Pamoja na utekelezaji mzuri wa programu ya Hifadhi ya mazingira kama inavyoonekana katika Taarifa,bado kuna mapungufu yaliyojitokeza kama changamoto katika kufikia malengo ya programu.
(i)Wachimbaji wadogo wadogo bado wanaendelea kuharibu kuharibu mazingira kwa uchimbaji holela wa madini katika vyanzo vya maji ndani ya pori la matabe.
(ii)Uchafuzi wamazingira unatokana na taka ngumu pamoja na plastiki bado unaendelea pamoja na jitihada kubwa iliyofanywa na wakuu wa wilaya kupitia miongozo iliyotolewa na ofisi ya makamu wa Rais kitengo cha mazingira .
(iii)Baadhi ya wilaya hazina jaa maalumu la utupaji taka(dampo)na hivyo kusababisha utupaji ovyo wa taka.Hali hii ni chanzo chanzo cha kupata magonjwa ya mlipuko.
(iv)Hali ya mazingira katika Bandari ya Kemondo na Bukoba Port siyo ya kuridhisha.Pamoja Ufuatiliaji uliofanywa na Halmashauri husika hamna shughuli yoyote ya utunzaji wa mazingira imefanyika hadi sasa.
(v)Shughuli za kilimo bado zinafanyika kwenye miteremko ya milima ,mabondeni na kwenye vyanzo vya maji hasa katika wilaya za Biharamulo ,Muleba,Ngara na Karagwe.
(vi)pamoja na kwamba takwimu zinaonyesha kupungua kwa tatizo la uchomaji moto,bado hali si ya kujipongeza sana. |