HALI YA ULAJI WA NYAMA NA UNYWAJI WA MAZIWA
Mazao ya mifugo yanayopatikana ndani ya wilaya ni maziwa ya ng'ombe. Nyama ya ng'ombe na ile ya wanyama wadogo pamoja na ndege zaidi ya ng'ombe 2,326 mbuzi 3,387 na nguruwe 163 walichinjwa na kuzalisha nyama zaidi ya kilogramu (carcase weight) 288,960 kwa mwaka 2006, ukilinganisha na kilogramu 264,150 kwa mwaka 2005. Aidha inakadiliwa kuwa zaidi ya Lita 6,658,974 za maziwa zilizalishwa kwa mwaka 2006/07. Kutokana na takwimu hizo wastani wa unywaji wa maziwa ni lita 30.3 kwa mwaka.
UJENZI/UKARABATI WA MIUNDO MBINU YA MIFUGO
Wilaya ya Biharamulo inayo miundo mbinu mbali mbali iliyowekwa kusaidia maendeleo ya mifugo. Yapo majosho 5 kati ya hayo majosho 3 yamekarabatiwa. Aidha Lambo la Nyabusozi limejengwa na kuwezesha upatikanaji wa maji kwa kipindi chote cha kiangazi.
HALI YA MASOKO YA MIFUGO NA MAZAO YAKE
Wilaya ya Biharamulo inao mnada mmoja wa mifugo Lusahunga. Mnada huu hauna miundo mbinu muhimu inayohitajika. Katika kipindi cha mwaka 2006/2007, zaidi ya ng'ombe 18,549 wenye zaidi ya Tsh 3,655,698,750 wameuzwa kupitia mnada huu. Nyama, maziwa na mayai ya kuku yamekuwa yakiuzwa moja kwa moja kwa walaji wa ndani ya Wilaya bila kusindikwa kwa kiwango cha wastani wa Tshs 1,500/= kwa kilo ya nyama, Tshs 200/= Lita ya maziwa na Tshs 200/= kwa yai moja.
|