JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
 
 
     
MIFUGO
 
[ Kilimo ] [ Nyumbani ] au
 

Mkoa wa Kagera unatekeleza Dira ya Sekta ya Mifugo kwa kuikuza na kuifanya ilingane na viwango vya kimataifa ambavyo ni endelevu kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Dira ya Taifa ya Sekta ya Mifugo inasema kuwa “IFIKAPO MWAKA 2025, KUWE NA SEKTA YA MIFUGO AMBAYO NI SHIRIKISHI NA INAYOZINGATIA UFUGAJI WA KISASA, ENDELEVU, INAYOENDESHWA KIBIASHARA, YENYE MIFUGO BORA NA YENYE TIJA KUBWA, ITAKAYOINUA MAISHA YA MTANZANIA NA KUTOA AJIRA, KUZALISHA MALIGHAFI KWA AJILI YA USINDIKAJI, KUONGEZA PATO LA TAIFA NA KUHIFADHI MAZINGIRA”.

Pia mkoa unatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala ya mwaka 2010 inayosema “KATIKA KIPINDI CHA ILANI 2010-2015 MKAZO UTAELEKEZWA KATIKA MATUMIZI YA MAARIFA KATIKA SEKTA YA MIFUGO. JUKUMU KUU LA MSINGI KATIKA UFUGAJI LITAKUWA NI KULETA MABADILIKO YATAKAYOIONDOA SEKTA HII KUTOA UDUNI WA UFUGAJI NA KUWABADILI WAFUGAJI WETU KUTOKA WAFUGAJI WAHAMAJI. MKAZO UTAELEKEZWA KATIKA KUTATUA MATATIZO YA MALISHO NA MAJI NA KUWAFIKISHA WAFUGAJI KATIKA UKULIMA MCHANGANYIKO NA UFUGAJI WA MABANDANI WENYE TIJA KUBWA, UTAKAOTOA NYAMA NA MAZIWA BORA.” pamoja na Azimio la KILIMO KWANZA .

Mkoa wa Kagera una uhakika wa kutekeleza Dira ya Sekta ya Mifugo, Ilani ya Uchaguzi na Azimio la KILIMO KWANZA kwa sababu ya kuwepo kwa fursa zifuatazo:-

•  Hali ya hewa nzuri kwa ajili ya upatikanaji wa malisho na maji ya mifugo.

•  Eneo zuri la kufuga ambalo halijatumika ipasavyo.

•  Upatikanaji wa mifugo bora kutoka kwa wananchi na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kwa ajili ya uzalishaji na unenepeshaji (fattening).

•  Uzoefu wa uhimilishaji uliopo kwa kutumia mbegu bora na kuongezeka kwa uwezo wa Halmashauri kununua vifaa vya uhimilishaji kupitia miradi inayotekelezwa kupitia Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya.

•  Soko la uhakika la mifugo na mazao yake katika nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda na hata D. R. Congo.

 

 
Hali ya Ufugaji

Sekta ya mifugo kwa mkoa wa Kagera huchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya mkoa huu. Asilimia kubwa ya wafugaji ni wale wafugaji wadogo wadogo, ambao hutegemea mifugo kwa ajili ya samadi kwenye kilimo; lishe bora kutokana na maziwa na nyama; chanzo cha mapato; ajira; nishati na shughuli nyingine za kijamii.

Mifugo na mazao ya mifugo yanayozalishwa huokoa fedha za kigeni ambazo Taifa lingetumia kuagiza vitu hivyo kutoka nje ya nchi. Uuzaji wa mifugo na mazao yake nchi za nje hulipatia Taifa fedha za kigeni.

Idadi ya Mifugo

Kaya zipatazo 1,600 au Wafugaji wapatao 113,000 hufuga ng'ombe wa asili mkoani Kagera. Kaya hizi za wafugaji 1,600 ni wale wenye makundi makubwa ya ng'ombe, sawa na asilimia 67 ya idadi yote ya ng'ombe katika mkoa. Wafugaji waliobakia ambao ndio wengi ni wafugaji wadogo wadogo.

Kwa hivi sasa mkoa unakadiriwa kuwa na ng'ombe wapatao 537,511 wanaofugwa ambapo ng'ombe wa asili ni 517,292 na ng'ombe wa maziwa ni 20,115. Mbuzi wafugwao ni 642,969 ambapo mbuzi wa asili ni 633,037 na mbuzi wa maziwa ni 9,932. Wanyama wengine ni kondoo 67,660, nguruwe; 11,243 na wanyama kazi kama vile punda 236 na farasi 18. Wengine ni bata; 64,087; Sungura; 13,201 na mbwa; 31,304.

