MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO.
Mkoa umeidhinishiwa Jumla ya shilingi 30,842,785,000.00 Kati ya fedha hizo shilingi 2,217,789,000.00 ni fedha za Sekretarieti ya Mkoa na shilingi 28,624,996,000.00 ni fedha za Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
MIRADI INAYOTEKELEZWA NA KATIBU TAWALA MKOA:
Kasma 6532: Miradi ya Kujitegemea ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya Shilingi 55,000,000.00 Fedha za ndani
Mfuko wa miradi ya kujitegemea ni kati ya mifuko iliyobuniwa na serikali ili ofisi ya Mkuu wa Mkoa iweze kuchangia, harakati za Maendeleo ya wananchi wake. Mradi huu upo chini ya uangalizi na usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya.
Lengo
Katika mwaka wa fedha 2009/2010 mkoa umeidhinishiwa kutumia shilingi 55,000,000 kuchangia juhudi za wananchi kwenye shughuli zao za kujiletea Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.
UTEKELEZAJI :
Jumla ya Shule za Sekondari kumi na mbili (12), na vikundi kumi na nane (18) vya ki-uchumi na kijamii vimepatiwa msaada. Aidha Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Josia Kibira(JOKOCU) na wa Chuo Kikuu cha Karagwe, vimechangiwa jumla ya shilingi 2,600,000 kuunga mkono juhudi za kuendeleza Elimu ya juu Mkoani.
Kasma 6338: Ujenzi wa Ofisi mpya za Jengo la Mkuu wa Mkoa Shilingi 860,000, 000.00 Fedha za ndani.
Lengo:
Katika kipindi cha 2009/2010 mkoa umeidhinishiwa kutumia shilingi 860,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la ofisi ya Mkuu wa Mkoa Hatua ya awali.
UTEKELEZAJI
Michoro kwa ajili ya jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa imetayarishwa na Mhandisi mshauri na tayari imepitishwa na wakala wa majengo. Zabuni za kumtafuta Mkandarasi atakayejenga ofisi zimefunguliwa tarehe 31/03/2010 na tathimini inaendelea ili kumpata mkandarasi kwa kazi husika.
Kasma 6331: Ujenzi wa Nyumba mpya za Katibu Tawala wa Wilaya Muleba na Missenyi Shilingi 146,852,000.00 Fedha za ndani
Lengo:
Katika mwaka wa fedha 2009/2010 Mkoa umelenga kujenga Nyumba kwa ajili ya Makatibu Tawala wa Wilaya za Missenyi na Muleba.
UTEKELEZAJI
Makandarasi watakaojenga nyumba ya Katibu Tawala wa wilaya ya Muleba na Katibu Tawala Missenyi wamepatikana na wameingia mikataba ya Ujenzi wa majengo husika.
Kasma 4404: Programu ya Maendeleo ya Kilimo Wilayani (DADPS) Shilingi 126,875,000.00 ( 5,677,000.00 Fedha za ndani 121,198,000.00 Fedha za Nje )
Lengo:
Lengo kuu la mradi huu ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za miradi ya kilimo inayotekelezwa katika Halmashauri ili kutoa ushauri sahihi kuhusu maendeleo ya Kilimo.
UTEKELEZAJI:
Watendaji 48 kutoka kwenye Halmashauri tano (5) wamefundishwa jinsi ya kuandaa mipango ya maendeleo ya kilimo. Maandalizi ya sikukuu ya nane nane (08/08/2009) yalifanyika, taarifa za robo za kwanza, ya pili na ya tatu za miradi ya kilimo zimeandaliwa na kutumwa OWM-TAMISEMI. Aidha, ukaguzi wa DADPS umefanyika katika Wilaya za Missenyi, Karagwe, Chato, Muleba, Biharamulo, Bukoba Manispaa, Bukoba vijijini na Ngara. Malipo kwa ajili ya ununuzi wa gari la mradi wa kilimo yamekamilika na gari hilo linatengemewa kufika wakati wowote kabla ya mwisho wa mwezi Juni 2010.
Kasma 5404: Ukarabati wa Hospitali ya Mkoa (Grade I Ward) Shilingi 415,000,000.00 Fedha za ndani
Lengo:
Katika kipindi cha 2009/2010 Mkoa umelenga kuendeleza ujenzi wa Wodi mpya Daraja la A katika Hospitali ya Mkoa awamu ya pili.
UTEKELEZAJI :
Mkandarasi atakayejenga wodi daraja la A awamu ya pili amepatikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote baada ya kukamilisha taratibu za kutia saini Mkataba.
Kasma 6338: Ukarabati wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Shilingi140,000 ,000.00 Fedha za ndani.
Lengo:
Katika mwaka wa fedha 2009/10 Mkoa umelenga kufanya ukarabati wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kujenga mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kutoa huduma bora.
UTEKELEZAJI :
Kazi za uwekaji vigae kwenye velanda na mazingira ya nje ya jengo zimekwisha kamilika. Mkandarasi atakayejenga uzio kuzunguka ofisi sehemu ya mbele amechanguliwa na amekamilisha taratibu za kutia saini mikataba tayari kuanza kazi.
KASMA 5493. MRADI WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI ( GLOBAL FUND HIV/AIDS Prevention Project).
Shilingi 80,000, 000.00 Fedha za nje.
