JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
BIHARAMULO
 
 
     
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
 
Halmashauri < [ Nyumbani ] au
 
 

Utawala

 

Wilaya ya Biharamulo imegawanyika katika Tarafa mbili (2) za Nyarubungo na Lusahunga. Pia inazo Kata 8 zenye jumla ya Vijiji 49 vyenye Vitongoji 299.

 

HALI YA WILAYA KWA JUMLA

•  Biharamulo ni mojawapo ya wilaya nane za Mkoa wa Kagera yenye eneo la kilometa za mraba 5,627. Kwa upande wa Kaskazini Wilaya inapakana na Wilaya za Muleba na Karagwe, Kusini inapakana na Wilaya za Kibondo na Bukombe. Kwa upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Ngara na Mashariki inapakana na Wilaya ya Chato. Wilaya ipo kati ya nyuzi 2 0 15' – 3 0 15' Kusini mwa Ikweta na 31 o – 32 o Mashariki mwa “Standard Meridian ”. Pia Wilaya iko kwenye mwinuko wa kati ya mita 1135 – 1650 kutoka usawa wa bahari.

Idadi ya Watu

Kutokana na sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, Wilaya ina idadi ya watu 162,181 kati ya hao 82,716 ni wanawake na 79,465 ni wanaume. Kutokana na wastani wa ongezeko la 4.8% la mwaka,kwa mwaka 2007 Wilaya inakadiriwa kuwa na watu 198,066. Pia Wilaya ina idadi ya kaya 27,066 zenye wastani wa watu 6 kwa kila kaya. Kutokana na takwimu hizo, Wilaya ina watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapatao 76,712 ambao ni sawa na asilimia 47.3 ya wakazi wote wa Wilaya hii.

 

 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
     
     
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa KAGERA, BUKOBA, TEL: 028 - 2222341/18, FAX: 028-2221356