AINA YA MIFUGO

H A L M A S H A U R I

Bukoba Vijijini

Manispaa ya Bukoba

Missenyi

Karagwe

Biharamulo

Chato

Ngara

Muleba

Jumla

Ng'ombe wa asili

30,279

851

77,954

138,671

59,000

72,569

55,057

82,911

517,292

Ng'ombe wa maziwa

2,769

2,497

1,434

5,575

469

33

2,874

4,464

20,115

Jumla Ng'ombe

33,048

3,348

79,488

144,246

59,469

72,604

57,933

87,375

537,511

Mbuzi wa Asili

66,626

1,802

58,022

133,407

32,882

62,757

182,587

94,954

633,037

Mbuzi wa Maziwa

1,500

600

790

948

276

200

169

5,449

9,932

Jumla Mbuzi

68,126

2,402

58,812

134,355

33,158

62,957

182,756

100,403

642,969

Kondoo

5,686

1,128

4,988

13,200

8,220

9,034

12,355

13,049

67,660

Nguruwe

1,277

243

1,366

1,256

420

278

2,170

4,233

11,243

Kuku wa Asili

244,300

1,268

155,431

73,484

26,237

84,607

153,575

93,103

832,005

Kuku wa Mayai

736

11,590

0

693

775

0

1,450

3,047

18,291

Kuku wa Nyama

4,564

4,844

0

0

0

0

0

0

9,408

Jumla Kuku

249,600

17,702

149,037

74,177

27,012

84,522

155,025

96,150

853,225

Bata

13,549

1,112

1,300

4,533

6,559

23,012

3,115

10,907

64,087

Sungura

5,659

272

2,000

2,027

180

43

1,520

1,500

13,201

Mbwa

4,795

652

1,000

9,717

4,500

2,574

5,502

2,564

31,304

Punda

0

0

0

36

78

87

13

22

236

Farasi

0

0

0

18

0

0

0

0

18

Paka

0

121

0

934

160

110

600

0

1,925

Njiwa

0

0

0

0

280

0

56

0

336

Kanga

0

0

0

0

206

42

28

0

276

Watumishi wa Umma wa Sekta ya Mifugo Mkoani Kagera

Bado kuna upungufu wa wataalamu wa Sekta ya Mifugo kuhudumia mifugo iliyopo. Kwa hivi sasa wanahitajika wataalam wa mifugo wengine 53. Mkoa unashukuru kupata Madaktari wapya wa Mifugo katika Halmashauri za wilaya za Missenyi na Ngara (DVOs). Kati ya Halmashauri zote ni Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba tu ambayo bado haijapata Daktari wa Mifugo wa Manispaa (MVO).Tunaipongeza sana Wizara kwa hilo.

Miundombinu ya Mifugo Iliyopo Mkoani Kagera

Majosho:

Jumla ya majosho 64 kati ya 141 sawa na asilimia 45% ya majosho yaliyopo mkoani Kagera yanafanya kazi. Hali ya uogeshaji mifugo imeendelea kuimarika na hivyo kupunguza magonjwa yanayoenezwa na kupe. Miradi inayotekelezwa chini ya Mipango ya Maendeleo ya Kilimo ya Wilaya (District Agricultural Development Plans –DADPs) na kuwepo kwa dawa za ruzuku ya serikali kunasaidia sana juhudi za mkoa katika kuimarisha huduma za majosho

Malambo

Mahitaji ya malambo katika mkoa ni 81 na jumla ya malambo 15 yanafanya kazi. Malambo yaliyopo yanatosheleza kuhudumia jumla ya ng'ombe 36,416

Machinjio

Mkoa unazo machinjio ndogo 55 na machinjio kubwa moja katika Manispaa ya Bukoba. (Jedwali Na. 5). Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kujenga machinjio kubwa ya Kisasa katika mji wa Kyaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. Mkoa unapendekeza kuwa ujenzi wa machinjio hiyo uende sambamba na ujenzi wa kiwanda cha kusindika ngozi pamoja na kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi

Minada ya Mifugo

Jumla ya minada 11 inafanya kazi kati ya minada 14 iliyopo.

 

Magonjwa ya Mifugo

Kuimarika kwa huduma za majosho na upatikanaji wa dawa ya ruzuku ya serikali ya kuogesha mifugo, kumesaidia idadi kubwa ya mifugo kuogeshwa na hivyo kupunguza magonjwa yanayoenezwa na kupe ingawaje bado magonjwa yanaendelea kujitokeza. Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2010 Ugonjwa wa Miguu na Midomo (Foot and Mouith Disease -FMD) umejitokeza katika Halmashauri za wilaya za Karagwe, Muleba, Chato na Bukoba. Hii kwa kiwango kikubwa imesababishwa na muingiliano wa mifugo unaosababishwa na mifugo kuingia kutoka nchi jirani bila kufuata taratibu na sheria.

