UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO NA BAJETI YA MATUMIZI YA KAWAIDA KWA MWAKA WA FEDHA 2010/11
Fedha zilizoidhinishwa na kutolewa:
Katika mwaka 2010/2011 kiasi cha shilingi 3,287,893,000 kiliidhinishwa kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Sekretarieti ya Mkoa. Hadi Juni, 2010 kiasi cha shilingi 1,283,321,218 zilikuwa zimepokelewa sawa na asilimia 39.2 ya fedha zilizoidhinishwa.
Matumizi ya fedha
Hadi Juni, 2011 jumla ya shilingi 1,275,321,218 zilitumika kutekeleza miradi sawa na asilimia 99 ya fedha zilizopokelewa.
KASMA 6532: Miradi ya kijitegemea ofisi ya mkuu wa Mkoa na wakuu wa Wilaya shilingi 55,000,000
LENGO:
Katika mwaka wa fedha 2010/2011 mkoa umeidhinishiwa kutumia shilingi 55,000,000 kuchangia juhudi za wananchi kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
UTEKELEZAJI
Kwa mwaka 2010/2011 mfuko umesaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na nguvu za wananchi ikiwemo ya ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa na maabara katika shule nane (8) za sekondari, pamoja na ujenzi wa mabweni mawili ya sekondari. Aidha, vikundi mbalimbali vya utamaduni, walemavu, kuweka na kukopa, wanawake na kwaya jimbo katoliki Kayanga vimesaidiwa, pamoja na kuchangia mfuko wa elimu wa wilaya Missenyi. Fedha hizo zilitumika kuchangia ukarabati wa jengo la maendeleo jimbo la Karagwe na kusaidia shughuli za michezo katika wilaya za Missenyi na Ngara (DAS CUP – Ngara).
Fedha zilizoidhinishwa |
- |
shilingi |
55,000,000 |
Fedha zilizopokelewa |
- |
shilingi |
55,000,000 |
Fedha zilizotumika |
- |
shilingi |
55,000,000 |
KASMA 6550 : Kusaidia maeneo yaliyoathiriwa na wakimbizi shilingi 233,292,000
LENGO:
Kujenga uwezo wa watumishi na jamii kusimamia maendeleo endelevu na kuboresha mazingira katika maeneo yaliyokaliwa na wakimbizi.
UTEKELEZAJI
Mafunzo yametolewa kwa wataalamu 66 wa sekretarieti ya mkoa na wa halmashauri, juu ya sera na sheria mbalimbali za kulinda mazingira, tathmini ya kimkakati ya mazingira na tathmini ya kimkakati ya athari za mazingira. Aidha, mafunzo yametolewa kwa wataalamu wa sekretarieti ya mkoa na serikali za mitaa kuhusu namna ya kupanga miradi ya maendeleo, ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni pamoja na mafunzo ya jinsi ya kuhusisha masuala ya jinsia kwenye mipango ya maendeleo. Pia tathimini ya mazingira katika wilaya za Ngara na Karagwe imefanyika na kuhudhuriwa na wahe. Madiwani, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na mwenyeviti wa vijiji.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
233,292,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
62,723,400 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
62,700,000 |
KASMA 4404: Programu ya maendeleo ya kilimo wilayani (ASDP) shilingi 86,476,000
LENGO:
Lengo kuu la mradi huu ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za miradi ya kilimo inayotekelezwa katika Halmashauri ili kutoa ushauri sahihi kuhusu maendeleo ya Kilimo.
UTEKELEZAJI
Kwa kipindi cha 2010/2011 ufuatiliaji umefanywa kwa miradi ya kilimo inayotekelezwa katika ngazi ya halmashauri. Ufuatiliaji umefanyika katika halmashauri za Bukoba, Muleba, Karagwe, Missenyi, Chato, Ngara na Biharamulo. Aidha, tathmini ya awali ya miradi ya umwagiliaji imefanyika katika wilaya za Muleba, Chato, Ngara na Biharamulo. Halmashauri zimewezeshwa kuandaa taarifa za kilimo kupitia mafunzo yaliyotolewa kwa robo nne. Vile vile maandalizi ya viwanja vya maonesho ya nane nane ya kanda ya ziwa huko mwanza yamefanyika pamoja na maandalizi ya bajeti ya DADPS kwa mwaka wa fedha 2011/12 yamefanyika na kuwasilishwa OWM – TAMISEMI.
Fedha zilizoidhinishwa |
- |
shilingi |
86,476,000 |
Fedha zilizopokelewa |
- |
shilingi |
80,799,000 |
Fedha zilizotumika |
- |
shilingi |
80,799,000 |
KASMA 4286: Mradi wa ujenzi wa bandari ya Kabango shilingi 1,000,000,000
MALENGO:
Mradi huu kwa mwaka huu utatekelezwa kwa kukamilisha malengo yafuatayo:
Kujenga gati eneo la bandari ambapo meli itatia nanga.
