliwa na kampuni ya ATTT kwa bei ya Tsh. 1,000/= hadi Tshs. 1,900/= kwa kilo.

 

HALI YA PEMBEJEO KWA MSIMU 2006/07

  Upatikanaji wa mbegu bora za Mahindi kutoka kwa Wafanya biashara binafsi umeendelea kuwa mzuri na wakulima wamehamasika kuzitumia. Wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wanapatikana katika mji mdogo wa Runazi na Biharamulo.

 

UPATIKANAJI WA MBOLEA YA RUZUKU NA USAMBAZAJI WAKE.

  Wilaya ya Biharamulo na Mkoa wa Kagera kwa ujumla haimo katika orodha ya Wilaya zitakazostahili kupata mbolea ya ruzuku.

 

HALI YA KILIMO CHA WANYAMAKAZI

Wilaya ya Biharamulo kwa sehemu kubwa inafaa kuendesha shughuli za kilimo kwa kutumia zana mbalimbali zinazokokotwa na wanyamakazi. Aidha kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya wanyamakazi katika shughuli za kilimo kama inavyooneshwa katika jedwali hapa chini:-

 

Tarafa

Zana

Mwaka 2004

Mwaka 2006

0ngezeko

Idadi

%

Nyarubungo

Plau za ng'ombe

291

342

51

18

Maksai

1,162

1,366

204

18

Mikokoteni

16

30

14

88

Lusahunga

Plau za ng'ombe

135

178

43

32

Maksai

538

710

172

32

Mikokoteni

10

30

20

200

Jumla Wilaya

Plau za ng'ombe

425

519

94

22

Maksai

1,700

2,076

376

22

Mikokoteni

26

60

34

131

 

Aidha katika msimu wa kilimo wa 2006/2007, jumla ya kaya 409 sawa na asilimia 1.7 zinatumia wanyamakazi katika shughuli za kilimo

 

HUDUMA ZA UGANI

Hali ya Maafisa Ugani katika Wilaya ni kama inavyooneshwa hapa chini:

 

KATA

Idadi Kaya zote

Kaya Shiriki Kilimo

Wanaohitaji (kuzingatia uwiano wa 1:700)

Maafisa ugani waliopo

Upungufu

B'mulo mjini

6819

6398

9

3

6

Nyarubungo

4226

3063

4

2

2

Runazi

3829

3817

5

2

3

Nyabusozi

2855

2282

3

1

2

Nyamigogo

1614

1284

2

1

1

Lusahunga

3120

2496

4

2

2

Kalenge

3605

2884

4

1

3

Nyakahura

1998

1652

2

2

0

Jumla

28,066

23,876

34

14

20

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/18, FAX: 028-2222341/2221356