Chanjo ya Kuzuia Magonjwa ya Mifugo

Mkoa umeendelea kutoa chanjo za mifugo ili kuzuia magonjwa mbali mbali kama vile Ugonjwa wa Miguu na Midomo(FMD); Ugonjwa wa Homa ya Mapafu (CBPP); Ugonjwa wa Kisiki cha Ngozi (LSD), Ugonjwa wa Ndigana Kali (ECF), Ugonjwa wa Chambavu (BQ), Kichaa cha Mbwa, Mdondo wa Kuku na Ugonjwa wa Gumboro. Mkoa wa Kagera unatekeleza Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza Ugonjwa Homa ya Mapafu (Roll Back Plan) ambapo chanjo ya awamu ya Kwanza ilianza tarehe 28 Mei, 2010.

Uhimilishaji wa Mifugo

Uhimilishaji wa ng'ombe wa maziwa na wale wa asili kwa kutumia mirija umeendelea kufanyika kwa wafugaji kupitia Halmashauri, Bodi ya Udhamini ya Mkoa (KAGERA DAIRY DEVELOPMENT TRUST- KADADET), na Watu binafsi kwa kutumia mbegu bora za mifugo.

Mafunzo kwa Wafugaji

Mwaka 2001 serikali ya Uholanzi ilikabidhi Chuo cha Wafugaji cha Kikulula, Karagwe kwa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo kwa wakati huo. Wataalam kupitia KADADET wameendelea kutoa mafunzo ya mifugo kwa kutumia michango ya wafugaji na Halmashauri za wilaya . Tunashukuru Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Halmashauri ya wilaya ya Karagwe kwa kuendelea kuchangia katika ukarabati wa Chuo hicho. Ili kutoa elimu bora kwa wakulima na pia mpango wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ya kutaka kukipandisha hadhi chuo hicho na hatimaye mwaka ujao wa fedha 2011/2012, chuo hicho kuanza kutoa mafunzo ya wataalamu katika ngazi ya Cheti na Astashahada, ili kujikimu na uhaba wataalamu wa mifugo tulionao nchini.

Uogeshaji wa Mifugo

Mifugo imeendelea kuogeshwa kwenye majosho ili kuua makupe na mbung'o kwa ajili ya kuzuia magonjwa. Baadhi ya wananchi huogesha mifugo yao kwa kutumia pampu za mikono pamoja na kutumia dawa za kupaka mgongoni. Idadi ya mifugo inayoogeshwa inaendelea kuongezeka kutokana na upatikanaji wa dawa za ruzuku ya Serikali, ujenzi na ukarabati wa majosho. Mkoa ulipokea lita 2,048.73 mwezi Juni 2010 na nyongeza ya lita 2,500 jumla lita 4,548.73 za dawa ya ruzuku ya kuogesha mifugo aina ya Paranex Ò (Alphacypermethrin) zenye thamani ya Tsh. 181,949,200. Mahitaji halisi ya dawa yalikuwa ni lita 9,050 ya dawa aina ya Paranex (Alphacypermethrin), lita 1,000 za Ecotix® (Cypermethrin), lita 360 za Cybadip® (Cypermethrin) na Lita 1,000 za dawa ya zamani ya Ruzuku ya Bayticol® (Flumethrin) sawa na jumla ya lita 11,410 . Ili wafugaji wa ng'ombe wa maziwa wanaotii masharti ya kufugia ndani (zero grazing) waweze pia kunufaika na dawa ya ruzuku tunaomba wigo wa aina za dawa zinazotolewa upanuliwe ili dawa za kupaka mgongoni (pour on preparation) ziweze kupatikana kwa bei nafuu. Mchanganuo wa kiasi cha dawa ya ruzuku iliyosambazwa katika Halmashauri umeambatishwa na taarifa hii (Jedwali Na. II)

Changamoto:

  1. Mkoa unahitaji gari maalum kwa ajili ya kukabiliana na maafa yanayotokana na magonjwa ya milipuko. Usafiri huu unaweza kupatikana kupitia Mpango wa kuzuia Kichaa cha Mbwa chini ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi au Mkakati wa Kujikinga na Mafua Makali ya Ndege kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi za Rwanda na Burundi .
  2. Mkoa bado una nia ya kujifunza maendeleo ya usindikaji wa ngozi na utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na ngozi nchini Ethiopia hususan katika jiji la Addis Ababa endapo fedha ya kugharamia safari hiyo ya mafunzo itapatikana.
  3. Zipo jitihada za kutosha za kuajiri wataalam wa mifugo katika Halmashuri ingwaje bado wataalam wengine wapatao 53 wanahitajika.
  4. Mifugo imeendelea kuingia kutoka nchi jirani bila kufuata taratibu na sheria na kusababisha kuingia na kusambaa kwa magonjwa ya milipuko.
  5. Kuna upungufu wa Vituo 6 vya Ukaguzi wa Mifugo vya mpakani (Veterinary Check Points).
  6. Bado mgongano wa kimawazo kati ya wananchi na Wawekezaji wa huria za Kampuni ya ranchi za Taifa (NARCO) haujaisha.
  7. Uibuaji wa miradi ya Mifugo kwenye fedha za Maendeleo (ASDP) kutoka kwa wananchi bado ni mdogo na uchangiaji ni mkubwa kwa miradi inayogharimu fedha nyingi.
  8. Hakuna uwekezaji wa kutosha katika Sekta ya mifugo ikiwa ni pamoja na usindikaji wa mazao ya mifugo kama vile ngozi na maziwa.
  9. Kuna uhaba wa majokofu kwa ajili ya kuhifadhi dawa za chanjo zinazopokelewa mkoani kabla hazijasambazwa katika Halmashauri.