Lengo :
Kuratibu na kufuatilia shughuli za maafa kwenye Halmashauri zote nane (8), kufanya ufuatiliaji kwenye Halmashauri zote 8, kufanya Vikao na Wadau 50 wanaoshughulikia UKIMWIi, kufanya mafunzo ya Ukimwi kwa vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na mapambano dhidi ya UKIMWI.
UTEKELEZAJI:
Uhamasishaji jamii juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI kwa kutumia gari la sinema umefanyika katika, Halmashauri Nane za Mkoa, kwa mda wa siku nne kwa kila halmashauri. Semina juu ya namna ya kupambana na UKIMWI imefanyika kwa wafanyakazi 180 mahali pa kazi. Kamati ya UKIMWI Mkoa imefanya ufuatiliaji wa shughuli za UKIMWI zinazotekelezwa katika Halmashauri zote za mkoa.
KASMA 5499: MRADI WA KUPAMBANA NA KUDHIBITI UKIMWI. Shilingi 30,000, 000.00 Fedha za nje.
Lengo :
Kutoa msaada wa kusimamia masuala ya UKIMWI kila robo ya mwaka kwa vikundi 24 vya kuweka na kukopa (SACCOSS) na NGO's katika Halmashauri nane (8).Kufanya vikao vya nusu mwaka.
UTEKELEZAJI :
Mpango wa utekelezaji wa shughuli za mradi huu uliandaliwa na kupelekwa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na Wizara ya Fedha na Uchumi kuombea Fedha. Shughuli zilizokuwa zimepangwa kufanyika hazikutekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha.
Kasma 3217: Mradi wa Maji Vijijini (Kujenga Uwezo) Shilingi 20,000,000.00 Fedha za Nje
Lengo:
Kufuatilia na kuzijengea uwezo Halmashauri za Wilaya katika kutekeleza Mradi wa usambazaji maji vijijni na usafi wa mazingira. Kuandaa vikao vya kila robo mwaka vya wahandisi wa maji wa Wilaya na Mamlaka za maji za Wilaya, pia kuandaa taarifa ya utekelezaji kwa kila robo ya mwaka.
UTEKELEZAJI
Mpango wa kuzijengea uwezo Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa kwa sekta ya maji umekamilishwa, kazi ya kuunganisha taarifa za robo mwaka (Robo ya kwanza, pili na ya tatu) za sekta ya maji imekamilika, shughuli za ufuatiliaji na usimamizi miradi maji kwa robo ya tatu imekamilika. Uratibu wa programu ndogo ya usambazaji wa maji katika vijiji 10 kwa kila Halmashauri umefanyika, pamoja na maadhimisho ya wiki ya maji tarehe 16-22/3/2010. Vikao vya wataalamu wa maji vya kila robo mwaka vimefanyika kwa robo zote ya kwanza hadi ya tatu.
KASMA 6254: Mpango wa Maboresho ya Utumishi wa Umma Awamu ya II. Shilingi 146,789, 000.00 Fedha za nje.
Lengo:
Mpango wa Maboresho ya Utumishi wa Umma awamu ya II unatekelezwa kwa fedha za nje chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kwa kushirikiana na Wizara ya Utumishi. Mkoa wetu umeidhinishiwa Shilingi 146,789,000.00, ili kuwajengea uwezo Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa katika kuimarisha mfumo wa utunzaji kumbukumbu, ujazaji wa fomu za “OPRAS”, jinsi ya kutengeneza mpango mkakati na pia kuimarisha matumizi ya mifumo ya Kompyuta (E- Government).
UTEKELEZAJI:
Tenda kwa ajili ya kuwapata makandarasi wa kuweka miundombinu ya kompyuta, wilaya za Chato na Muleba, kuimarisha mawasiliano ya ndani ofisi ya mkuu wa Mkoa, na wa kununua Kompyuta tano (5) zimetangazwa. Mafunzo ya mfumo wa utayarishaji wa Bajeti ya Mikoa yamefanyika kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa na kwa Makatibu Tawala wa Wilaya zote. Tovuti ya Mkoa imeboreshwa na Masjala ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeboreshwa.
KASMA 5421: Mfuko wa Afya (Health Sector Basket Fund). Shilingi 227,273,000 Fedha za nje.
Lengo:
Kutekeleza Sera za Afya na kuzijengea uwezo Halmashauri (8) juu ya kusimamia utoaji bora wa huduma za Afya. Kutoa Elimu kwa watumishi juu ya maambukizi ya UKIMWI, kufanya vikao na wadau vya uhamasishaji wa kuzuia maambukizi ya UKIMWI na kuimarisha kamati za kudhibiti UKIMWI.
UTEKELEZAJI:
Shughuli za ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za afya kwenye Halmashauri zimefanyika. Taarifa za utekelezaji wa mipango ya afya ya Halmashauri kwa kipindi cha Robo ya kwanza, pili na tatu imehakikiwa na kuwasilishwa Wizara ya fedha na Uchumi na OWM-TAMISEMI. Mipango ya afya ya Halmashauri nane na Mkoa kwa kipindi cha 2010/2011 imeandaliwa.
MIRADI INAYOTEKELEZWA NA HALMASHAURI KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010
Halmashauri zimeidhinishiwa jumla ya shilingi 28,624,996,000.00 zikiwa shilingi 5,751,513,000 fedha za ndani na shilingi 22,873,483,000.00 fedha za nje.
|