JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
 
 
     
SHULE ZA MSINGI,SEKONDARI NA VYUO
 
Mada .. [ Nyumbani ] au
 
ELIMU YA MSINGI
 

WANAFUNZI NA WALIMU

Mkoa una jumla ya Shule za Msingi 1007 zenye jumla ya mikondo 13,196. Kati ya hizo shule 984 ni za Serikali na 23 ni za Binafsi. Jumla ya wanafunzi waliopo katika shule zote za msingi ni 499,581 wakiwemo wavulana 250,230 na wasichana 249,349 kama jedwali linavyoonyesha.

Idadi ya Shule za Msingi na Wanafunzi

 

WILAYA

IDADI YA SHULE

WANAFUNZI

SERIKALI

SERIKALI

BINAFSI

JUMLA

WAS

WAV

Biharamulo

74

-

74

20,011

20,680

40,691

Chato

126

-

126

34,924

36,887

71,811

Bukoba (V)

134

1

135

31,611

31,536

63,147

Missenyi

95

3

98

18,746

19,113

37,859

Bukoba (M)

23

6

29

9,229

9,045

18,274

Karagwe

204

8

212

53,545

51,928

105,475

Muleba

221

3

224

47,866

47,762

95,628

Ngara

107

2

109

33,417

33,279

66,696

Jumla

984

23

1007

249,349

250,230

499,581

Idadi hiyo inahitaji walimu 12,487 ili kufikia uwiano wa mwalimu na mwanafunzi 1:40 uliowekwa na wizara. Jumla ya walimu waliopo ni 8,518 tu sawa na uwiano wa 1 :58 . Kuna upungufu wa walimu 3,969 sawa na asilimia 31.7.

 

 
 
 

ELIMU YA UFUNDI

Mkoa una jumla ya vyuo vya Ufundi 31. kati ya hivyo vyuo vya Serikali ni 5 na 26 ni vya Taasisi au watu binafsi. Jumla ya wanachuo katika vyuo hivi ni 675 wakiwemo wanawake 315 na wanaume 360.

Fani zinazofundishwa katika vyuo hivi ni pamoja na Useremala, Uashi, Sayansi Kimu, TEHAMA, Ushonaji na Uhunzi. Jedwali lifuatalo linaonyesha mgawanyo wa vyuo hivi kiwilaya.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikana na wizara nyingine imeunda kamati ya kukarabati na kuanzisha vyuo vya Ufundi katika halmashauri zisizo na vyuo hivi.

Idadi ya Vyuo Vya Ufundi

 

 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
ELIMU YA SEKONDARI
 

SHULE ZA SEKONDARI

Mwaka 2007 mkoa ulifanikiwa kufungua shule mpya za Sekondari 71. Ongezeko hili ni sawa na asilimia 78.02 ya shule 91 zilizokuw a na usajili hadi kufikia mwaka 2006.

•  Jumla ya shule za serikali zilizosajiliwa hadi sasa ni 186. Kati ya hizo 162 ni za Serikali na 24 za Mashirika au Binafsi.

•  Mkoa pia unazo shule za ‘A' Level zipatazo 11 zikiwemo 6 za serikali na 5 za watu au taasisi binafsi.

•  Lengo la mkoa ni kuongeza shule za aina hiyo kwa kujenga shule mpya au kupanua shule zilizopo ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari.

Idadi ya Shule za Sekondari zilizopo na zinazojengwa

Na.

Wilaya

Idadi Ya Shule Za Zamani

Idadii Ya Shule Mpya

Shule Zinazojengwa

 

 

Jumla

1.

Biharamulo

4

6

6

16

2.

Bukoba (M)

6

7

3

16

3.

Bukoba (V)

18

7

5

30

4.

Chato

9

8

5

22

5.

Karagwe

17

17

8

42

6.

Missenyi

9

9

2

20

7.

Muleba

19

8

6

33

8.

Ngara

9

9

5

23

JUMLA

91

71

40

202

 

 
 

WALIMU

Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa ambayo walimu wengi wanaopangiwa hawaripoti. Mwaka 2007 mkoa ulipangiwa jumla ya walimu wa sekondari 296. Kati ya hao walimu 120 walikuwa wa stashahada, walimu 156 wa kozi ya muda mfupi na walimu 20 wa soko la ajira.

  • Walimu 250 tu sawa na asilimia 84 ndio walioripoti. Mkoa unapambana na tatizo hili kwa kuzishauri halmashauri kujenga au kutafuta nyumba za kuishi walimu ili kuwavutia walimu wapya wanaoripoti katika vituo vya kazi.
  • Mahitaji ya mkoa kwa walimu wa shule za sekondari kwa sasa ni walimu 2,362 lakini mkoa unahitaji walimu 4,320 kwa shule 162 zitakapokamilika kuwa na mikondo minne kuanzia kidato cha Kwanza hadi cha Nne.
  • Kwa sasa mkoa una walimu 1,194 tu sawa na asilimia 27.6 tu.

Mkoa unakabiliana na matatizo ya walimu kwa :-

•  kuwashauri wakuu wa shule kuwatumia wanafunzi waliomaliza kidato cha sita wanaoishi kwenye maeneo hayo

•  Kuwatumia walimu wastaafu pamoja na walimu kutoka shule za jirani wenye ujuzi wa masomo yasiyo na walimu shuleni hapo

•  Kuwashauri wazazi kupitia mikutano ya kijiji na kata kuchangia gharama za kuwalipa walimu wasio katika mfumo rasmi wa ajira.

Hata hivyo hili ni suluhisho la muda mfupi. Mkoa unaomba serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi uangalie kujengewa Chuo cha Ualimu kitakachokuwa kinatoa mafunzo ya stashahada ili kuwapata walimu ambao watakuwa wanayafahamu mazingira ya mkoa huu na hivyo kukubali kubaki hapa watakapomaliza mafunzo yao .

 

 

 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
Mada [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 028-2752184