Kuanza ujenzi wa barabara ya lami Km. 1
Kukamilisha Ujenzi wa nyumba nne za watumishi na ofisi za wafanyakazi wa eneo hilo la bandari.
UTEKELEZAJI
Hadi kufikia Juni, 2011 ujenzi wa gati umefikia asilimia 17%, majengo matatu (3) yamekwisha kamilika, kati ya hayo mawili ni ya kuishi familia mbili. Ofisi moja imekamilika pamoja na vifaa vitakavyotumiwa na wahandisi kwenye eneo la mradi.
Fedha iliyoidhinishwa |
- |
shilingi |
1,000,000,000.00 |
Fedha iliyotolewa |
- |
shilingi |
651,526,000.00 |
Fedha iliyotumika |
- |
shilingi |
651,526,000.00 |
Kasma 6389: Ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa awamu ya II shilingi 1,040,000,000 fedha za ndani.
LENGO:
Kuendeleza ujenzi wa miundombinu kwa kujenga jengo jipya la ofisi ya Mkuu wa Mkoa hatua ya pili.
UTEKELEZAJI :
Mradi huu utatekelezwa kwa awamu tatu. Katika awamu ya kwanza eneo la mradi limekwisha sawazishwa na ujenzi wa msingi na nguzo za jengo umekamilika kwa asilimia 40%. Mhandisi mshauri wa mradi ni Archplan International wa Dar es salaam, meneja wa mradi ni wakala wa majengo Tanzania na mkandarasi ni Kampuni ya Elerai Construction Ltd ya Arusha.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
1,040,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
00 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
00 |
Kasma 6331: Ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa wilaya Missenyi na nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya Muleba shilingi 191,852,000 fedha za ndani.
LENGO:
Kuendeleza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya Mkuu wa Wilaya ya Missenyi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba awamu ya pili.
UTEKELEZAJI:
Tathmini ya zabuni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi awamu ya pili imekamilika kwa ajili kumpata mkandarasi na kuanza kazi ya ujenzi awamu ya pili.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
191,852,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
30,000,000 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
30,000,000 |
Kasma 5404: Ukarabati wa Hospitali ya Mkoa (Wodi Daraja A) awamu ya tatu; shilingi 100,000,000.00 fedha za ndani
LENGO:
Kukamilisha ujenzi wa wodi mpya daraja la 'A' katika hospitali ya mkoa awamu ya pili na kununua vitendea kazi na samani.
UTEKELEZAJI:
Ujenzi wa wodi umekamilika na vitendea kazi vimenunuliwa kutoka Bohari ya dawa.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
100,000,000.00 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
100,000,000.00 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
100,000,000.00 |
Kasma 6387: Ukarabati wa nyumba ya kupumzikia viongozi shilingi 30,000,000.00 fedha za ndani.
LENGO:
Kujenga na kukarabati majengo ya kupumzikia viongozi katika wilaya za Muleba na Bukoba ili kuboresha mazingira ya kuishi viongozi wanaotembelea mkoa.
UTEKELEZAJI:
Mchakato wa kuwatafuta wakandarasi kwa ajili ya kujenga na kukarabati majengo ya kupumzikia viongozi umekamilika. Hadi Juni, 2011 hakuna fedha iliyopokelewa kutoka HAZINA.
Fedha iliyoidhinishwa |
– |
shilingi |
30,000,000 |
Fedha iliyopokelewa |
– |
shilingi |
00 |
Fedha iliyotumika |
– |
shilingi |
00 |
KASMA 5493. MRADI WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI (GLOBAL FUND HIV/AIDS Prevention Project). Shilingi 80,000, 000 Fedha za nje.
LENGO :
Kuratibu na kufuatilia shughuli za kudhibiti UKIMWI kwenye halmashauri zote nane (8), kufanya ufuatiliaji kwenye halmashauri zote 8, kufanya vikao na wadau 50 wanaoshughulikia kudhibiti UKIMWI na kufanya mafunzo ya kudhibiti UKIMWI kwa vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI.
UTEKELEZAJI:
Uhamasishaji jamii juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI umefanyika kwa kutumia gari la sinema katika halmashauri za Bukoba mjini, Bukoba vijijini na Missenyi kwa kutumia fedha za matumizi mengineyo.
Fedha iliyoidhinishwa |
– |
shilingi |
80,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
00 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
00 |
Kasma 5495: Kuzuia maambukizi ya UKIMWI; shilingi 30,000,000 fedha za nje.
LENGO:
Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji mpango wa kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika halmashauri za wilaya na manispaa katika kipindi cha 2010/2011.
