JJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA MKUU WA MKOA KAGERA
     
 
     
 
 
     
 
[ Nyumbani ] au
 
USTAWI WA JAMII

Mkoa wa Kagera kama ilivyo mikoa mingine ya Tanzania unaendelea kutoa huduma za ustawi wa jamii kwa wananchi wake. Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wanaendelea kuongezeka siku hadi siku kwenye Mkoa wa kagera.

Sababu zinazopelekea kuongezeka kwa watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi ni pamoja na:- Vifo vya akina mama baada ya kujifungua, Magonjwa ya akili kwa mama akiwa na mtoto mchanga, magonjwa hasa janga la UKIMWi, Mifarakano ya familia na uteketezaji wa watoto kutokana na hali ngumu ya maisha.

Aidha Kwa kipindi cha mwaka 2010/2011, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali (mashirika ya dini, taasisi zisizo za kiserikali pamoja na watu binafsi) Mkoa unaendelea kutoa huduma za Ustawi wa Jamii katika maeneo yafuatayo:-

 

Kutoa huduma kwa makundi maalum

•  Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi

•  Watu wenye ulemavu

•  Wazee

 

Huduma kwa Watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi

Mkoa una jumla ya watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi 85,594 ambao wamebainishwa katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera. Mkoa kwa kushirikiana na taasisi za dini na mashirika ya yasiyo ya serikali unatoa huduma kwa watoto wapatao 46,376, kati yao wanawake ni 23,038 na wanaume ni 23,338.

Idadi ya watoto waliotambuliwa na Halmashuri wanazotoka imeoneshwa kwenye jedwali hapo chini:

S/N

HALMASHAURI

ME

KE

JUMLA

1.

Ngara

3,118

3,062

6180

2.

Misenyi

4,585

4,671

9256

3.

Karagwe

3,515

3,415

6,930

4.

Bukoba Manispaa

844

1,105

1,949

5.

Muleba

12,905

12,455

25,360

6.

Chato

7,600

7,252

14,852

7.

Bukoba

9,021

8,210

17,231

8.

Biharamulo

2,055

1,781

3,836

 

JUMLA

43,643

41,951

85,594

Misaada iliyotolewa ni pamoja na karo za shule, sare za shule, vyakula, nguo, sabuni matandiko ya nyumbani pamoja na matumizi mengine. Pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi mifugo mbalimbali hutolewa kwa walengwa kwa ajili ya kujiongezea kipato na kujikwamua na umasikini. Huduma nyingine ni kutoa elimu juu ya janga la UKIMWI, unafundisha staid za kazi na kilimo bora kwa kuzingatia sera ya “kilimo Kwanza ”. Baada ya kuwapatia elimu hiyo vijana pamoja na walezi wao wanapewa mbegu bora za mazao mbalimbali kwa ajili ya uzalishaji.

Taasisi na mashirika yanayotoa huduma ni TADEPA, MAPEC, WAMATA, KARADEA, SAWAKA, WOMEDA, WvT, HUYAWA Roman Catholic, Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania, Humuliza, Matumaini Mapya, PACT Tanzania, UNICEF kupitia Global Fund na mashirika mengi yaliyopo hapa Mkoani

Mkoa una jumla ya vitua na makao 16, vituo 11 ni makao ya watoto yatima, vituo 2 watoto wa mitaani, 1 ni makao ya wazee, na 2 ni makao ya walemavu. Kati ya hivyo vituo 3 vinaendeshwa na Serikali, 7 mashirika ya dini na vituo 6 vinavyoendeshwa watu binafsi.

Huduma kwa wazee

Mkoa una kituo kimoja cha kutunza wazee ambacho kiko chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii. Kituo kina jumla ya wazee 17 kati yao wanawake 7 na wanaume 10 .

Mkoa unatoa huduma ya matibabu bure kwa wazee kwenye kila kituo cha kutolea huduma za afya.

Huduma kwa familia zenye matatizo

Huduma iliyotolewa ni pamoja na ushauri nasaha, kupewa matibabu na kulipiwa bima za afya, na kutembelea familia ili kutoa ushauri katika familia husika.

Kipindi cha Julai 2010 hadi Juni 2011 Mkoa umepokea jumla ya mashauri 24 ya ya ndoa, mashauri 31 ya matunzo nje ya ndoa , mashauri 1 7 ya kunyang'anywa watoto. Mashauri hayo yalishughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na wahusika waliridhika na utatuzi huo isipokua mashauri saba ya ndoa, na mashauri 3 ya kunyang'anywa watoto yalipelekwa mahakamani ili kutolewa uwamuzi wa kisheria.

