
Eng. Avitus Exavery-Mhandisi wa maji Sekretarieti ya Mkoa
MAFANIKIO
Upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa mkoa wa Kagera waishio vijijini umefikia wastani wa asilimia 55.3. na Manispaa ya Bukoba asilimia 76.5. Jitihada hizi zimepatikana kutokana na fedha za serikali, wahisani na michango ya wananchi.
• Kuanzisha Kamati za Maji za Vijiji hadi kufikia 483 (asilimia 64.6) kati ya vijiji 748. Idadi ya mifuko ya maji imefikia 395 yenye jumla ya Tshs, 83,351,165.
• Kuunda sheria ndogo ndogo za Halmashauri ili kulinda uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira.
• Kusajiri vyombo huru vya watumiaji maji (COWSOs).
• Kuanzisha Bodi za maji za miji mikuu ya wilaya katika miji ya Biharamulo, Ngara, Muleba na Karagwe. CHANGAMOTO:
Uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira hususan uchomaji moto bado ni mkubwa. • Uharibifu wa Miradi mingi mikubwa ya bomba inayoendeshwa na mitambo kutokana na jamii kushindwa kupata fedha za uendeshaji na matengenezo.
• Ukosefu wa ulipiaji wa maji mijini ambalo ni tatizo kubwa kwa baadhi ya Taasisi kwa wakati mwafaka
Ukosefu wa vipuri vya kufanyia marekebisho ya miradi ya maji kwa wakati mwafaka. MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO:
• Matumizi ya sheria ndogo ndogo za hifadhi ya vyanzo vya maji yametiliwa mkazo Aidha upandaji wa miti rafiki wa maji na kukata miti ambayo hufyonza maji mengi kama Mikalitusi na kusababisha vyanzo vya maji kukauka unaendelea.
• Uhamasishaji wa Kamati za Maji na vikundi vya watumiaji maji ikiwa ni pamoja na kutunisha mifuko ya maji kwa shughuli hizo unafanyika.
• Mamlaka za maji kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa na Wilaya hali hii imeanza kubadilika kwa baadhi ya Taasisi kwa kulipia malimbikizo ya madeni yao .
• Tunahimiza ujenzi wa miradi yenye Technologia nyepesi kama uvunaji wa maji ya mvua, uchakavu wa miundo mbinu mijini unaosababisha upotevu wa maji mengi na kusababisha gharama kubwa za uendeshaji na matengenezo. Jitihada zinafanywa kulekebisha miundo mbinu kwa fedha za Serikali na Wahisani.
• Serikali inatekeleza Programu ya maji ambapo utekelezaji wake kwa upande wa vijijini umefikia hatua ya kujenga miundombinu ya maji kwenye vijiji kumi vya awali kwa kila hHalmashauri ya Wilaya.
Na kwa upande wa mjini Mhandisi Mshauri atakayefanya utafiti na kusanifu miradi ya maji kwenye miji mikuu ya Wilaya za Mkoa wa Kagera yuko kwenye hatua za mwisho za kupatikana kwake.
|