UTEKELEZAJI:
Ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za kudhibiti UKIMWI pamoja na uhamasishaji wa masuala mbalimbali ya UKIMWI kwa njia ya sinema umefanyika katika vijiji 300 kati ya vijiji 600 katika halmashauri zote umefanyika.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
30,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
15,000,000 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
15,000,000 |
Kasma 3217: Mradi wa Maji Vijijini (kujenga uwezo); Shilingi 35,000,000 fedha za nje.
LENGO:
Kufuatilia na kuzijengea uwezo halmashauri za wilaya katika kutekeleza mradi wa usambazaji maji vijijini na usafi wa mazingira. Kuandaa vikao vya kila robo mwaka vya wahandisi wa maji wa wilaya na mamlaka za maji za wilaya, pia kuandaa taarifa ya utekelezaji kwa kila robo ya mwaka.
UTEKELEZAJI
Maandalizi ya mpango wa kujengea uwezo watumishi wa sekretarieti ya mkoa na serikali za mitaa kwa sekta ya maji yamekamilika. Hadi Juni, 2011 hakuna fedha iliyotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
35,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
00 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
00 |
Kasma 5486: Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Afya shilingi 227,273,000 fedha za nje.
LENGO:
Kutoa ushauri katika halmashauri za wilaya juu ya namna ya utoaji huduma bora kwa jamii, kufanya mikutano na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekretarieti ya mkoa yanayohusu kujikinga na UKIMWI. Pia mkoa umepanga kukagua na kupitia miongozo mbalimbali juu ya uboreshaji huduma za afya.
UTEKELEZAJI:
Vikao vinne vya kila robo mwaka kupitia taarifa za utekelezaji za halmashauri vimefanyika, ziara kwenye halmashauri zimefanyika mara mbili (2) kufuatilia na kutoa ushauri juu ya magonjwa yanayoambukiza. Aidha, vikao vinne (4) vya kupitia taarifa za afya za halmashauri vimefanyika.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
227,273,000.00 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
227,272,818.00 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
227,272,818.00 |
Kasma 6337: Ujenzi wa ofisi za Wakuu wa Wilaya shilingi 50,000,000.00 fedha za ndani.
LENGO:
Kufanya maandalizi ya kujenga ofisi kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya za Muleba na Biharamulo ili waweze kusimamia kikamilifu shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
UTEKELEZAJI:
Mradi wa ujenzi wa ofisi za wakuu wa wilaya za Muleba na Biharamulo uko kwenye hatua ya upembuzi yakinifu. Aidha, utayarishaji wa michoro ya mipango miji katika maeneo zitakapojengwa ofisi zote mbili umekamilika.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
50,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
50,000,000 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
50,000,000 |
Kasma 4628: Mpango shirikishi wa utunzaji wa misitu shilingi 6,000,000 fedha za nje
LENGO
Kuratibu, kusimamia na kutoa ushauri katika halmashauri ya wilaya ya Muleba juu ya namna nzuri ya utunzaji wa misitu kwa kupitia mbinu shirikishi ili kuleta ufanisi katika utunzaji wa misitu .
UTEKELEZAJI
Fedha ya mradi ilipokelewa mwishoni mwa robo ya nne, hivyo shughuli zilizopangwa kufanyika kwa mwaka wa fedha 2010/2011 zitanyika mapema katika robo ya kwanza ya mwaka 2011/12. Aidha, shughuli zilizopangwa kufanyika ni pamoja na kuhudhuria kikao cha maandalizi ya utekelezaji wa mpango shirirkishi wa misitu kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujua wajibu wa kusimamia , kutunza na matumizi ya fedha pamoja na vitendea kazi, kuandaa mpango shirikishi wa kuhifadhi misitu, kutoa ushauri kuhusu kanuni za kuhifadhi maliasili na utekelezaji wake na kufanya ufuatiliaji wa shughuli za uhifadhi wa misitu.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
6,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
8,000,000 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
00 |
Kasma 4553: Mradi mfuko wa ngozi shilingi 3,000,000 fedha za ndani
LENGO
Ufuatiliaji wa utekelezaji mkakati wa kufufua na kuendeleza sekta ya viwanda vya ngozi katika mamlaka za serikali za mitaa .
UTEKELEZAJI
Wilaya za Karagwe, Missenyi na Chato zimetembelewa kuangalia hali ya mafunzo na ukarabati wa machinjio. Aidha, Manispaa ya Bukoba ilitembelewa kuhamasisha kuanzisha viwanda vidogo vya kusindika ngozi.
Fedha iliyo idhinishwa |
– |
shilingi |
3,000,000 |
Fedha iliyo pokelewa |
– |
shilingi |
3,000,000 |
Fedha iliyo tumika |
– |
shilingi |
3,000,000 |
|