Mikakati ya Mkoa Katika Sekta ya Mifugo

Mkoa wa Kagera umejiwekea mikakati ifuatayo katika kuendeleza Sekta ya mifugo ili kuwawezesha wananchi kujiongezea kipato na kupambana na umasikini:-

•  Kuufanya Mkoa wa Kagera kuwa huru kwa Magonjwa muhimu (Disease Free Zone) ili kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na nchi jirani za Uganda , Rwanda , na Burundi kuweka mpango shirikishi katika kutokomeza magonjwa muhimu ya mifugo.

•  Kujenga vituo 6 vya Ukaguzi wa Mifugo vya mpakani (Veterinary Check Points) kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya husika pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

•  Kupata majokofu 3 (majokofu ya ubaridi wa kawaida 2 na jokofu la kugandisha 1) kwa ajili ya kuhifadhi dawa za chanjo mkoani kabla ya kuzisambaza katika Halmashauri.

•  Wafugaji kuhimizwa kutumia madume bora na mbegu bora kwa ng'ombe wao wa kienyeji ili kuzalisha mitamba chotara kwa ajili ya maziwa na nyama.

•  Kupunguza vifo vya ndama wa ng'ombe wa asili vinavyotokana na magonjwa ya kupe toka asilimia 35 mpaka asilimia 5 na vile vya ng'ombe wa maziwa toka asilimia 8 mpaka 2 na kuwahamasisha wafugaji kuogesha mifugo yao na kufuata kanuni bora za ufugaji.

•  Kufanya ziara ya mafunzo kwa lengo la kujifunza mafanikio ya nchi ya Ethiopia hususan jiji la Addis Ababa katika kusindika na kutengeneza bidhaa za ngozi kwa lengo la kuongeza tija.

•  Kuendelea kutenga maeneo ya ufugaji na kuhimiza wafugaji kuyaendeleza maeneo yao na kuweka programu za unenepeshaji wa mifugo.

•  Kuendelea kuelimisha Wafugaji umuhimu wa kutumia mbinu za ufugaji bora na kuvuna mifugo yao kwa wakati ili kubadili tabia yao ya kichungaji na kuwa wafugaji kupitia vituo vya kuwaendeleza wafugaji (Farmers Extension Centres) na Chuo cha Wafugaji cha Kikulula kwa kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wafugaji.

•  Mifuko ya LDF (Livestock Development Fund) kuanzishwa katika Wilaya zote na kuitunisha kama ilivyo agizo la Serikali ili iweze kusaidia kuleta maendeleo ya mifugo Wilayani.

Namna ya kukabiliana na changamoto

Mkoa unachukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika Sekta ya Mifugo ingawaje nguvu za ziada zinahitajika kutoka Serikali Kuu kukabiliana na changamoto hizo, kama vile kuwaondoa wahamiaji haramu na mifugo yao ambao mara nyingi ni tishio kwa uingizaji wa Magonjwa ya Mifugo, kusababisha migongano isiyokwisha kati ya wananchi na wahamiaji haramu, wizi, ujambazi pamoja na nchi jirani kufaidika zaidi na rasilimali ndogo tuliyonayo.

Mkoa umeendesha zoezi la kuwaondoa mifugo haramu katika mapori ya Burigi na Biharamulo. Pia mkoa unaendelea kuweka mpango murua wa kuheshimiana kati ya vijiji vilivyomo ndani ya Huria za Taifa katika kusuluhisha mgogoro wa ardhi uliopo kati ya Wawekezaji, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) na Wanavijiji.

Ili kudhibiti wimbi la mifugo inayoingizwa kiholela mkoani Kagera ni muhimu kuendelea kuboresha mazingira ya wakaguzi waliopo katika vituo vya mipakani na kupeleka wengine kwenye vituo ambavyo havina wataalam.

 

 
 
 

 

 

 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 

 

 

•   

 

 

 

 
 

 

     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 027-2752184