JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BIHARAMULO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 
 
 

MAJI

Lengo kuu la sekta hii ni kuendeleza na kuimarisha mazingira ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya hii kwa kutumia teknolojia sahihi na rahisi inayokubalika na yenye gharama nafuu kiuendeshaji.

Hadi sasa asilimia ya wakazi wa wilaya wanaopata maji safi ni 38.0

Ili kufikia azma hii, Wilaya ilijiwekea mikakati ifuatayo ili kufikia lengo la kuwapatia wananchi wake maji safi na salama kwa umbali ulio karibu: (Ndani ya mita 400)

•  Kuendeleza uchimbaji wa visima vifupi vya maji na kuimarisha vyanzo vya asili na utunzaji wake.

•  Kuendeleza teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua

•  Kujenga na kuendeleza miradi ya maji ya bubujiko.

•  Kushirikisha wananchi kikamilifu katika kuhudumia miradi ya maji na matumizi ya maji hayo – (kuwashirikisha tangu hatua ya kupanga hadi uendeshaji).

•  Kuimarisha vikundi vya watumiaji maji (WUGs).

Kutokana na vyanzo mbalimbali vya maji vilivyopo wilayani, jumla ya wakazi 80,228 ambao ni asilimia 38 ya wakazi wote wilayani wanapata maji kutokana na vyanzo kama inavyoonyeshwa katika jedwali hapo chini.Pia Inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2010 idadi ya Wakazi 106,956 sawa na asilimia 54 ya wakazi wote Wilayani watapata maji safi na salama.

Upatikanaji wa maji katika mji wa Biharamulo

Mji wa Biharamulo una idadi ya wakazi 15,000. Kati ya hao Wakazi 10,000 wanapata maji ambayo ni sawa na asilimia 67. Upatikanaji wa maji katika Mji wa Biharamulo ni kwa njia zifuatazo, Maji ya bomba (ya kusumwa na mashine), Mradi wa mububujiko (Gravity), na Vyanzo vya asili vilivyoboreshwa. Inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2010 idadi ya Wakazi 11,250 sawa na asilimia 75 watapata maji safi na salama.

Mikakati iliyowekwa kufikia lengo hili ni pamoja na

  • Kukarabati vyanzo 3 vya maji na mataki 5 ya kuhifadhi maji.

  • Kufunga bomba mita 18,000 maeneo mapya ya Mji

  • Kununua mitambo 5 ya kusukumia Maji

  • Kujenga matenki 4 yenye ujazo wa m3 6000

  • Kukarabati mabomba ya kusambazia maji yenye urefu wa mita 20,0000

  • Kuhamasisha Wananchi umuhimu wa kutunza miundo mbinu ya maji na uhifadhi wa maji


 

 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

Hali ya Upatikanaji Maji Wilayani Biharamulo

 

Na

 

Aina ya chanzo

Idadi ya vyanzo

Watu wanao

hudumiwa

 

%

1.

Miradi ya Bubujiko

6

10,200

13

2.

Visima vifupi

109

32,700

41

3.

Visima Virefu

10

6,000

7

4.

Vyanzo vya Asili

19

5,700

7

5.

Matanki ya kuvuna maji ya mvua

61

15,250

19

6.

Miradi ya maji ya nguvu ya Pampu/Solar

2

10,200

13

Jumla

 

80,228

100

  Matatizo yanayokabili huduma ya maji na mikakati ya utatuzi

Matatizo

Utatuzi

Uharibifu wa vyanzo vya maji unaotokana na ukataji miti, uotaji wa miti inayotumia maji mengi katika ukuaji, ufugaji usipangiliwa, ujenzi wa makazi kwenye vyanzo vya maji.

•  Kuelimisha jamii zana ya utunzaji wa vyanzo vya maji.

•  Kupeleka mahakamani watu wote wanaoingilia vyanzo vya maji.

•  Halmashauri ya wilaya imeshatunga sheria ndogo ya kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji na imeanza kutumika.

Uhaba wa vyanzo vya maji

 

Kuendeleza jitihada za kuimarisha vyanzo vya maji vya asili

Ongezeko kubwa la watu lisiloendana na matumizi endelevu ya raslimali zilizopo

Kuhusisha sekta binafsi katika uendeshaji wa miradi ya maji

Gharama kubwa ya uendeshaji na ukarabati wa miundo mbinu ya maji.

•  Kuendeleza miradi ya maji yenye kutumia teknolojia rahisi na yenye gharama nafuu kiuendeshaji.

•  Kuanzisha na kuendeleza utaratibu wa kulipia maji kwa watumiaji.

 

Kutotumia njia endelevu za uendeshaji wa miradi ya maji

Kuhusisha sekta binafsi katika uendeshaji wa miradi ya maji

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera,BUKOBA, TEL: 028- 2222341/-18, FAX: 028-2221356