 

 
 
 
 

 

 
 
 

 

 
 
 
 

Bi. Rebbeca Gwambasa----Afisa Ustawi wa Jamii-Mkoa wa Kagera

Huduma kwa watu wenye ulemavu

Mkoa umehakikisha kwamba jamii ya watu wenye ulemavu wanalindwa na kupewa haki ya kuishi kama raia wengine, Mkoa umezitaka Halmashauri na Serikali za vijiji kuhakikisha kwamba walemavu wote, hasa wa ngozi (Albino) wanalindwa na kuhifadhiwa dhidi ya wauaji

Idadi ya walemavu waliotambuliwa na Halmashuri wanazotoka imeoneshwa kwenye jedwali hapo chini:

S/N

HALMASHAURI

ME

KE

JUMLA

1.

Bukoba Manispaa

269

253

522

2.

Muleba

130

300

430

3.

Missenyi

215

500

715

4.

Bukoba Vijijini

125

300

425

5.

Chato

-

-

-

6.

Ngara

233

650

883

7.

Biharamulo

303

325

628

8.

Karagwe

420

520

940

 

JUMLA

1695

2848

4543

Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa ambayo ilikumbwa na wimbi la mauaji na mashambulizi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) tatizo la mashambulizi na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kwa Mkoa wa Kagera lilijitokeza mwezi septemba mwaka 2008. wilaya ambazo tatizo hili lilijitokeza ni Ngara, Biharamulo Muleba na Karagwe. Mkoa ulipoteza watu wenye ulemavu wa ngozi wapatao 5 na mmoja alikatwa viungo vya mwili wake na kuwa kilema wa maisha, sababu kubwa zilizojitokeza kuhusiana na tatizo hili ni imani potopfu ya baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa viungo vya binadamu wenye ulemavu wa ngozi vinasaidia kupata utajiri.

Mkoa ulifanya jitihada ya kuwaelimishwa kuhusu kuwalinda walemavu wa ngozi kuachana na imani za kishirikina zinazosababisha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, na kila kijiji kimeagizwa kuwatunza albino waishio katika vijiji vyao.

MAFANIKIO

•  Mkoa umefanikiwa kutoa huduma za matibabu bure kwa wazee wanaofika hospitali mbalimbali hasa Hospitali ya mkoa na hospitali za Wilaya.

•  Kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Walemavu, Mkoa wa Kagera umefanikiwa kuunzisha Mfuko wa watu wenye ulemavu (Walemavu Trust Fund) ili kuwasaidia walemavu kuendesha shughuli mbalimbali.

•  Mkoa umefanukiwa kuwaweka pamoja watoto walemavu wa ngozi (Albino) kwenye shule ya msingi ya Mugeza mseto kwa ajili ya usalama wao, pamoja na kupatiwa elimu kama watoto wengine.

•  Kuimarisha ushirikiano na taasisi mbalimbali na mashirika ya dini katika kutoa huduma mbalimbali kwa makundi maalum.

CHANGAMOTO ZINAZOKABILI SEKTA YA USTAWI WA JAMII

  • kwa kuwa makundi hayo yanaongezeka kwa kasi kwenye jamii yetu, Hakuna takwimu sahihi za walemavu, wazee, watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
  • Jamii haijapata mwamko katika kuchangia fedha katika mifuko ya kusaidia watoto walio katika mazingira magumu.
  • Uwezo mdogo na umasikini unasababisha wazazi/walezi kutelekeza familia zao kwa sababu wanashindwa kuzihudumia.
  • Hakuna ufadhili endelevu hivyo kusababisha baadhi ya viyuo kukosa mahitaji muhimu kwa ajili ya watoto.

 

MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO HIZI:-

•  Kutambua watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, walemavu na wazee ili kupata takwimu sahihi kwa kuwa makundi hayo yanaongezeka kila siku kwenye jamii yetu.

•  Kutayarisha maeneo yatakayotumika kutoa huduma za afya kwenye vituo vyote vinavyotoa huduma ya afya na kuwa na watoa huduma kwa ajili ya kwa wazee.

•  Kuhamasisha Jamii juu ya kutambua umuhimu wa kuchangia mfuko wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

•  Kushauri wananchi kuunda vikundi ili wapate mafunzo ya ujasiriamali kusudi waweze kujikwamua katika umasikini.

•  Kuelimisha jamii kuondokana na mila potofu zinazopelekea mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino), yatokanayo na imani potofu za utafutaji mali.

 
 

 

 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
[ Rudi nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2008 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, BUKOBA, TEL: 028 - 2220215/17, FAX: 0282752184