JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BIHARAMULO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
: SEKTA YA USHIRIKA

MAENDELEO YA VYAMA VYA USHIRIKA VYA AKIBA NA MIKOPO (SACCOS) NA MPANGO WA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI NA KUONGEZA AJIRA

Wilaya ya Biharamulo kabla ya mchakato wa kuwawezesha Wananchi kiuchumi na kuongeza ajira hapo Desemba, 2005 ilikuwa na Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) 10 zenye jumla ya Wanachama 465 wakiwemo wanaume 378 na wanawake 87.

Hadi kufikia Mwezi Novemba 2007 Wilaya inazo SACCOS 13 zenye wanachama 2,507 wakiwemo wanaume 1,654 na wanawake 853 . Vikundi vidogo vidogo vya uzalishaji mali vilivyojiunga na SACCOS hizo ni 81 .

 

 

HALI HALISI YA MAENDELEO YA SACCOS WILAYANI

  • Hisa zilizokwisha kusanywa katika SACCOS ni Tshs. 29,871,500/=

  • Akiba zilizokwisha kusanywa katika SCCOS ni Tshs. 715,477,167/=

  • Amana zilizokwisha kusanywa katika SCCOS ni Tshs. 328,259,315/=

  • Jumla ya Mtaji ni Tshs. 1,073,607,982/=

  • Mikopo iliyokopeshwa Wanachama Tshs. 2,840,667,000/=

  • Mikopo iliyorejeshwa benki Tshs. 1,604,494,416/70

  • Mikopo bado kurejeshwa Tshs. 1,236,172,583/30

NB: Mikopo ambayo bado haijarejeshwa ipo katika mzunguko wa kukopwa na muda wake wa kurejesha bado.

 

 

VIKUNDI AMBAVYO VIPO KATIKA HATUA YA KUPATA USAJILI

•  Biharamulo Teachers SACAS

•  Sima SACAS

•  Vijana SACAS

•  Muungano Nyarubungo SACAS

 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI NA KUONGEZA AJIRA KWA KUTOA MIKOPO YENYE MASHARTI NAFUU

 

Mpango wa uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi (NEEP) ni mpango mpya Nchini Tanzania unaolenga katika kuwawezesha Wananchi kushiriki katika shughuli za Kiuchumi katika Sekta mbalimbali kama ilivyoainishwa kwenye sera ya Taifa ya kukuza Uchumi na Kuondoa umasikini (MKUKUTA). Msisitizo wa Mpango umewekwa kwenye maeneo ya uzalishaji na fursa za kuongeza ajira kama vile Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Viwanda vidogo na Biashara, kwa kulenga Wajasiliamali wadogo na wa kati mijini na vijijini. Wajasiliamali wanaolengwa ni Wananchi wenye kipato kidogo wanaofanya jitihada za kuendeleza shughuli halali za kujiongezea kipato lakini hawana mitaji wala dhamana za kuwawezesha kukopa katika mabenki kwa taratibu za kawaida.

Utekelezaji wa mpango huu ulianza kwa baadhi ya maafisa kutoka Halmashauri zote Nchini kupatiwa mafunzo maalumu juu ya Mpango kwa ajili ya kusaidia wananchi katika maeneo yao

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI

WILAYANI BIHARAMULO 

Halmashauri ilianza kwa kutoa semina ya uelewa kwa Viongozi na Maafisa Watendaji wa Kata zote 8 na Vijiji vyote juu ya Mpango huo kwa njia ya kutoa mikopo kwa wajasiriamali. Semina za uelewa juu ya uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi na kuongeza ajira kwa Wajumbe wa Kamati za Maendeleo za Kata (WDC), Viongozi wa SACCOS/SACAS na Wawakilishi wa Vikundi vya uzalishaji mali zilifanyika mwezi Februari, 2007. Hadi kufikia 31 Machi, 2007 maombi 390 ya Wajasiriamali yenye thamani ya Tshs. 600,000,000/= yaliwasilishwa Benki – NMB Ltd Tawi la Biharamulo. Mikopo iliyotolewa katika kipindi hicho ni ya maombi 22 yenye thamani ya Tshs. 28,277,000/=

Aidha mnamo mwezi Mei, 2007 Mamlaka ya Benki – NMB ilisitisha utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali mpaka hapo itakapotangazwa tena.

KIKWAZO KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO HUU.

Taarifa/Takwimu za utoaji Mikopo chini ya mpango huu hazipatikani kwa urahisi kutoka kwa watoa mikopo (Taasisi), na Benki ya NMB imetoa taarifa kuishia tarehe 31March 2007 tu.

Uelewa wa Wananchi juu ya Maandiko ya Miradi ya kuombea Mikopo na uendeshaji wa shughuli za ujasiriamali bado ni duni.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA KUTATUA KIKWAZO HIKI

Mawasiliano yamefanywa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi- Wizara ya Mipango Uchumi na uwezeshaji, kufahamishwa juu ya tatizo hilo na kuomba utatuzi wa suala hilo .

Halmashauri imeweka mkakati wa makusudi kuendesha mafunzo /Elimu zaidi jinsi ya kuandika maandiko ya Miradi ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa shughuli zote za ujasiriamali.

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa KAGERA, BUKOBA, TEL: 028 - 2222341/18, FAX: 028-222356